Monday, August 1, 2016

WADAU WA SEKTA YA AFYA KANDA YA KASKAZINI WADAU WAKUBALIANA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA.

  Meneja Masoko wa AAR Insurance Tanzania, Tabia Masoud akitambulisha wafanyakazi wenzake kwa wadau wa sekta ya afya wa mkoa kanda ya Kaskazini wakati wa mkutano wa kampuni hiyo na wadau hao kujadiliana namna ya kuboresha huduma za afya jana jijini Arusha.
  Meneja Maendeleo ya Biashara wa AAR Insurance Tanzania, Hamida Nassor akijadiliana jambo na wadau mbalimbali waliohudhuria mkutano kati ya kampuni hiyo na wadau wa sekta ya afya kanda ya kaskazini kujadiliana namna ya kuboresha huduma za afya jana jijini Arusha
Wadau wa sekta yaw a kanda ya kaskazini wakijadiliana wakati wa mkutano kati yao na kampuni ya bima ya afya ya AAR Insurance Tanzania juu ya namna ya kuboresha huduma za afya jana jijini Arusha.
 Wadau wakijiandikisha.
  Meneja Masoko wa AAR Insurance Tanzania, Tabia Masoud akiongea machache.
 Wadau wakiwa katika picha ya pamoja. 

Ikiwa ni sehemu ya jitihada zake kuimarisha utoaji huduma za afya nchini, kampuni ya bima ya AAR Insurance Tanzania pamoja na wadau wake waliopo Kanda ya Kaskazini wamekubaliana kuhakikisha huduma zitolewazo kwa wateja wake zinakuwa za ubora wa hali ya juu na za kuridhisha. Maazimio hayo yamefikiwa baada ya wadau hao kukutana jijini Arusha mwishoni mwa wiki ambapo walijadiliana mikakati na changamoto za kiutendaji zinazokabili utoaji huduma za afya.

Akiongea katika mkusanyiko huo uliojumuisha wadau kutoka hospitali mbalimbali, vituo vya afya, zahanati, kliniki na maduka ya dawa kutoka mikoa ya kanda ya kaskazini, Mkuu wa Operesheni wa AAR Insurance Tanzania, Wilfred Rono alisema ubora wa huduma ya afya unaweza kuboreshwa na uongozi bora, kuwa na mipango mizuri, elimu na mafunzo, upatikanaji wa rasilimali, menejimenti thabiti ya rasilimali, wafanyakazi, na ushirikiano miongoni mwa wadau na akaongeza kuwa ni muhimu kwa wadau hao kukutana na kuweka mikakati.

Wilfred Rono pia aliongeza kwamba dhumuni la tukio hilo lilikuwa ni kuimarisha uhusiano kati ya kampuni hiyo kubwa zaidi ya bima ya afya na wadau wake huku na kuongeza kuwa mkutano huo umetumika kuelimisha wadau juu ya bidhaa na huduma za bima ya afya.

AAR Insurance Tanzania ni sehemu ya AAR Insurance Holdings ambayo ndio kampuni kubwa zaidi ya bima za afya kwenye ukanda wa Afrika Mashariki.

No comments:

Post a Comment