Sunday, January 29, 2017

WAONGOZA UTALII / WABEBA MIZIGO YA WATALII WATOA KILIO KWA SERIKALI

Katibu wa chama cha waongoza Watalii (TTGA)akiwa anazungumza na waandishi wahabari na wadau wa utalii katika kongamano Utalii mambo ya utalii na uhifadhi kwa waandishi wa habari na wadau wa utalii katika ukumbi wa Palace Hotel 28 January 2017.
Katibu wa wabeba mizigo ya watalii (porters)Loshiye Mollel kongamano Utalii mambo ya utalii na uhifadhi kwa waandishi wa habari na wadau wa utalii katika ukumbi wa Palace Hotel 28 January 2017.Picha na Vero Ignatus Blog
Afisa Utalii Mkoa wa Arusha Florah Bazili akiwasilisha mada wakati huohuo akijibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa na waandishi wa habari pamoja na wadau wa utalii.
Katibu wa jukwaa la wahariri Nevilly Meena akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wadau wa utalii katika kongamano hilo.
Jumapili Chenga kutokA Mjumuiko wa Maliasili Tanzania akiwasilisha mada katika kongamano hilo leo tarehe 28 januari 2017. 
Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari Mkoani Arusha Cloud Gwandu akichangia mada katika kongamano la Utalii mambo ya utalii na uhifadhi kwa waandishi wa habari na wadau wa utalii katika ukumbi wa Palace Hotel 28 January 2017.Picha na Vero Ignatus Blog.
Wadau wa Utalii wakiwa katika kongamano hilo kwaajili ya kubadilishana uzowefu .
Mmiliki wa blog ya jamii Pamella Molle akifuatilia kwa makini yanayoendelea katika kongamano hilo la mambo ya utalii kwa waandishi wa habari na wadau wa utalii.Picha na Vero Ignatus Blog
Aliyevaa tisheti nyekundu Andrew Ngobole Mkuu wa chuo cha uandishi wa habati na utangazaji Arusha (AJTC)Akifuatilia yanayoendelea katika kongamano hilo la mambo ya utalii kwa waandishi wa habari na wadau wa utalii leo.Picha na Vero Ignatus Blog.
Mwandishi wa kituo cha Luninga cha Azam Iddy Uwesu akifuatilia kwa mkini mada zilizokuwa zikiendelea katika kongamano hilo.

Na.Vero Ignatus Arusha. 


Waongoza utalili wanaosaidia watalii kupanda milima wameiomba serikali kutazama upya malipo wanayopewa katika utekelezaji wa kazi zao kwasababu hayalingani na ugumu wa kazi wanazofanya kuhudumia watalii.Kwa sasa waongoza watalii hao wanalipwa wastani wa kiwango cha dola 10 za kimarekani kwa siku ,kiasi ambacho hakilingani na kazi wanazozifanya.

Hayo yamesemwa na katibu wa waongoza watalii Immanuel Mollel katika sa kongamano la mambo ya utalii na uhifadhi kwa waandishi wa habari na wadau wa utalii inayofanyika kwa siku mbili katika hotel ya Palace iliyopo Jijini Arusha.

Katibu huyo amezitaja changamoto mbalimbali ambazo wanazipitia ni pamoja na kukosa mikataba ya ajira, wao kulazimika kununua leseni ili waweze kuwaongoza watalii, uharibifu wa mazingira na tabia nchi pamoja na ujangili. Kwa upande wake Katibu wa chama cha wabeba mizigo ya watalii Loshiye Mollel amesema changamoto kubwa wanazozipata ni pamoja na mazingira magumu wanayokabiliana nayo katika utendaji kazi wao.

“wakati tunapokuwa mlimani umebeba mzigo wa mgeni kuna magonjwa ya mlimani ,sasa namna ya kumuokoa huyu mbeba mizigo ya mtalii ni shida sana ,kwani itawalazimu wale ambao wapo kule juu mlimani wakushushe kwa machela hadi chini ,huko napo unakutana na changamoto nyingine hakuna gari kwani magari yapo mawili tu"

"Tupo wabeba mizigo zaidi ya 28,000,kwa siku moja tunakuwa mlimani zaidi ya wabeba mizigo (porters) 4000 au 3000,tunaiomba serikali kutuongezea magari ili kuwepo urahisi wakati wa kumsaidia mbeba mizigo ya watalii anapopata shida akiwa mlimani) mlimani,a

No comments:

Post a Comment