Sunday, December 25, 2016

Profesa Muhongo asheherekea Krismasi kwa kufanya makubwa Musoma Vijijini

Mbunge wa Musoma Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ametoa mifuko 300 ya saruji kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa Zahanati ya Kigeraetuma iliyopo Kijiji cha Kamuguruki, Musoma Vijijini ikiwa ni zawadi ya sikukuu ya Krismasi.

Zawadi hiyo imetolewa leo kijijini humo katika hafla ya chakula aliyoiandaa kwa ajili ya wananchi wa Kijiji hicho pamoja na vijiji vingine mara baada ya ibada iliyofanyika katika kanisa la Menonite lililopo kijiji cha Nyakatende, Musoma Vijijini..

Katika hafla hiyo Profesa Muhongo aliongozana na familia yake pamoja na rafiki zake kutoka Ujerumani ambao kwa pamoja walijumuika na wananchi wa Musoma vijijini kusherehekea.
 Kanisa la Menonite la kijiji cha Nyakatende ambapo Mbunge wa Musoma Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, familia yake na rafiki zake kutoka Ujerumani walishiriki ibada ambapo aliahidi kuchangia ujenzi wake. 
 Mbunge wa Musoma Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa tatu kutoka kushoto waliokaa katika viti) katika picha ya pamoja na waumini wa Kanisa la Menonite mara baada ya kumalizika ibada.
Diwani wa Kata ya Nyakatende, Rufumbo Rufumbo (katikati) akionesha vifaa vya umeme jua alivyokabidhiwa na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) . 
 Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (aliyeshika kipaza sauti) akiwa amepanga foleni na wananchi wa jimboni mwake kwa ajili ya kuchukua chakula.
 Wananchi wa Kata ya Nyakatende wakichukua chakula

Mbunge wa Musoma Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa pili kulia) akionesha vifaa vya umeme jua ambavyo Balozi wa Korea nchini anatarajiwa kupeleka mtaalamu jimboni humo ili kuwafundisha vijana namna ya utengenezwaji wake ili kujipatia kipato

No comments:

Post a Comment