Tuesday, September 27, 2016

MASAUNI AWAONGOZA WAJUMBE WA BARAZA LA TAIFA LA USALAMA BARABARANI KUTOA MISAADA KITUO CHA WATOTO YATIMA MJINI GEITA

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akimkabidhi fedha taslimu Shilingi 1,119,000, Msimamizi wa Kituo cha Watoto Yatima cha Moyo wa Huruma kilichopo mjini Geita, Sista Adalbera Mukure kwa ajili ya kusaidia majukumu mbalimbali ya ulezi wa watoto hao. Fedha hizo zilitolewa na Masauni pamoja na Wajumbe wa Baraza hilo kwa lengo la kusaidia kituo hicho. Pia Baraza hilo lilitoa mchele gunia moja, kilo 50 za sukari, dumu la mafupta ya kupikia, sabuni Katoni 11 pamoja na fulana 100.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akimkabidhi misaada mbalimbali, Msimamizi wa Kituo cha Watoto Yatima cha Moyo wa Huruma kilichopo mjini Geita, Sista Adalbera Mukure kwa ajili ya kusaidia watoto hao. Pia Masauni alimkabidhi msimamizi huyo wa kituo mchele gunia moja, dumu la mafupta ya kupikia, sabuni Katoni 11, fulana 100 pamoja na fedha taslimu Shilingi 1,119,000 ambazo zilitolewa na wajumbe wa Baraza hilo. Kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, ambaye pia ni Katibu wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (aliyembeba mtoto) na Katibu wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga (kulia) wakiwa na baadhi ya watoto Yatima wa Kituo cha Moyo wa Huruma cha mjini Geita, mara baada ya Masauni kukabidhi fedha taslimu shilingi 1,119,000 pamoja na vyakula kwa kituo hicho ambapo misaada hiyo ilitolewa na Baraza la Usalama barabarani ambalo linaadhimisha Wiki ya Nenda kwa Usalama mjini humo.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akizungumza na Watoto Yatima wa Kituo cha Moyo wa Huruma kabla ya kuwakabidhi misaada mbalimbali ambayo aliwaongoza Wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani kukusanya misaaida mbalimbali. Misaada hiyo iliyotolewa ni fedha taslimu shilingi 1,119,000 pamoja na mchele gunia moja, kilo 50 za sukari, dumu la mafupta ya kupikia, sabuni Katoni 11 pamoja na fulana 100.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (aliyembeba mtoto), Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali Mstaafu, Ezekiel Kyunga (kulia kwa Masauni),  pamoja na Wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani wakiwa katika picha ya pamoja na Watoto Yatima wa Kituo cha Moyo wa Huruma cha mjini Geita, wakati Mwenyekiti huyo wa Baraza pamoja na wajumbe wake kukitembelea kituo hicho na kukabidhi misaada mbalimbali. Tukio hilo lilifanyika mara baada ya Masauni kuizindua Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo inaadhimishwa Kitaifa mjini Geita. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.

No comments:

Post a Comment