Saturday, January 28, 2017

TAMASHA LA "MAJIMAJI FLAVA" LAFANA

Kaimu Mkurugenzi Kitengo cha Sanaa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bibi. Leah Kihimbi ambaye alimwakilisha Mhe. Waziri Nape Nnauye akitoa maoni yake kuhusiana na igizo la Tamasha la "MajiMaji Flava" ambalo lilionyesha baadhi ya matukio ya ukatili yaliyofanywa na Wajerumani enzi za ukoloni dhidi ya watu weusi. Tamasha hilo lilifanyika jana 27/01/2017 Makumbusho ya Taifa, Jijini Dar es Salaam.

Waigizaji wa Tamasha la "MajiMaji Flava" wakielimisha jamii kwa vitendo juu ya baadhi ya matukio yaliyowahi kutokea wakati wa kipindi cha ukoloni wa Wajerumani nchini Tanzania 27/01/2017 katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wageni waalikwa toka mataifa mbalimbali wakishuhudia maigizo mbalimbali wakati wa Tamasha la "MajiMaji Flava" ambalo lilionyesha baadhi ya matukio ya ukatili yaliyofanywa na Wajerumani enzi za ukoloni dhidi ya watu weusi. Tamasha hilo lilifanyika jana 27/01/2017 Makumbusho ya Taifa, Jijini Dar es Salaam.


Waigizaji kutoka Ujerumani na Tanzania wakiigiza namna baadhi ya matukio wakiyoyafanya Viongozi mbele ya Wananchi kipindi cha ukoloni kilichopelekea watu wengi kupoteza maisha wakati wa vita vya maji maji.


Waigizaji kutoka Ujerumani na Tanzania wakitoa burudani ya muziki wakati wa "Tamasha la MajiMaji Flava" lililofanyika jana 27/01/2017 Makumbusho ya Taifa, Jijini Dar es Salaam.
(Picha zote na Benedict Liwenga-WHUSM)

No comments:

Post a Comment