Saturday, February 4, 2017

DKT NCHIMBI AAGIZA MAAFISA KUSIMAMIA MIRADI INAYOTEKELEZWA WALENGWA WA TASAF

Na Gasper Andrew- Singida.


Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi ameagiza maafisa mifugo kata kusimamia kwa karibu miradi ya ufugaji kuku na mbuzi inayotekelezwa na kaya maskini zilizopo kwenye mpango wa TASAF 111.

Amesema kuku au mbuzi katika miradi hiyo wakifa kwa kukosa huduma kutoka kwa maafisa mifugo,maafisa hao watalazimika kufidia kuku au mbuzi hao watakaokufa.

Akilijengea nguvu agizo lake hilo Dkt. Nchimbi alitoa kutoka mfukoni kwake shilingi 150,000 taslimu na kumpatia afisa mifugo kata ya Kikonge Wilayani Iramba kwa ajili ya kuikarabati pikipiki yake iweze kumrahihishia kufika kwenye miradi ya kaya maskini.

Dkt. Nchimbi ametoa agizo hilo juzi muda mfupi baada ya kumaliza kukagua bwawa la kijiji cha Kikonge wilaya ya Iramba linalojengwa kwa nguvu za kaya maskini.Amesema serikali pamoja na wadau wanaotoa fedha kwa kaya maskini,ili ,ziweze kujikwamua kutoka lindi la umaskini.

“Njia mojawapo ya kuzisaidia kaya hizi maskini kuboresha vipato vyao,ni hii ya miradi midogo midogo ya ufugaji kuku,mbuzi na mifugo meinge.Ninyi maafisa mifugo ambao mpo karibu na kaya hizi,zisimamieni kikamilifu,msisubiri mfuatwa,ninyi ndio muifuate miradi huko iliko”,alisisitiza.Aidha, mkuu huyo wa mkoa, amewataka watendaji hao wahakikishe wana simamia watoto wa kaya maskini wana hudhuria shuleni bila kukosa.

“Serikali inaamini hawa watoto wa kaya maskini ambao TASAF inagharamia masomo yao, ndiyo watakao kuja kuwa mtaji kwa kaya maskini kujikomboa kiuchumi. Kwa hiyo upo umuhimu mkubwa wa kusimamimiwa na kuhimizwa kusoma kwa bidii”,alifafanua.

Mkuu huyo wa mkoa, pia amewataka walimu watambue kwamba wana fundisha watoto ambao wengine wakiwa ni wa kaya maskini,.Kwa hali hiyo, mchango wao unatakiwa katika kuwa jengea misingi itakayo weza kusaidia kuzikomboa kiuchumi kaya zao.

Awali mratibu TASAF mkoa wa Singida, Patrick Kasango, alisema mpango wa kunusuru kaya maskini (PSSN) unatekelezwa na TASAF 111, katika wilaya zote sita za mkoa huu.Alisema mpango huo ulianza na kaya 39,426, lakini kutokana na sabaubu mbalimbali hadi sasa zimebaki kaya lengwa 39,102.

“kaya hizi maskini zimewezeshwa kupata mahita ya msingi ikiwemo chakula hasa wakati wa njaa, mahudhurio shuleni yameboresha kwa wanafunzi na kuboresha afya za watoto wadogo wanaodhuziria kliniki.Kwa kifupi,hadi januari mwaka huu, zaidi ya shilingi 20.3 bilioni, zimehawilishwa kwa kaya masikini mkoani kwetu”,alisema Kasango.

Wakati huo huo Mmoja wa wanaufaikaji wa mpango huo wa TASAF 111,Elizabeth Mkumbo,amesema amefanikiwa kujenga nyumba bora,kuwa na akiba na kuanzisha ufugaji wa kuku kupitia fedha za mradi wa TASAF 111.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (anayeangalia kamera) akimpatia Nya Mathias shilingi 34,500 kama malipo ya kuchimba bwawa kwa siku 15 ambapo kila siku anapaswa kulipwa shilingi 2,300. Fedha hizo zimetolewa na TASAF 111 kwa ajili ya kunusuru kaya maskini kupitia miradi ya jamii iliyoibuliwa na walengwa wa TASAF.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akiangalia bwawa linaloendelea kuchimbwa na kaya maskini za kijiji cha Kikonge wilaya ya Iramba kupitia TASAF 111. Mkuu huyo wa mkoa ameagiza halmashauri zote zisaidie kutoa fedha ili ujenzi wa mabwawa yaliyoibuliwa na kaya masikini yaweze kukamilika kwa muda mfupi.
Mkazi wa kijiji cha Kikonge wilaya ya Iramba Mkoani Singida Stephano Mkiya akizungumza muda mfupi kabla ya zoezi la kuhaulisha fedha za TASAF 111 za kunusuru kaya maskini amesema kupitia fedha za TASAF ameweza kuanzisha ufugaji wa mbuzi na pia anamudu kuwasomesha watoto wake.
Mkazi wa kijiji cha Kikonge wilaya ya Iramba Mkoani Singida Elizabeth Mkumbo akizungumza muda mfupi kabla ya zoezi la kuhaulisha fedha za TASAF 111 za kunusuru kaya maskini, Elizabeth amesema kupitia fedha za TASAF ameweza kujenga nyumba bora ya mabati na kwa sasa ana uhakika wa chakula tofauti na kipindi hajaunganishwa na mpango wa TASAF.
Mratibu wa TASAF Mkoani Singida Patrick G. Kasango akizungumza muda mfupi kabla ya zoezi la uhaulishaji wa fedha za TASAF 111 za kunusuru kaya maskini 146 katika kijiji cha Kikonge wilaya ya Iramba mkoani hapa. Kwa mujibu wa Kasango hadi sasa kaya 39,102 maskini Mkoa wa Singida zimenufaika kwa kupatiwa zaidi ya shilingi bilioni 20.3.

No comments:

Post a Comment