Friday, January 13, 2017

ZIARA YA MSIMAMIZI WA CADESE KATIKA MRADI WA UMEME JUA WA MAJARIBIO, HOSPITALI YA WILAYA NYAMAGANA, MWANZA


Mratibu wa Mradi wa Umeme Jua wa Majaribio katika hospitali ya wilaya ya Nyamagana, Amin Abdallah (kushoto mbele) akimwongoza Msimamizi wa Mradi wa Kuwajengea Uwezo Wataalam wa Nishati na Tasnia ya Uziduaji (CADESE), Paul Kiwele (kulia mbele) pamoja na wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini katika ziara kwenye mradi huo.
Mratibu wa Mradi wa Umeme Jua wa Majaribio katika hospitali ya wilaya ya Nyamagana, Amin Abdallah (kulia) akielezea mfumo wa kuongozea vifaa vya umeme jua katika hospitali ya wilaya ya Nyamagana.
Mratibu wa Mradi wa Umeme Jua wa Majaribio katika hospitali ya wilaya ya Nyamagana, Amin Abdallah (kushoto) akionesha mita maalum ya kuruhusu umeme kuingia na kutoka kwenye Gridi ya Taifa.
Mratibu wa Mradi wa Umeme Jua wa Majaribio katika hospitali ya wilaya ya Nyamagana, Amin Abdallah ( wa pili kutoka kulia) akionesha karabai zinazotumia umeme jua zilizotolewa na mradi huo kwa wavuvi wa soko la samaki la Mwaloni jijini Mwanza.
Mmoja wa wavuvi katika soko la samaki la Mwaloni jijini Mwanza, Joseph Athony (kushoto) akielezea manufaa ya karabai zinazotumia umeme jua zilizotolewa na Mradi wa Umeme Jua wa Majaribio.

Sehemu ya wodi za wagonjwa katika hospitali ya wilaya ya Nyamagana iliyofungwa umeme jua.
Mratibu wa Mradi wa Umeme Jua wa Majaribio katika hospitali ya wilaya ya Nyamagana, Amin Abdallah, (kulia) akielezea maendeleo ya mradi huo kwa Msimamizi wa Mradi wa Kuwajengea Uwezo Wataalam wa Nishati na Tasnia ya Uziduaji (CADESE), Paul Kiwele ( wa pili kutoka kulia). Wengine ni  wataalam kutoka Sehemu ya Nishati Jadidifu, Wizara ya Nishati na Madini.
Mratibu wa Mradi wa Umeme Jua wa Majaribio katika hospitali ya wilaya ya Nyamagana, Amin Abdallah (kulia) akieleza jambo kwa Mtaalam kutoka Sehemu ya Nishati Jadidifu- Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Stephan Kashushura (katikati). Kushoto ni Nasra Mohamed kutoka  Wizara hiyo.

No comments:

Post a Comment