Monday, July 25, 2016

KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI YAKAMILISHA WASHINDI 100 WA PROMOSHENI YA TUSKER FANYA KWELI UWINI

  Meneja wa Bia ya Tusker Jasper Migambile akitoa ufafanuzi wa jambo wakati wa droo ya mwisho ya Milioni 100 na Tusker Fanya Kweli Uwini iliyofanyika mwishoni mwa wiki.
 Meneja wa Bia ya Tusker Jasper Migambile(kushoto) akiongea kwa njia ya simu na mmoja wa washindi wa droo ya mwisho ya Tusker Fanya Kweli Uwini wakati wa droo hiyo, kushoto kwake ni mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini Emmanuel Ndaki akihakiki taarifa za mshindi na kulia ni mshindi wa kwanza wa promosheni hiyo Michael Mwinuka akifwatilia kwa makini.
  Mshindi wa kwanza wa promosheni ya Tusker Fanya Kweli Uwini Michael Mwinuka(kulia) akichanganya vocha wakati wa droo ya mwisho ya promosheni hiyo huku akishuhudiwa na Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini Emmanuel Ndaki pamoja na Meneja wa Bia ya Tusker Jasper Migambile(kushoto) pamoja na Meneja wa Bia ya Tusker Jasper Migambile(kushoto)
Mshindi wa kwanza wa promosheni ya Tusker Fanya Kweli Uwini Michael Mwinuka(kulia) akimkabidhi vocha yenye jina la mshindi Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini Emmanuel Ndaki wakati wa droo ya mwisho iliyofanyika mwishoni mwa wiki.

Kampuni ya Bia ya Serengeti kupitia bia yake ya Tusker mwishoni mwa wiki iliyopita imechezesha droo ya 9 na ya mwisho ya promosheni ya Milioni 100 na Tusker Fanya Kweli Uwini. Droo hiyo iliyofanyika katika studio za ITV inakamilisha washindi 100 wa promosheni hiyo ambao wamepata Tsh 1,00,000 kila mmoja na kukamilisha jumla ya Tsh 100,000,000 iliyoahidiwa na kampuni hiyo kwa watumiaji wa bia ya Tusker.

Droo ya mwisho ya Milioni 100 na Tusker Fanya Kweli Uwini ilikua ya namna yake kwani ilichezeshwa na moja ya washindi waliopita wa promosheni hiyo ambaye alijishindia Milioni moja katika droo ya kwanza ya promosheni na kushuhudiwa na wakaguzi wa mahesabu na maofisa kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha nchini. 

Washindi wafuatao walitangazwa kuwa washindi wa droo ya tisa ya Tusker Fanya Kweli Uwini - Jane Mchaki na Lilian Mateme kutoka Kilimanjaro, Ramadhani Mwagace kutoka Iringa, Angelo Caruso kutoka Morogoro, Nyango J. Nyango kutoka Mwanza, Kasmiry Membe kutoka Tabora, Tina John, Mpate Mpate, Gerard Kaganda pamoja na Liberatus Massawe kutoka Dar es Salaam.

Akizingumza wakati wa droo hiyo Meneja wa Bia ya Tusker Jasper Migambile alisema kuwa, “Tumekamilisha washindi 100 na tayari tumeshatoa Tsh 100,000,000 kwa wateja wetu na washindi wa promosheni ya Tusker Fanya Kweli Uwini tuliyoiendesha kwa muda wa wiki kumi. 

Promosheni iliyokua imejaa fursa kwa wateja wetu, tunaamini umebadili maisha ya wengi kupitia hii promosheni hivyo ni dhahiri kuwa tumefanikiwa kwa kiwango kikubwa kufikia malengo yetu kwani tumekuwa na washindi ambao walitumia pesa tuliyowapa katika biashara, kulipa ada za shule, ujenzi na mengine mengi ya kimaendeleo. Tumemaliza rasmi droo na kutoa Milioni moja kwa washindi lakini bado bia kibao za bure zitakua sokoni kwaajili ya wateja wetu na watumiaji waTusker.”

Pia alitoa shukrani kwa niaba ya Kampuni ya Bia ya Serengeti kwa wadau wote waliofanikisha droo zote tisa na promosheni yote kwa ujumla. “Kwa namna ya pekee kabisa napenda kuwashukuru wana habari kwa mchango wao mkubwa kuwataarifu watanzania na wateja wetu yote yanayojiri katika promosheni hii, mmekua daraja kati yetu na wateja wetu hivyo tunashukuru sana. 

Pia sitakua na fadhila nisipowashukuru watu hawa muhimu na mihimili ya droo zetu zote Bodi ya michezo ya kubahatisha nchini na wakaguzi wa mahesabu, wamefanya kazi ya kikamilifu na ndio maana leo tunahitimisha droo ya mwisho chini ya uangalizi wao” aliongeza Jasper.

Siku zote droo za promosheni hiyo huchezeshwa na muwakilishi kutoka Kampuni ya Bia ya Serengeti lakini hii ilikua kinyume ambapo mshindi wa kwanza wa promosheni hiyo ndiye aliyechezesha droo hiyo na kuokota majina kumi ya mwisho. “Mimi nilishinda katika droo ya kwanza ya promosheni hii na kujishindia Milioni moja iliyonisaidia sana kulipa ada za shule kwa watoto wangu, ilikuja wakati muafaka kabisa muda wa watoto kufungua shule baada ya likizo ya mwezi Juni. 

Tusker iliniaokoa sana na sasa sina mawazo ya watoto wapo shule na mimi naendelea na mshughuli zangu za kujenga Taifa”. Alisema Michael Mwinuka mmoja wa washindi wa droo ya kwanza ya promosheni ya Tusker na ndiye aliyechezesha droo ya 9.

Naye mkaguzi kutoka Bodi ya michezo ya kubahatisha nchini Emmanuel Ndaki alitoa tamthmini yake juu ya promosheni hiyo mara baada ya droo ya mwisho kumalizika, “niwapongeze sana Kampuni ya Bia ya Serengeti kupitia bia ya Tusker kwa kufuata vigezo vilivyowekwa na bodi kwa kuendesha promosheni ya Milioni 100 na Tusker Fanya Kweli Uwini kikamilifu”.

‘Tusker Fanya Kweli Uwini’ ni promosheni iliyoanza takribani wiki tisa zilizopita mikoa yote nchini na leo imekamilisha washindi 100 na kufungwa rasmi kwa droo za promosheni hiyo.  

No comments:

Post a Comment