Thursday, January 12, 2017

JUMBA LA WATUMWA LAWA KIVUTIO KWA WATALII VISIWANI ZANZIBAR

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
HISTORIA ya watumwa na kuanza kwa dini ya kikristo visiwani Zanzibar yawa kivutio kikubwa sana kwa watalii kutoka nchi mbalimbali kwa kufika katika Kanisa la The Cathedral Church of Christ lilijengwa na Bishop Edward Sterre kufahamu undani wakuja kwa dini hiyo kwneye visiwa hivyo.

Kanisa hilo limejengwa lilipokuwa Soko la watumwa lilijojengwa mwisho wa karne ya 19 pakitumika kama eneo la kuhifadhi watumwa wanaotolewa maeneo mbalimbali na Zanzibar ikiwa ndio kitivo cha biashara hiyo na Bishop Edward Sterre akaamua kuwanunua watumwa hao kwa lengo la kukomesha biashara ya utumwa na wakati wa ujenzi wa jengo la kanisa  watumwa walitumika kujenga na ikiwa ni kama  kuwakomboa na kisha baadae kuwabatiza na kuwa wakristo.

Kwa sasa kanisa hilo linaweza kupokea wageni kutoka mataifa mbalimbali  wanaoenda kufahamu historia ya watumwa na kuanza kwa dini ya kikristo pia kuna huweza kufika 1000 kwa siku kulingana na kipindi kilichopo.

Katika chumba kimoja cha watumwa walikaa takribani 75 yaani watoto 25 na wakubwa 50 na waliweza kukaa humo kwa kipindi kisichopungua siku mbili hadi tatu na wengine walikufa kutokana na kukosa hewa pamoja na kutokupewa chakula, mbali na hilo pia walifariki kwa magonjwa ya mlipuko kwani walikuwa wakilala juu ya kibaraza lakini kwa chini wakawa wanatumia kama sehemu ya haja ndogo na kubwa wakisubiri maji yajae baharini ili yaingie na kusafisha.

Picha za maeneo ya kanisa hilo liliopo eneo la Darajani Mkunazini Visiwani Zanzibar.
The Cathedral Church ambapo kabla ya kuwa kanisa lilitumika kama soko la watumwa visiwani humo wakiletwa kutoka sehemu tofauti kwa ajili ya biashara hiyo.
 Muonekano wa nje wa The Cathedral Church of Christ lilijengwa na Bishop Edward Sterre lililojengwa karne ya ya 19 kwa lengo la kukomesha biashara ya utumwa.

 Kanisa la Thed Cathedral Church of Christ katika muonekano wake wa ndani.
Wageni mbalimbali wakiwa wametembelea kanisa hilo na kufahamu historia ya watumwa iliyokuwa imeshamiri visiwani Zanzibar na kuanza kwa dini ya kikristo.
 Kinandsa cha kwanza kutumika katika kanisa hilo na kinapatikana katika nchi kadhaa barani Afrika ikiwamo Visiwa vya Zanzibar.
 Kinanda kingine kilichokuwa kinatumika kanisa hapo pamoja na kuharibika bado kinaendelea kutumia kwa ibada na kinafanya kazi kama kawaida.
 Kinu kilichojengwa ndani ya Kanisa hilo ambapo kilikuwa kinatumika kwa ajili ya kubatiza watumwa na baadae kuanza kutumika kwa ajili ya watoto.
 Moja ya chumba walichokuwa wanakaa watumwa wanawake na watoto 75 na walikaaq humo kwa siku mbili hadi tatu.
 Njia inayoelekea kwenye vymba vilivyokuwa vinatumika kukaa kwa watumwa ambapo  Bishop Edward Sterre aliamuru sehemu hii ndiyo ijengwe kanisa.

Picha ya Bishop  Bishop Edward Sterre ikiwa ndani ya kanisa hilo.
 Chini ni kaburi lake likiwa nyuma ya madhabahu ambapo alizikwa.


No comments:

Post a Comment