Thursday, October 27, 2016

Balozi wa Tanzania nchini Malawi awataka Polisi Ileje kudhibiti Magendo mipakani

  Balozi wa Tanzania nchini Malawi,Victoria Mwakasege, akizungumza na baadhi ya  viongozi wa Wilaya ya  ileje wakati wa ziara yake ya kukagua mpaka kati ya Tanzania na Malawi.
Balozi wa Tanzania nchini Malawi,Victoria Mwakasege akisaini kitabu cha wageni kilichoshikwa na katibu Tawala wa Wilaya ya Ileje, Mary Joseph.   
 Mkuu wa Wilaya ya Chitipa,Grace Chirwa akizungumza na baadhi ya watendaji wa Tanzania na Malawi wakati wa ziara ya kukagua mipaka.
 Balozi wa Tanzania nchini Malawi,Victoria Mwakasege, akiwa na watendaji wa wa nchi zote mbili katika mpaka wa Tanzania na Malawi.
Picha ya pamoja ya watendaji wa Tanzania na Malawi.

BALOZI wa Tanzania nchini Malawi, Victoria Mwakasege, amewataka Polisi kuimarisha ulinzi katika mipaka kati ya Tanzania na Malawi katika Wilaya ya Ileje.

Balozi Mwakasege amesema hayo wakati wa ziara yake ya ujirani mwema kati ya Wilaya ya Ileje ya Tanzania na Chitipa ya Malawi katika mpaka wa Isongole.

“lazima tukomeshe na kufunga njia zote za panya hasa zile ambazo zinapitisha bidhaa haramu kwa aupande wetu wa tanzania” amesema Mwakasege.

Ameongeza kuwa kuna bidhaa zingine nchini Malawi ni halali lakini kwetu ni haramu, jambo ambalo linaleta shida kwa vijana wetu hasa pombe nyingi zinazotoka nchi hiyo, kwetu zimepigwa marufuku.

Amesema kuwa pombe za viroba na Sukari vimekuwa zikitumia kuvushwa kwa njia za panya hali inayo hatarisha afya ya mlaji na kuikosesha serikali mapato.

No comments:

Post a Comment