Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Ngabaganga Taraba akifungua
mafunzo ya mgambo katika kata za Mwaweja na Ukenyenge wilayani humo, ambapo
aliwataka vijana kuwa wazalendo. Akiwapongeza kwa kujitoa kwao kuhudhuria mafunzo
hayo, alisema suala la ulinzi wa mali na raia ni la kila mwananchi.
Aliwataka kutumia mafunzo hayo kwa mtazamo chanya na kuwa mabalozi wazuri wa
amani na uzalendo kwa nchi yao. Aidha, Taraba aliwapongeza wakufunzi wa mafunzo
hayo kwa kazi nzuri ya kuwafundisha vijana stadi za ukakamavu ili wawe walinzi wazuri
wa amani.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kengese akimkaribisha Mkuu wa
Wilaya kuzungumza na vijana wanaopata mafunzo hayo pamoja na watendaji wa vijiji
mbalimbali wa kata hizo waliofika viwanjani hapo. Wengine kushoto ni Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga, Mkuu wa Wilaya
hiyo, Nyabaganga Taraba na kulia ni Afisa kutoka Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji,
Yusuf Kambi.
Vijana wanaopitia mafunzo ya mgambo wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kishapu,
Ngabaganga Taraba wakati akitoa nasaha zake kwao alipofungua mafunzo hayo kata
za Ukenyenge na Mwaweja wilayani humo.
Vijana wakipita kwa ukakamavu mbele ya Mkuu wa Wilaya ambaye pia ni Mwenyekiti
wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kishapu, Ngabaganga Taraba pamoja na
viongozi mbalimbali walipoonesha namna wanavyopata mafunzo hayo kutoka kwa
wakufunzi wao.
Sehemu ya wananchi na watendaji wa vijiji mbalimbali vya kata za Ukenyenge na
Mwaweja wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kishapu wakati akizungumza alipofungua
mafunzo ya mgambo wilayani humo. Kushoto ni Mshauri wa Mgambo Wilaya, Charles
Lyambisha.
Sehemu ya wananchi na watendaji vijiji wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya na Mwenyekiti
wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Kishapu, Ngabanga Taraba wakati
akifungua mafunzo ya mgambo kata za Ukenyenge na Mwaweja.
No comments:
Post a Comment