Wednesday, January 11, 2017

SERIKALI KUFANYA MAPITIO YA SHERIA YA SEKTA YA SANAA NA BURUDANI –WAZIRI NAPE

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

WAZIRI wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye amesema wanatarajia kufanya mapitio ya sheria zinazohusu sekta ya sanaa na burudani nchini ili kutoa fursa kwa taasisi binafsi kuwekeza zaidi.

Katika kufanya mapitio hayo wataangalia jinsi ya kufanyia kazi sheria mbovu zinazokandamiza sekta ya sanaa na burudani nchini na kuziondoa kabisa ili kuleta manufaa kwa wasanii na wadau wanaohusika na sanaa.

Nape ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa akizindua rasmi urushwaji wa matangazo ya Kombe la mataifa Afrika (AFCON) pamoja na kumkabidhi bendera kwa msanii wa Bongofleva Nasib Abdul(Diamond Platnum) anayekwenda kutumbuiza katika ufunguzi wa mashindano hayo yatakayofanyika Januari 14 nchini Gabon.

Amesema wasanii na watu wengine kwenye sanaa wamekuwa wakifanya kazi kwa juhudi kubwa licha ya kutofaidika na kazi wanazozifanya na hatimaye wakijikuta wakiwa chini kadri siku zinavyozidi kwenda mbele.

Amesema serikali imedhamiria kushughulikia masuala yote yanayofanya wasanii na wadau wngine kuwa wanyonge kutokana na uwepo wa sheria hizo.

‘Natambua Kampuni ya Multichoice kupitia king’amuzi chake cha DStv katika kuhakikisha wanakuza na kuendeleza masuala ya michezo na burudani nchini, na sisi kuonesha tunaunga mkono jitihada zao tutapitia sheria zote ambazo zimekuwa ni kikwazo kwenye ukuzaji tasnia ya sanaa hapa nchini’ amesema Nape.

Nape alimpongeza Diamond Platnum kwa kupata nafasi ya kwenda kutumbuiza katika mashindano hayo na kudai kuwa kitendo hicho kinaipa faraja Tanzania licha ya kuwa hawajapeleka timu katika mashindano hayo makubwa barani Afrika.

Nae Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Multichoice Tanzania, Salum Salum amesema watanzania wataweza kujioneamashindano hayo Mubashara kutoka nchini Gabon kupitia king’amuzi chao cha DStv kwenye kifurushi cha bei ya chini cha Shilingi 19,975 pekee.

Amesema kampuni hiyo itagharamia tiketi za watu sita kutoka kundi la WCB ili kufanikisha adhma ya msanii Diamond Platnum kufanya shoo yenye uwezo wa kuijulisha dunia kuwa Tanzania inavipaji vingi vya uimbaji mziki licha ya kutopewa sifa katika baadhi ya maeneo mengine.

Aidha Salum amesema mashindano yatakuwa yakionyeshwa mubashara(Live) ili kuweza kutoa fursa ya watanania na kujikita zaidi kwenye michezo ili na wao wapate nafasi ya kushiriki mashindano hayo katika kipindi cha miaka ijayo.
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye akizungumza wakati wa hafla ya kumkabidhi bendera kwa msanii wa Bongofleva Nasib Abdul(Diamond Platnum) anayekwenda kutumbuiza katika ufunguzi wa mashindano hayo yatakayofanyika Januari 14 nchini Gabon iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye, akimkabidhi bendera msanii wa Bongofleva Nasib Abdul(Diamond Platnum) anayekwenda kutumbuiza katika ufunguzi wa mashindano yatakayofanyika Januari 14 nchini Gabon iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Multichoice Tanzania, Salum Salum akizungumza wakati hafla ya kumkabidhi bendera msanii wa Bongofleva Nasib Abdul(Diamond Platnum)anayekwenda kutumbuiza katika ufunguzi wa mashindano yatakayofanyika Januari 14 nchini Gabon iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Msanii wa Bongofleva Nasib Abdul(Diamond Platnum) anayekwenda kutumbuiza katika ufunguzi wa mashindano yatakayofanyika Januari 14 nchini Gabon akizungumza na waandishi habari juu ya safari hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Balozi DSTV, Joti akizungumza wakati wa hafla ya kumkabidhi bendera msanii wa Bongofleva Nasib Abdul(Diamond Platnum) anayekwenda kutumbuiza katika ufunguzi wa mashindano yatakayofanyika Januari 14 nchini Gabon iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.


No comments:

Post a Comment