Monday, September 5, 2016

ZANTEL WAZINDUA OFA YA JIBWAGE NA MBUZI KUSHEREHEKEA SIKUKUU YA IDD.

 Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kuzindua ofa maalumu kwa wateja wanaotumia mtandao wa simu za Mkononi wa Zantel ofa ya shinda mbuzi, pamoja na kutoa mbuzi kwa Vituo 50 vya kulelea watoto yatima jijini Dar es Salaam.
 Meneja huduma na bidhaa wa Zantel, Ernest sengeu akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mara baada ya Mkurugenzi Mkuu wa Zantel Tanzania kuzindua Ofa maalumu kwa wateja wa nzantel ambapo wateja watajiunga kwa kubonyeza *149*15# ili kushiriki ofa hiyo ambayo mwisho nwake ni sikukuu ya Idd ya Kuchinja amayo itakuwa Septemba 13. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin.
 Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin akimkabidhi Mbuzi mwakilishi wa Kituo cha Kulelea watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu cha Kurasini National Childrens Home, Silas Kusewa Kurasini jijini Dar es Salaam leo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin akimkabidhi Mbuzi mwakilishi wa Kituo cha Kulelea watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu cha Tanzania Mitindo House Klichopo Kiamboni, Khadija Mwanamboka mara baada ya Mkurugenzi huyo kuzindua Ofa maalumu kwa wateja wake ya shinda mbuzi.
Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin akimkabidhi Mbuzi mwakilishi wa Kituo cha Kulelea watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu cha Help2kids.Org, Leah Mchomvu Kituo kilichopo Mbezi Beach jijini Dar es Salaam leo.

KAMPUNI ya Simu za Mkononi Zantel imezindua Kampeni ya Jibwage na Mbuzi katika kusherehekea Sikukuu ya Idd el Adha, ikitambulika pia kama 'Sherehe ya Kuchinja' kwa kutoa mbuzi 500 kwa wateja wake wenye matumizi ya  zaidi huku mbuzi 100 wakigawiwa katika vituo mbalimbali vya watoto yatima nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin amesema "Hii ni sehemu ya kuwashukuru wateja wetu na kusherehekea pamoja nao Sikukuu ya Idd. Imekuwa ni utamaduni wetu kurudisha katika jamii kupitia kampeni na miradi mbalimbali, hivyo kwa leo Zantel inatoa mbuzi 500 katika kusherehekea Sikukuu hii ya Kuchinja.”

Idd el –Adha ni moja ya sikukuu mbili muhimu za Kiislamu ambayo waumini wa dini ya kiislamu huiadhimisha kwa kuonyesha umuhimu wa kutoa sadaka kwa kuchinja na ibada.

Mbuzi 400 watatolewa kwa wateja wa Zantel wenye matumizi zaidi kuliko wengine na ambao watakuwa wamejisajili katika kampeni kwa kupitia *149*15# na kuchagua  “Jibwage na Mbuzi”. Kujisajili katika promosheni hii ni bure kwa wateja wote wa Zantel. Kila siku wateja 40 watakaokuwa wametumia muda zaidi watajizawadia mbuzi.

 “Hii si bahati nasibu, wale wateja wa juu watakaokuwa wametumia dakika nyingi bila kuchezeshwa mchezo wa bahati watakuwa wamejizawadia moja kwa moja hivyo natumia fursa hii kuwahamasisha wateja wetu kujisajili ili kupata mbuzi na kusambaza furaha ya Eid katika familia zao” alisema  Benoit

Mbuzi 100 wanaobaki watatolewa msaada kwa  vituo vya watoto yatima vilivyochaguliwa katika mikoa mbalimbali. 

“ Pia tunatumia nafasi hiyo hiyo kusaidia watoto yatima na wale wasioweza kufanikisha sadaka hii ya kuchinja ili nao wafurahi pamoja na wengine na kushiriki upendo unaotokana na Idd”,  ameongeza.

Miongoni mwa miradi ambayo Zantel imetoa misaada ni mradi wa kina mama wanaozalisha zao la mwani Unguja, huduma za maktaba Zanzibar –Zanzibar Library Services, vile vile kompyuta na internet ya bure kwa kikundi cha wasanii cha Mkubwa na Wanawe na vituo mbali mbali vya walimu Zanzibar.

No comments:

Post a Comment