Monday, January 9, 2017

MWAKYEMBE ATEMBELEA MAHAKAMA MAALUM YA RUSHWA NA UHUJUMU UCHUMI

 Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe akiangalia chumba cha kuendeshea kesi katika mahakama ya makosa ya rushwa na uhujumi uchumi alipoitembelea leo
 Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe akiangalia chumba cha kuendeshea kesi katika mahakama ya makosa ya rushwa na uhujumi uchumi alipoitembelea leo
  Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe akimsikiliza kaimu mkuu wa mahakama hiyo Kanda ya Dar es Salaam Mhe. Jaji Winnie Koroso alipokuwa akiatoa taarifa ya utendaji wa mahakama hiyo  alipoitembelea leo
 Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe akizungumza baada ya kufanya ziara katika Mahakama malum ya makosa ya Rushwa na Uhujumu uchumi Kanda ya Dar es Salaam leo
Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe akiangalia kitabu ambacho huingizwa orodha ya mashauri yaliyofunguliwa katika Mahakama maalum ya makosa ya rushwa na ufisadi alipoitembelea leo.



Waziri wa mambo ya katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe ametembelea Divisheni Maalum ya Mahakama inayojishughulisha na makosa ya rushwa na uhujumu uchumi nchini Kanda ya Dar es Salaam na kujionea namna inavyoendesha shughuli zake.

Akizungumza katika ziara hiyo Waziri Dkt Mwakyembe amewataka watendaji wa mahakama hiyo kuzingatia lengo la uanzishwaji wa mahakama hiyo ili kuleta tija na ufanisi uliofanywa kuanzishwa kwake.

“Mahakama hii ni chombo maalum kilichoundwa ili kushughulikia masuala ya rushwa na uhujumu uchumi ndani ya muda mfupi, nyinyi kama watendaji hamna budi kuongeza bidii na kuhakikisha mashauri yote yanayoletwa katika mahakama hii yanamalizika ndani ya muda mfupi huku mkizingatia haki za kila mmoja na hivyo kufanikisha lengo la kuanzishwa kwake ”,alisema Dkt Mwakyembe

Aidha alisema uanzishwaji wa mahakama hiyo ulilenga kuifanya Tanzania kupunguza utendaji wa makosa ya aina hiyo au kuyamaliza kabisa na kuongeza kuwa kwa hali ilivyo sasa inaonekana kuwa uhalifu wa aina hiyo umepungua.

Kutokana na kupungua kwa makosa hayo mhe. Waziri alisema anafikiria kuandaa mpango wa kupunguza kiwango cha gharama za makosa ambayo yatapelekwa mbele ya mahakama hiyo . “Inaonekana yale makosa ya ufisadi mkubwa hakuna kwa sasa na hili no moja ya lengo la kunazisha mahakama hii na kwa hali hiyo nafikiria kuja na mpango wa kupunguza kiwango cha thamani ya makosa ambayo kitakuwa ni chini ya kile kilichowekwa awali cha sh. Bilioni moja,” alisema Dr. Mwakyembe.

Akizungumza katika kikao hicho Kaimu Mkuu wa Mahakama hiyo Maalum Mhe. Jaji Winnie Korosso alisema mahakama hiyo ina uwezo wa kupunguza kiwango cha thamani ya makosa husika yanayopaswa kupelekwa na kuongeza kuwa mahaklama hiyo pia inao uwezo wa kusikiliza kesi zote zinazohusiana na nyara za serikali bila ya kujali thamani yake.

“Mahakama hii inao uwezo wa kupunguza kiwango cha thamani ya mashitaka yanayoletwa hapa, pia ijulikane wazi kuwa mashitaka yote yanayohusu nyara za taifa yanaweza kuletwa katika mahakama hii wakati bila ya kujali thamani yake,”alisema Mhe. Koroso 

Akiongelea utendaji kazi wa mahakama hiyo Mhe Jaji Koroso alisema mpaka sasa mahakama hiyo imeshasikiliza maombi ya dhamana tisa ambapo sita yameshafanyiwa kazi na maombi mengine yanaendelea kushughulikiwa. 

Amesema mahakama hiyo iko katika kanda zote 14 za Mahakama Kuu nchini na hivyo mashauri yanayostahili kusikilizwa na mahakama hiyo yanaweza kupokelewa na kusikilizwa nchi nzima kupitia kanda hizo na sio kwam,ba iko Dar es Salaam pekee.

Aliasema kwa kuwa mahakama hiyo ni maalum mashauri yanayopelekwa yanatakiwa yawe yamemalizika ndani ya miezi tisa (9) na hivyo hazina budi kuendeshwa kwa haraka ili kufanikisha lengo la kusikilizwa kwa haraka na hivyo kusaidia taifa.

No comments:

Post a Comment