Saturday, January 14, 2017

Benki ya NMB Wachangia Ujenzi wa Skuli ya Msingi Ngambwa Kisiwa cha Uzi Wilaya ya Kati Unguja

Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said akipokea msaada wa mfano wa hundi ya shilingi milioni kumi kwa ajili ya ujenzi wa Skuli ya ngambwa uzi kutoka kwa Kaimu Meneja wa Benki ya NMB Ndg. Waziri Barnabas, hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika katika ukumbi wa Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Kati Unguja Dunga.
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said (mwenye koti) akipokea msaada wa mfano wa hundi ya shilingi milioni kumi kwa ajili ya ujenzi wa Skuli ya msingi Ngambwa uzi kutoka kwa Kaimu Meneja wa Benki ya NMB Ndg. Waziri Barnabas, mwenye tai kulia Afisa Elimu wa Wilaya ya Kati Unguja Ndg. Makame Haji na kushoto kwa Mwakilishi Sheha wa Ngambwa Ndg. Amour Ali Mussa na Mratibu wa Shughuli za Serikali SMZ  Wilaya ya Kati Unguja Ndg. Khamis Foum. hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika katika ukumbi wa Ofisi Kilimo Gunga Wilaya ya Kati Unguja.

Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Wilaya ya Kati Unguja akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhiwa hundi ya shilingi milioni kumi kutoka kwa Kaimu Meneja wa Benk ya NMB Tanzania kwa ajili ya ujenzi wa Skuli ya Msingi Ngambwa kisiwa cha Uzi Wilaya ya Kati Unguja na kutowa shukrani kwa msaada wao huo kutowa kwa ajili ya jamii kuwapatia watoto wao majengo ya skuli katika eneo lao. Benk ya NMB itejenga jengo la Skuli hiyo katika Kijiji cha Ngambwe Uzi.

Kaimu Meneja wa Benk ya NMB Waziri Barnabas akizungumza na Uongozi wa Wilaya ya kati Unguja kuhusuana na kuguswa kwa hali ya kijiji hicho cha ngambwa watoto kupata elimu yao ya msingi masafa marefu na makazi yao. kushoto Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Wilaya ya Kati Ungja. 
 Afisa Elimu Wilaya ya Kati Unguja Ndg. Makame Haji, akitowa shukrani kwa uongozi wa Benk ya NMB kwa msaada wao huo kuwakumbuka Wakazi wa Ngambwa kuwapatia msaada kwa ajili ya kumalizia jengo la Skuli yao ya Msingi. ilioazwa msingi na wananchi wa kijiji hicho. 
Mratibu Shughuli za Serikali ya SMZ Wilaya ya Kati Unguja Ndg Khamis Foum akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi msaada huo kwa ajili ya maendeleo ya ujenzi wa jengo la Skuli ya Msingi Ngambwa Uzi. na kutowa shukrani kwa Mwakilishi na Mbunge wa Jimbo la Tunguu kwa msaada wao kufanikisha shughuli hiyo ya ujenzi wa Skuli hiyo kuwapunguzia masafa marefu watoto wa ngambwa kufuati masomo katika eneo la uzi.
Maafisa wa Benk ya NMB wakiwa katika ukumbi wa mkutano wakishuhudia hafla hiyo ya makabidhiano.
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said akimkabidhi zawadi ya embe za boribo za muyuni Kaimu Meneja Mkuu wa NMB Waziri Barnabas, baada ya hafla hiyo ya kukabidhi cheki ya shilingi milioni kumi kwa ajili ya ujenzi wa Skuli ya Msingi Ngambwa.  

Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Wilaya ya Kati Unguja Mhe, Simai Mohammes Said akimkabidhi zawadi ya mananasi ya Zenj Kaimu Meneja wa Benki ya NMB Ndg Waziri Barnabas, baada ya hafla ya kukabidhi cheki shilingi milioni kumi kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa Skuli ya Msingi Ngambwa Uzi Wilaya ya Kati Unguja.
Imetayarishwa na OthmanMapara. Blog.
Zanzinews.com
Mob. 0777424152. Or 0715424152.  

No comments:

Post a Comment