Thursday, July 28, 2016

Serikali yapongeza mpango wa Airtel FURSA, kikundi cha wanawake chapokea msaada wa shs milioni 10.

 Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kushoto) akikabidhi msaada wa mashine ya kutengeneza sabuni na vifungashio vyenye thamani ya zaidi ya milioni 10/- kupitia mpango wa Airtel FURSA ‘Tunakuwezesha’ kwa Mwenyekiti wa Kikundi cha Tupendane cha Tandika, Nasra Haji  katika hafla iliyofanyika kituoni hapo Manispaa ya  Temeke jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Afisa Maendeleo ya Vijana wa Manispaa hiyo, Anna Marika. 
Afisa Maendeleo ya Vijana wa Manispaa ya Temeke, Anna Marika (kushoto) akikabidhi kwa niaba ya Airtel msaada wa na vifungashio vya sabuni  baada ya kampuni hiyo kukabidhi  mashine ya kutengeneza sabuni vyenye thamani ya zaidi ya milioni 10/- kupitia mpango wa Airtel FURSA ‘Tunakuwezesha’ kwa Mwenyekiti wa Kikundi cha Tupendane cha Tandika, Nasra Haji  katika hafla iliyofanyika kituoni hapo jijini Dar es Salaam jana.  Wa (pili kushoto) ni Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi.

Kufatia mchango wake katika maendeleo ya miradi ya vijana Serikali imeupongeza mpango wa Airtel FURSA kwa kuwawezesha vijana nchi nzima kukuza uchumi wao.

Hayo yamesemwa na Afisa maendeleo ya vijana wa wilaya ya Temeke , Bi Anna Marica wakati Airtel kupitia mpango wake wa Airtel FURSA ilipotoa msaada wenye thamani ya shilingi milioni 10  kwa kikundi kilichoundwa na wanawake 12 cha Tupendane kilichopo Temeke jijini Dar es salaam

Alisema”  kupitia mradi wa Aritel FURSA, Airtel Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kuwasaidia vijana nchini na kupongeza kikundi cha Tupendane kwa kuwa moja kati ya vikundi vilivyofikiwa na Airtel FURSA

“Kikundi cha Tupendane kimeonyesha mfano mzuri hususani kwa vijana wakike na napenda kuwahasa muongeze hari na kufanyakazi kwa bidii zaidi ili kuongeza uzalishaji na kutengeneza ajira kwa vijana waishio jijini Dar es salaam.” Alisema Marica

Msaada wa vifaa uliotolewa kwa kikundi hicho ni pamoja na mashine mpya ya kutengenezea sabuni, vifungashio pamoja na kuboreshewa mazingira ya ofisi ya kufanyia kazi.

Kwa upande wake Meneja huduma kwa jamii, Bi Hawa Bayumi alisema“  tunatambua juhudi na ubunifu mkubwa unaofanywa na kikundi hiki na tunaamini msaada huu utasaidia kuinua mapato yao  kwa ujumla.

 “Huu ni msimu wa pili wa mradi wetu wa Airtel FURSA ambapo mpaka sasa tumeweza kuwafikia vijana wajasiriamali 20, makundi ya wajasiriamali 30 pamoja na kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa zaidi ya vijana 3000 nchini. leo tunajisikia furaha kukiwezesha kikundi hiki cha Tupendane kwani tunatambua kwa kuwawezesha vijana hawa 12 tutaweza kuziwezesha familia zao na jamii kiuchumi kwa namna moja au nyingine“ alisema Bayumi

 Mwenyekiti wa kikundi cha Tupendane Nasa Hija Siri aliwashukuru Airtel kwa kuwafikia vijana wengi na kutatua changamoto zao na kuahidi kutumia msaada huo kuongeza uzalishaji

 “ kupitia msaada huu tunauhakika wa kuongeza kiwango cha uzalishaji wa bidhaa zetu kwani kwa sasa tunatengeneza lita 20 kwa siku, na kwa msaada huu sasa tutazalisha hadi lita 100 kwa siku  haya kwetu sisi ni mafanikio makubwa na tunawashukuru sana Airtel”alisema Nasa

 Kikundi cha tupendane kilianza biashara zake kwa kuuza vitenge na kukopesa kwa wateja, biashara hii haikuwa ya mafanikio kwani wateja walishindwa kulipa madeni yao kwa wakati ndipo walipoamua kuanzisha biashara ya kutengeneza na kusambaza sabuni za maji na shampoo za nywele

No comments:

Post a Comment