Thursday, January 26, 2017

MKUU WA MKOA WA SINGIDA AFANYA ZIARA KWENYE HALMASHAURI ZA WILAYA ZA MKOA HUO.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dr Rehema Nchimbi (wa pili kutoka kushoto) akishiriki kupalilia zao la mtama Mtama katika ziara aliyoifanya Mkoani humo.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dr Rehema Nchimbi akishiriki kupanda Mihogo katika ziara aliyoifanya Mkoani humo.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dr Rehema Nchimbi (wapili kutoka kulia) akishiriki kikamilifu katika shughuli za kilimo katika ziara aliyoifanya Mkoani humo.
Mkoa wa Singida Dr Rehema Nchimbi akishiriki chakula cha mchana baada ya kukaribishwa na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Mwenge Singida katika ziara aliyoifanya Mkoani humo.

Na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Singida.

Viongozi, Watendaji na Watumishi wa Halmashauri zote za Mkoa wa Singida wametakiwa kuhakikisha taarifa zote za mapato na matumizi zinawafikia wananchi wote katika ngazi ya Kata na Kijiji ili waweze kuelewa hasa kiasi cha fedha zilizoingizwa na Serikali katika Halmashauri na namna zinavyo tumika.

Agizo hili limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi katika ziara yake ya kuzitembelea Halmashauri zote za Mkoa huo kwa lengo la kujenga Uelewa wa pamoja, utumishi wa pamoja, na kasi ya pamoja ili kufikia lengo pamoja kwa maslai  mapana ya Taifa.

Kwa upande wa Wakuu wa Idara na Vitengo Dkt Nchimbi amewaagiza wawe na taarifa za kila siku za watendaji na watumishi katika mnyororo wote wa kiutendaji na kiuongozi na kuepuka kutegemea taarifa za makaratasi na ili kuimrisha utendaji wa kuzingatia matokeo yanayo onekana.

Niaibu sana kwa Mganga Mkuu wa Wiwala (DM) kushindwa kutoa takwimu pale unapo ulizwa swali nje ya ofisi yako juu ya idadi ya watoto waliozaliwa ndani ya siku tatu katika wilaya yako au Afisa Elimu wa Halamashari unashindwa kutoa jibu la ni Walimu wangapi katika Halmashauri yako hawakuingia kazini kwa sabau za kiafya. Sinto penda hali hii iendelee kujitokeza katika Mkoa wa Singida. Aliongeza Dkt Nchimbi.


Mh Dkt Nchimbi pia amewataka Watumishi wa umma Mkoani Singida kuzinduka usingizini na kuacha kufikiri kuwa bado wapo katika kipindi cha uchaguzi na kuendekeza siasa badala ya kufanya kazi ya kuwatumikia wanchi kwa uaminifu na uadilifu kama inavyo taka serikali ya hawamu ya tano ya Tanzania chini ya Rais Dkt John Joseph  Pombe Magufuli.

Sinto mvumilia mtumishi yeyote wa umma ndani ya Mkoa wangu wa Singida atakae shindwa kwendana na kasi ya Serikali ya hawamu hii ya Tano, sitaki kuendelea kusikia msamiati wa Chini ya Kiwango katika Ujenzi na wale wote watakao husika na ujenzi wa chini ya kiwango watakamatwa na kulazimika kulipa thamani ya fedha zote zilizotumika katika ujenzi huo, watumishi wa Umma ni lazima watambue kuwa wafanyapo kazi waweke mbele maslai ya umma kwanza yaana wananchi kwanza. Alisema Mh Dkt Nchimbi.

Katika suala la usalama wa Chakula Mh Dkt Nchimbi amelitaja kuwa ni wajibu wa kila mmoja hivyo ni lazima Viongozi, Watendaji, Watumishi wa Halmashauri na Wananchi kwa Ujumla wawajibike kwa pamoja kuhakikisha kuna usalama wa chakula hasa kwa kulima Mazao yanayo tumia maji kwa ufanisi kama vile Mihogo, Mtama naViazi lishe.
  
Dkt Nchimbi amesisitiza kuwa viongozi na watendaji wote walime mashamba yasio pungua nusu heka ya kilimo cha  mihogo, viazi lishe, mtama, Watumishi wa halmashauri zote wawe na mizinga isiyo pungua miwili ya ufugaji nyuki na kila shule iwe na heka moja au zaidi ya Mihogo, viazi lishe au Mtama, pia ziwe na nusu heka au zaidi ya mazao hayo kwaajili ya walimu.

Ili kutatua changamoto ya upungufu wa makazi ya watumishi wa Umma katika Mkoa wa Singida Mh Mkuu wa Mkoa Dkt Nchimbi ameziagiza  Halmashauri zote za mkoa huo kuwapatia watumishi hasa walimu viwanja vya kujenga nyumba za makazi kwa utaratibu ambao ni rafiki na mishahara yao na licha ya kutatua changamoto ya makazi kwa watumishi pia utaratibu huo utasaida ustaafu mwema kwa watumishi wa Halmashauri hizo.

 Katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi amezindua shughuli mbali mbali za kilimo zenye kuzingatia mazao yanayo tumia maji kwa ufanisi kama vile Mihogo, Mtama naViazi lishe na pia amezindua Huduma maalum ya Afya katika Halamashuri ya Mkoa huo

No comments:

Post a Comment