Monday, February 6, 2017

CCM KIGOMA YAVUNA WANACHAMA WAPYA 868 AKIWEMO MWENYEKITI WA CHAMA CHA ACT-WAZALENDO NA CUF WILAYANI KAKONKO




CHAMA Cha CCM Mkoa wa Kigoma kimevuna jumla ya Wanachama wapya 868 kutoka vyama mbalimbali vya siasa akiwemo mwenyekiti wa chama cha ACT-Wazalendo Venasi Busunzu wa wilaya ya Kakonko na Mwenyekiti wa CUF Kilembwe Omari mgombea udiwani kata ya Sinuka wamekabidhiwa kadi ya chama hicho jana, katika hitimisho ya sherehe za madhimisho ya kutimiza miaka 40 ya CCM.

Akihitimisha sherehe hizo jana zilizo fanyika Kimkoa Katika kijiji cha Mwakizega Wilayani Uvinza Mwenyekiti wa CCM kigoma Amani Kabourou , alisema katika maazimisho waliyafanya Mkoa mzima katika Wilaya zote walipatikana wanachama wapya 726 na kutoka vyama vya upinzani ni wanachama 146 ambao walikabidhiwa kadi katika sherehe za maazimisho zilizo fanyika jana katika Kijiji cha Mwakizega kata ya Mwakizega Wilaya ya Uvinza.

Alisema wanachama hao Waliamua kurudi katika Chama hicho kutokana na Shughuli kubwa zinazo fanywa na chama hicho , ambapo mpaka sasa kuna Maendeleo Makubwa yaliyo fanyika katika Kipindi cha Mwaka mmoja cha uongozi wa serikali unaongozwa na Serikali ya Chama cha Mapinduzi.

Kabourou alisema Kwa sasa Viongozi wa chama hicho wameweka mikakati wa kukisafisha chama hicho kwa kuondoa viongozi wote wasio na sifa wanaokichafua sana na kuifanya CCM kuwa mpya na Serikali mpya kutokana na Misingi iliyo wekwa na waanzirishi wa Chama hicho.
Akizungumzia hatua hiyo, aliyekuwa mwenyekiti wa ACT wazalendo Bususnzu alisema amegundua mapungufu makubwa katika chama cha awali hali ,iliyomshawishi kujiunga na ccm ni pamoja na viongozi kuhamasisha misuguano kwa jamii ,ili nchi isitawalike lakini kwa awamu ya serikali ya wamu ya tano ya John Magufuli ni kigezo cha upinzani kukubali uwajibikaji wake wenye tija kwa wananchi.

Akizungumzia hilo Kilembwe Omari alisema amerudi kundini akiwa na wananchama 34 kutoka chama cha ACT wazalendo ,akidai amerudi kwa baba na mama yake akiwa na wenzake hao,sababu aminiye na kubatizwa ameokoka na anatumaini atakuwa mumini mzuri wa chama hicho.

Akiongezea hilo Aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF,wilaya ya Kakonko Amana Ramadhani alisema anapokea kadi kwa hiari japokuwa amekulia katika upinzani akiwa mwenyekiti wa kina mama kwa miaka 15 wa chama cha CUF,kwa sababu ya sera zake akijua kitawakomboa wananchi,kumbe kipo kwa ajili ya kupata ruzuku ya serikali.

Alisema tangu mwaka 1990 wapo wanachama wawili hali inayokwamisha jitihada za kuleta maendeleo ,awali aliamini ujio wa UKAWA ni kuimarisha vyama lakini kilichotokea ni ubaguzi wa udini na kugombea maslai binafsi na si wananchi,hivyo hana budi kujiunga na ccm ili kutimiza ndoto za kuinua uchumi .

Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Emanuel Maganga alisema kwa awamu ya tano ya serikali ya leo,imetatua kero mbalimbali za wananchi,hususani katika sekta ya elimu kigoma imepiga hatua 2015/16 wilaya ya kakonko ilishika nafasi ya kwanza matokeo ya kidato cha pili na kidato cha sita kigoma ilishika nafasi ya kwanza kitaifa.

Maendeleo hayo ni pamoja na sekta ya miundombinu ya barabara ,miradi ya maji zimetengwa kiasi cha sh.milioni 10 kwa kila wilaya ya kigoma kwa ajili ya kukamilisha miundombinu ya maji iliyokuwa ikisuasua sanjari na umalizwaji wa barabara ya Kidahwe hadi kasulu na nyakanazi Kakonko huku Uvinza hadi Tabora fungu la fedha zimepangiwa bajeti katika mwaka wa 2016/17.

No comments:

Post a Comment