Tuesday, August 30, 2016

Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki yafunguliwa rasmi Jijini Mwanza

Mkuu wa Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, Dkt.Leonard Massale, hii leo akifungua Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayofanyika Jijini Mwanza. 

Maonesho hayo yameandaliwa na Chemba ya Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo nchini TCCIA, yalianza Agosti 26,2016 na yanatarajiwa kufikia tamati Septemba 04,2016 katika viwanja wa Rock City Mall.
Na BMG
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, Dkt.Leonard Massale, akizungumza kwenye Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayofanyika Jijini Mwanza. 
Mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Mwanza, Elibariki Mmari, akizungumza kwenye Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayofanyika Jijini Mwanza. 
Mwenyekiti wa TCCIA mkoani Mara, akizungumza kwenye Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayofanyika Jijini Mwanza. 
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye wa Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayofanyika Jijini Mwanza. 
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye wa Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayofanyika Jijini Mwanza. 
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye wa Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayofanyika Jijini Mwanza. 
Picha ya pamoja.

Wafanyabiashara katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wamehimizwa kuchangamkia fursa za kibiashara na uwekezaji zilizopo katika soko la pamoja la nchi hizo kutokana na soko hilo kuwa na idadi kubwa ya wateja.
Akifungua maonesho ya 11 ya biashara ya Afrika Mashariki yanayofanyika kwenye viwanja vya Rock City Mall jijini Mwanza,Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela amesema soko lililopo kwenye nchi hizo lina zaidi ya wateja milioni 140 na hivyo likitumika vizuri litatoa fursa ya kuuziana bidhaa wenyewe kwa wenyewe.
Kwenye hotuba ya ufunguzi iliyosomwa na Mkuu wa wilaya ya Ilemela Dkt.Leonard Massale,mkuu huyo wa mkoa amesema badala  ya wafanyabiashara hao kutegemea masoko ya nje yanayofikika kwa gharama kubwa,wanapaswa kuuziana bidhaa ndani ya nchi za Afrika Mashariki na hivyo kuinua uchumi wa nchi hizo.
Aidha amewahimiza waandaaji wa maonesho hayo chemba ya wafanyabiashara, wenye viwanda na kilimo nchini, TCCIA, kuyatangaza zaidi ili yavutie makampuni mengi kutoka nchi zingine.
Katika hotuba yake Mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Mwanza, Elibariki Mmari, amesema licha ya kuandaa maonesho hayo kwa miaka 11 mfululizo bado wanakabiliwa na changamoto ya kutokuwa na eneo linalofaa kwa ajili ya maonesho hayo na hivyo kulazimika kuhama mara kwa mara na kuiomba serikali kuharakisha upimaji wa eneo la maonesho Nyamuhongolo ili kujenga majengo ya kudumu.
Maonesho ya mwaka huu yanashirikisha zaidi ya washiriki 300 kutoka nchi mbalimbali zikiwemo Kenya, Uganda, China na wenyeji Tanzania ambapo kuna mabanda ya bidhaa mbalimbali pamoja na wanyama hai.
Bonyeza HAPA Kujua Zaidi

No comments:

Post a Comment