Tuesday, July 26, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIMU.TV: Mkuu wa mkoa wa Dar Es salaam Paul Makonda, ameishauri TAMISEMI kuwachukulia hatua wahusika wote walioshiriki katika mkataba usio wa haki wa ujenzi Machinga Complex; https://youtu.be/tEH85noqFXA

SIMU.TV: Rais Dr Magufuli ameiomba benki ya maendeleo ya Afrika ADB, kuendelea kushirikiana na Tanzania katika ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya maendeleo;https://youtu.be/DDuBFzUtic4

SIMU.TV: Waziri mkuu Kassim Majaliwa, ametoa siku 14 kwa serikali ya mkoa wa Dodoma kutoa mpango kazi wa utekelezaji wa uamuzi wa serikali kuhamia mkoani humo;https://youtu.be/C_aJWRdRnXI

SIMU.TV: Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo, imefanikiwa kukamilisha zoezi la utengenezaji wa madawati bila kutumia fedha za serikali wala hamlashauri;https://youtu.be/KBButcakG2U

SIMU.TV: Huduma ya usafiri wa umma mkoani Mwanza, ililazimika kusimama kidogo kutokana na mgomo wa madereva uliosababishwa na malumbano baina yao na askari polisi wa barabara; https://youtu.be/cTuw8oizgpY

SIMU.TV: Katibu mkuu wa TAMISEMI Mhandisi Mussa Iyombe, amesema serikali inajipanga kutumia mfumo wa Dijitali katika usajili wa sensa ya watu na makazi kwa awamu ijayo; https://youtu.be/IANDQIU8Pxk

SIMU.TV: Mapato ya fedha kwa njia ya simu za mikononi, yameongezeka kwa asilimia 7 zaidi kulinganisha na mapato ya mwaka uliopita; https://youtu.be/Hk5NghXiXX4

SIMU.TV: Benki ya Posta Tanzania imetoa mikopo ya shilingi za kitanzania Bilioni 278 kwa makundi mbalimbali ya wajasiliamali nchini; https://youtu.be/FTTYUA5SQa0

SIMU.TV: Maonyesho ya bidhaa za baharini yanatarajia kufanyika nchini China mwezi ujao huku watanzania wakishauriwa kutumia fursa kwa ajili ya kukuza masoko ya bidhaa zao;https://youtu.be/EvLxfhxBgOU

SIMU.TV: Ndoto za klabu ya soka ya Yanga kutinga katika hatua ya Nusu Fainali kombe la shirikisho barani Afrika, zinazidi kuzama baada ya kuruhusu kufungwa mabao 3-1 na Medeama ya Ghana; https://youtu.be/F8nynm9OG4U

SIMU.TV: Kocha mkuu wa timu ya Taifa, Taifa stars Charles Boniface Mkwasa, leo ametangaza kikosi kitakachoingia kambini kujiwinda na mchezo wao dhidi ya Nigeria;https://youtu.be/x8uZ_UHtCEE

SIMU.TV: Shirikisho la mpira wa miguu Duniani FIFA, hatimaye limeongeza idadi ya timu zitakazoshiriki michuano ya kombe la dunia kutoka 32 za awali mpaka 40;https://youtu.be/WBp-1AcCTk4

SIMU.TV: Jeshi la polisi mkoani Mwanza limelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya madereva wa daladala na makondakta waliokuwa wameziba barabara.https://youtu.be/SOl3SJIHLUQ

SIMU.TV: Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU imewapandisha kizimbani watu wawili kwa kosa la kugushi nyaraka za TRA na kuisababishia serikali hasara.https://youtu.be/lcf04oZski4

SIMU.TV: Idara ya uhamiaji mkoani Mtwara imewakamata wahamiaji haramu 18 waliokuwa wakijaribu kuvuka mpaka wa Tanzania na Msumbiji.https://youtu.be/6djE_b7eh3A

SIMU.TV: Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Dar es Salaam imebaini ubadhirifu mkubwa wa fedha katika ujenzi wa jengo la Machinga complex.https://youtu.be/pxCrFVImjVU

SIMU.TV: Mkuu wa mkoa wa mjini Magharibi ametoa wito kwa wadau mbalimbali kujitokeza kuchangia madawati katika visiwa vya Zanzibar ili kumaliza tatizo la upungufu wa madawati. https://youtu.be/62tQyYdqNs0

SIMU.TV: Wanafunzi wa shule ya msingi Mongo la Ndege iliopo Ukonga jijini Dar es Salaam wameushukuru mfuko wa bunge kwa kuwasaidia madawati.https://youtu.be/Cq8Z1WAKcAI

SIMU.TV: Shule ya msingi Msanzi B inaelezwa kukabiliwa na uhaba wa madarasa ya kusomea jambo ambalo linsababisha wanafunzi kuingia darasani kwa zamu.https://youtu.be/LFfN4pVoqbQ

SIMU.TV: Rais Dr John Pombe Magufuli akutana na kufanya mazungumzo na makamu wa rais wa benki ya maendeleo ya Afrika AfDB na kuishukuru benki hiyo kwa kushirikiana na Tanzania katika kutekeleza miradi ya maendeleo. https://youtu.be/cMQ6n2QnWkQ

SIMU.TV: Kampuni za simu hapa nchini zinakabiliwa na changamoto ya miundo mbinu ili kuwafikia wakazi wengi waishio maeneo ya vijijini. https://youtu.be/Oiu0LG-J_d8

SIMU.TV: Mkuu wa wilaya ya Kyela mkoani Mbeya ameunda bodi ya zao la kakao ili kuwasaidia wakulima katika masuala mbalimbali ya uzalishaji wa zao hilo.https://youtu.be/ww8yXR9bzLY

SIMU.TV: Kocha mkuu wa timu ya taifa Charles Boniface  ametangaza kikosi kitakacho vaana na timu ya taifa ya Nigeria. https://youtu.be/HTZMAqU7XmU

SIMU.TV: Shirika la hifadhi za taifa nchini TANAPA limeamua kutumia michezo ya Olimpic kutangaza vivutio vilivyopo nchini Tanzania. https://youtu.be/cZ36DelVfOo

SIMU.TV: Warembo wanaowania taji la miss Dar Indian Ocean wametemelea kampuni ya Africa media group ili kujionea inavyofanya kazi. https://youtu.be/6co56bCaalk

SIMU.TV: Aliyekua mchezaji wa Liverpool Joh Allen ameihama timu hiyo na kujiunga na klabu ya Stoke City. https://youtu.be/HMJ6PV9nuaw

No comments:

Post a Comment