Saturday, October 29, 2016

PROGRAMU YA JIANDALIE AJIRA YAZINDULIWA RASMI

Naibu Waziri wa Elimu , Sayansi na Teknolojia Mhandisi Stella Manyanya (kulia) akikata utepe wakati uzinduzi wa program ya JIANDALIE AJIRA inayolenga kupunguza tatizo la ajira nchini. Wengine katika picha ni Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Kimataifa wa Vijana (IYF), Bw. William Reese (wa pili kulia), Mwenyekiti wa bodi wa Taasisi ya Ujasiriamali na Ushindani TECC Bi. Beng’I Issa (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Ujasiriamali na Ushindani, Bw. Sosthenes Sambua (wa pili kushoto) na Ahmed Makbel Mkurugenzi Msaidizi wa Ajira kutoka ofisi ya Waziri Mkuu (katikati).
Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa wa Mfuko wa Kimataifa wa Vijana (IYF), Bw. William Reese, akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa program ya Jiandalie Ajira jana jijini Dar es Salaam, wengine katika picha ni Mwenyekiti wa bodi wa Taasisi ya Ujasiriamali na Ushindani (TECC) Bi. Beng’I Issa (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa (TECC) Sosthenes Sambua katikati, program hiyo ili zinduliwa na Naibu Waziri wa Elimu , Sayansi na Teknolojia Mhandisi Stella Manyanya kwenye ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam jana.

Na Ally Daud-MAELEZO. 

Mfuko wa Kimataifa wa Vijana( Interanational Youth Foundation) imezindua rasmi programu mpya ya miaka mitano wa JIANDALIE AJIRA unaowalenga vijana hapa nchini kama moja ya jitihaha za kukuwajengea vijana mafunzo ya ufundi stadi na ujasiriamali kuondokana na tatizo la ajira . 

Akizindua programu hiyo, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Technolojia ,Mhandisi Stella Manyanya alisema program hiyo ni ukombozi mkubwa kwa vijana hapa nchini kwa kuwa itawawezeshae kutengEneza ajira na kukuza uchumi. 

“Programu hii imekuja kutengneza vijana kuwa wabunifu na kutengneza ajira ikiwa ni pamoja na kuajiri wengine na siyo kuwa wasaka ajira,”na kwa kufanya hivyo taifa litapiga hatua kiuchumi,aliongeza kusema,Mhandisi huyo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nyasa” alisema Mhandisi Manyanya 

Aidha Mhandisi Manyanya aliupongeza mfuko huo wa IYF kwa kuja na mradi ambao utatekelezwa kwa ushirikiano na Taasisi ya Ujasirimali na Ushindani (TECC), Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) na Shirika lisilokuwa la kiserikali la The MasterCard Foundation. 

Mhandisi Manyanya alisema pia programu hiyo itawezesha kuwaandaa wakufunzi wa chuo cha VETA ili waweze tumika katika kuwafundisha vijana ambao ndio walengwa katika mradi mzima na ambao wanachangamoto kubwa ya ajira. 

Mbali na hayo Mhandisi Manyanya alikitaka chuo hicho kuendeleza na kupanua wigo wa ushirikiano na waajiri ili kujenga nguvu kazi kukidhi matwakwa ya soko la ajira kwenda sambana na dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025. 

Kwa upande wa Rais wa IYF ambaye pia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa mfuko huo Bw.William Reese alisema mfuko wao umeandaa mpango huo kwa nchi za Tanzania na Msumbiji kwa ajili ya kuwaandaa vijana katika elimu ya mafunzo ya ufundi stadi na uujasirimali 

“Tatizo la ajira siyo la Tanzania tu bali la dunia nzima kwa nchi zilizoendelea na ambazo hazijaendelea”, na hitaji mipango ya pamoja, ya kidunia na yakinchi kwa kushitrikiana na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali” alisema Bw. Reese. 

Pia Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika IYF (Regional Director,Africa) , Bw.Mathew Breman alisema mpango wa jiandallie ajira utaendeshwa kwa muda wa miaka mitano na unalenga kuwapatia mafunzo ya ufundi stadi na jasirimali kwa vijana. 

” Programu hii inahusu vijana wa miaka 18 hadi 24 na watapata mafunzo na mikoa inayolengwa ni pamoja na Dar es Salaam, Dodoma, Mtwara,na Morogoro,” na vijana 22,500 watanufaika na mradi huu, aliongeza Bw. Breman. 

Aidha Bw. Breman mradi unaletekezwa katika nchi Msumbiji ambapo kwa pamoja na Tanzania utanufaisha vijana 30,000 kupata mafunzo ya ufundi stadi na ujasiriamali katika kipindi hicho. 

Mwenyekiti wa Bodi wa Taasisi ya Ujasirimali na Ushindani (TECC),Bi. Issa Beng’I alisema program hiyo ni muhimu kwa vijana. 

“Tunazo program nyingi hapa nchini Tanzania, ikiwemo kijana jiajiri, vijana wa bodaboda,vijana wa JKT, na sasa program ya jiandalie ajira itawawezesha kujitambua zaidi,” na kufanikiwa kwa hili ni ukombozi mkubwa kwa taiafa letu, aliongeza kusema Bi. Issa. 

Moja ya vijana , Nuru Mungi akitoa ushuhuda wa biashara yake, alisema mafanikio aliyoyapata katika ujasirimali yamekuja baada ya kupata mafunzo (TECC). 

“ Kutokana na mafunzo haya sasa namiliki kiwanda kidogo cha kutengneza sabuni na naamini kupitia program ya jiandalie ajira vijana wengi watanufaika na kupanua wigo wa ujasirimali.alisema. 

Mkurugenzi Msaidizi wa Ajira toka Ofisi ya Waziri Mkuu, Ahamed Makbel,alisema tatizo la ajira hapa nchini kwa kwa sasa limefikia asilimia 10.3. 

“Tatizo hili kwa vijana limefikia asilimia 11.7 kwa vijana amabyo ni nguvu kazi kubwa inayobeba asilimia 56 kwa nchi nzima, vijana hao wanaumri kati ya miaka 15 hadi 35. 

Mfuko wa IYF umesha fanya kazi katika mataifa zaidi ya 70 duniani ili kuweza kusaidia vijana mbalimbali kwa ajili ya kukuza uchumi wa kijana na taifa kwa ujumla ili kufikia uchumi wa kati. 

No comments:

Post a Comment