Saturday, January 7, 2017

MPOGOLO AZINDUA MATEMBEZI YA UVCCM, ZANZIBAR LEO


Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akizungumza kabla ya kuzindua matembezi ya UVCCM ya miaka 52 ya CCM, kwenye Viwanja vya Donge, Vijibeni, Wilaya ya Kaskazini Jimbo la Donge, mkoa wa Kaskazini Unguja.

Vijana wakihamasika na kuonyesha kuwa tayari kuanza matembezi ya UVCCM ya miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibara, baada ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, kutoa maneno yaliyoshiba nasaha, wakati wa hotuba yake ya kuzindua matembezi hayo leo.

Mpogolo akikabidhi picha ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere kwa mmoja wa viongozi wa matembezi hayo
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Lodrick Mpogolo (wanne kushoto-mstari wa mbele), akizindua matembezi ya UVCCM ya Miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar, kwa kutembea na vijana hao kutoka kwenye Viwanja vya Donge, Vijibeni, Wilaya ya Kaskazini Jimbo la Donge, mkoa wa Kaskazini Unguja. Picha zote na Bashir Nkoromo. 


Matembezi yakaanza
.


Mpogolo akikabidhi picha ya Rais wa Zanzibar na Mweneyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein

Mpogolo akikabidhi picha ya Amirijeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli kwa mmoja wa viongozi wa matembezi hayo 
 
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akisalimia baadhi ya viongozi wa UVCCM, baada ya kuwasili kwenye uzinduzi wa matembezi ya miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar, kwenye Viwanja vya Donge, Vijibeni, Wilaya ya Kaskazini Jimbo la Donge, mkoa wa Kaskazini Unguja. Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka na Mwenyekiti wa UVCCM Sadifa Khamis Juma.
Vijana wa Kikundi cha Sarakasi cha Mtimkavu wakionyesha uhodari wao wakati wa uzinduzi wa matembezi hayo.
Vijana wa Kikundi cha Sarakasi cha Mtimkavu wakionyesha uhodari wao wakati wa uzinduzi wa matembezi hayo.


Vijana wa Kikundi cha Sarakasi cha Mtimkavu wakionyesha uhodari wao wakati wa uzinduzi wa matembezi hayo.
Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM- Zanzibar Abdulghafar Idrisa Juma akitoa maneno ya utangulizi, wakati wa uzinduzi wa matembezi hao, leo
Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka akimkaribisha Mwenyekiti wa UVCCM, kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara kuzindua matembezi hayo, leo.
Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini, Issa Juma Ame, akizungumza baada ya kukaribishwa na Mwenyekiti wa UVCCM, wakati wa uzinduzi wa matembezi hayo, leo
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais, Mama Asha Balozi, Seif Ali Idi, akizungumza baada ya kukaribishwa na Mwenyekiti wa UVCCM kusalimia wakati wa uzinduzi wa matembezi hayo, leo.

Mama Asha Balozi Seif, akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo sh. milioni tatu, kwa ajili ya kusaidia watakaokuwa matembezini, wakati wa uzinduzi wa matembezi hayo, leo.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo, akimshukuru Mama Asha Balozi Seif, kwa kutoa msaada wa mchele na mafuta kwa ajili ya chakula cha vijana watakaoshiriki matembezi ya Miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar, wakati wa uzinduzi wa matembezi hayo leo.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akimkabidhi mifuko ya saruji, Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini, Issa Juma Ame wakati wa uzinduzi wa Matembezi hayo. saruji hiyo ambayo ni mifuko 100, imetolewa na UVCCM, kwa ajili ya ujenzi wa shule katika wilaya hiyo.

Mwenyekiti wa UVCCM, Sadifa Khamis Juma akizungumza kabla ya kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo kuzindua matembezi hayo, leo.

Vijana wa Brass Bandi ya UVCCM, wakitumbuiza kumkaribisha Naibi Katibu Mkuu wa CCM-Bara kuzindua matembezi hayo.

PICHA ZAIDI ZA MATEMBEZI HAYO/>BOFYA HAPA

No comments:

Post a Comment