Thursday, January 19, 2017

WAZIRI NAPE:NITARUDISHA HESHIMA YA KAZI ZA WASANII NCHINI

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

WAZIRI Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye,amesema kuwa anafanya harakati za kapambana na kazi za wasanii ziweze kupata heshima na pamoja na masilahi kwa wasanii hao hili waweze kujiongeza kipato.

Nape ameyasema hayo leo wakati alipokutana na Wasanii juu ya masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya filamu, amesema wasanii wanafanya kazi ngumu lakini hawanufaiki na kazi wanayoifanya huku jamii ikiona mafanikio.

Amesema katika kazi za filamu ziweze kupata heshima kunahitajika kutengeneza sera ambayo itamaliza malalamiko ya wasanii na wawekezaji wanaweza kuwekeza katika katika sekta hiyo.

Nape amesema kuna watu wanakuja kutaka kuwekeza katika sekta ya filamu kutokana na kutokuwepo kwa sera wawekezaji hao wanakimbia na kwenda nchi nyingine zilizoweka sera.Aidha amesema kupatikana kwa sera kutapunguza maharamia wanaofanya kazi wasanii na kujipatia kipato kikubwa kuliko wale wanaofanya kazi halisi.

"kazi za wasanii ambazo hazina stika ziko katika maghala ya TRA na kati hizo za wasanii zina kesi mahakamani.Nape amesema katika juhudi hizo kumekuwa na maneno kwa baadhi ya wasanii ya kumpiga vijembe huku akiwa anafanya kazi ya kukamata kazi hizo kwa gharama yake mwenyewe" amesema Waziri Nape.

Hata hivyo amesema katika kupambana na maharamia baadhi ya wasanii wanashirikiana na ambao wameshiriki mkono na taarifa zote za mkutano huo wanaupata lakini hatajali na operesheni zingine zitaendelea.

Hata hivyo ameitaka baraza la Sanaa la Taifa Basata kusajili kazi za wasanii licha ya kuwepo kwa sheria za ovyo ovyo.Katika Mkutano huo ubwabwa ulionunuliwa kwa wasanii na kuliwa uwanja wa taifa unadaiwa kutolewa na maharamia wa kazi za wasanii ambapo Waziri Nape amepinga kuwa hakuna kitu kama hicho.

Waziri nape amewatahadharisha wasanii ambao wanajiona wana majina na kushindwa kushiriki mkutano huo na kufanya wasanii waliofika kuwa wao ndio wanashida huku akitaja kuwa jambo hilo ni la wasani wote hivyo kila mtu anapaswa kushiriki.
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akiongea na wadau katika sekta ya filamu alipokutana nao leo kujadili changamoto za sekta hiyo na jinsi ya kupambana na maharamia wa kazi za wasani na kuwatoa hofu juu ya wasiwasi wao wa Mali zilizowahi kukamatwa kuwa zimerudishwa kwa wahusika. 
Wadau wa Sekta ya Filamu wakimsikiliza Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye alipokutana nao leo Jijini Dar es salaam. 
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akimsikiliza Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Bw. Simon Mwakifamba 
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akiangalia kazi haramu za wasanii zilizokamatwa kwa wasambazaji zilizopo katika ghala la kampuni ya madalali ya YONO iliyopo Ilala Bungoni. 
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akiangalia mashine ya kudurufu santuri za muziki na video wasambazaji zilizopo katika ghala la kampuni ya madalali ya YONO iliyopo Ilala Bungoni. 
Baadhi ya Wasanii wakiangalia kazi haramu za wasanii zilizokamatwa kwa wasambazaji zilizopo katika ghala la kampuni ya madalali ya YONO iliyopo Ilala Bungoni. 

No comments:

Post a Comment