Thursday, January 12, 2017

COSATO CHUMI ATATUA TATIZO LA MASHUKA KATIKA ZAHANATI,VITUO VYA AFYA NA HOSPITALI ZA JIMBO LA MAFINGA MJINI

Na Fredy Mgunda, Iringa
Mbunge wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi ametoa jumla ya mashuka mia moja (100) kwenye zahanati,vituo vya afya na hospitali ya mafinga kwa lengo la kuboresha huduma za kiafya kwa wananchi wanaopata huduma katika maeneo hayo.
Akizungumza na blog hii mbunge huyo alisema kuwa aliomba mashuka kutoka mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF)kwa lengo la kuboresha huduma za kiafya katika jimbo la mafinga mjini.
“Zahanati na vituo vya afya vingi vinachangamoto nyingi lakini moja wapo ni kukosekana kwa mashuka ya kutosha kwenye maeneo mbalimbali ya kiafya hivyo nilichukua jukumu la kwenda mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF)kuomba  msaada wa mashuka na namshukuru mungu wamenisaidia na kunipa mashuka haya yote”. Alisema Chumi

Aidha Chumi aliwataka watendaji wa sekta ya afya katika jimbo la mafinga kuwahudumia wagonjwa kwa weledi wao ili kuifanya kada hiyo kuondokana na changamoto ambazo zimekuwa zikiwakumba mara kwa mara kutoka kwa wananchi.
“Nimeleta mashuka haya naomba mtumie na kuyatunza ili yaweze kudumu kwa muda mrefu kwa kuwa ni mashuka yenye ubora wa hali ya juu kama mnavyoyaona lakini boresheni huduma kwa kutoa huduma nzuri kwa wananchi hapo ndio wananchi watafurahia serikali yao”.Alisema Chumi
Chumi aliwashukuru mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF)kwa kuwapa mashuka hayo ambayo yamefanikiwa kutatua changamoto ya ukosefu wa mashuka katika jimbo la mafinga na amewaomba wazidi kuwasaidia wananchi wa jimbo hilo.
Kwa upande wao viongozi wa zahanati hizo walimshukuru mbunge wa jimbo hilo Cosato Chumi kwa kujituma na kutafuta njia za kutatua changamoto kwenye zahati zote za jimbo la Mafinga mjini tofauti na ilivyokuwa hapo awali kwa viongozi wengine.
“Unaona toka ameingia madarakani amekuwa akiwaleta viongozi mbalimbali wa serikali ili kutafuta njia za kutatua changamoto za huduma za afya,alimleta naibu waziri wa wizara ya afya na maendeleo ya jamii Hamis Kigwangala na wengine wengi kwenye sekta nyingine”. Walisema viongozi hao
Baadhi ya madiwani waliendelea kujivunia juhudi za mbunge wao kwa kazi kubwa anayoifanya kuwaletea maendeleo katika jimbo la Mafinga Mjini ambapo hapo awali ilikuwa vigumu kushudia  mbunge akijituma kama anavyofanya Cosato Chumi

Naye mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Mafinga Charle Makoga amesema kuwa changamoto ya huduma ya afya katika vijiji vya jimbo la Mafinga ni mbaya na inahitaji juhudi binafsi kuwasaidia wananchi na kuongeza kuwa tatizo la umeme ni kubwa katika vijiji ambavyo havipokupata umeme wa REA awamu ya kwanza na pili na ndio sababu inayosababisha huduma za kiafya kudorola katika baadhi ya vijiji.
Mbunge wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi akikabidhi mashuka kwenye moja ya Zahanati ilikuwa na upungufu wa mashuka katika kata ya Isalavanu wakati wa ziara yake ya kukagua na kugundua changamoto za zahanati za jimbo la mafinga mjini

 Mbunge wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi kushoto akiwa na katibu wake pamoja na mfanyakazi wa zahanati matanana wakati wa ziara yake
 Mbunge wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi akiwasalimia wananchi wa kata ya Isalavanu wakati wa ziara yake
Mbunge wa mafinga mjini akitandika moja ya shuka kati ya mashuka aliyoyagawa katika zahanati mbalimbali katika jimbo lake. Mashuka hayo yametolewa na mfuko wa bima ya afya NHIF

No comments:

Post a Comment