Thursday, June 23, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIMU.TV: Chama cha wajane nchini kimeiomba serikali kufanya marekebisho kwa sheria inayowahusu wajane ili kutoa nafasi ya kupata mirathi sawa na wanaume;https://youtu.be/OHnQD2L4whQ

SIMU.TV: Muamko mdogo wa elimu na matumizi ya muda mrefu kutafuta maji vinaelezwa kuwa ni changamoto kubwa zinazoathiri maendeleo ya wananchi wilayani Hanang;https://youtu.be/UJGUmOS2dfY

SIMU.TV: Takribani kaya 100 mkoani Pwani zimekabidhiwa msaada wa vyakula kwa ajili ya mfungo wa mwezi wa ramadhani huku jamii ikiaswa kusaidia jamii zenye uhitaji;https://youtu.be/ytwhkCXYALk

SIMU.TV: Waziri mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mashindano ya kuhifadhi Quran jijini Dar es salaam; https://youtu.be/aw3l0McDVro

SIMU.TV: Halmashauri ya wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera kupitia kamati yake ya kudhibiti magendo imekamata tani 5 za kahawa zikisafirishwa kwenda nje ya nchi kimagendo;https://youtu.be/8h-O8nY3uGs

SIMU.TV: Mamlaka ya mapato nchini TRA imewataka walipa kodi kutumia miamala halali ya kulipia kodi ili kukwepa walanguzi wa kodi maarufu kama vishoka;https://youtu.be/L9KCysJJxCY

SIMU.TV: Serikali imekamilisha taratibu taratibu zote za kumiliki kwa asilimia 100 kampuni ya TTCL baada ya kununua hisa 35 kutoka kwa mwekezaji wa zamani;https://youtu.be/qnwUxblZkRg

SIMU.TV: Uongozi wa klabu ya soka ya Simba umesema wachezaji wa timu hiyo wanatarajia kuingia kambini wiki ijayao kujiandaa na mzunguko wa ligi msimu ujao;https://youtu.be/LgIdnTDLGKg

SIMU.TV: Mechi kati ya klabu ya Yanga na TP Mazembe ya DRC Congo itachezwa saa kumi aalasiri baada ya mpango wa kuhamishia usiku kugonga mwamba; https://youtu.be/HA-TSzs899s

SIMU.TV: Timu ya soka ya JKT Oljoro imepata msaada wa vifaa vya michezo vyenye thamani ya shilingi milioni 3 kutoka kwa kampuni ya bima ya Sanlam life insurance;https://youtu.be/CHkVb1WOlTA

SIMU.TV: Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uingereza na klabu ya Leceister City Jamie Vardy amesaini mkataba mpya wa miaka 4 klabuni hapo na kuzima ndoto za Arsenal kupata saini ya mchezaji huyo; https://youtu.be/06YfLjKQBto

SIMU.TV: Rais Dr John Magufuli amerejesha shilingi bilioni 12 kwa tume ya taifa ya uchaguzi ili zitumike kujengea majengo ya tume ya taifa ya uchaguzi NEC.https://youtu.be/ScNA8-fktug

SIMU.TV: Rais amemteua Profesa Makenya Maboko kuwa mwenyekiti wa bodi ya shirika la viwango nchini TBS na Dr Omari Ally Amiri kuwa naibu mkurugenzi wa mamlaka ya uvuvi wa bahari kuu. https://youtu.be/Lrb_TeqQ5ag
SIMU.TV: Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro imeagizwa kuweka utaratibu mzuri wa kupeleka chakula kwa wananchi wa tarafa ya ngorongoro kwa wakati.https://youtu.be/739fOxKHvXY

SIMU.TV: Benki ya dunia imekubali kutoa dola za Marekani milioni mia tano ili kuboresha sekta ya nishati nchini. https://youtu.be/A6V2951PeCM

SIMU.TV: Zaidi ya abiria 50 waliokuwa wakisafiri na basi la Buti la zungu kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam wamenusurika kifo baada ya basi hilo kupata ajali iliosababishwa na kifusi kilichokuwa njiani. https://youtu.be/dARdqa7zV8c

SIMU.TV: Mmiliki wa gazeti la Dira ya mtanzania amemuomba radhi waziri wa katiba na sheria kwa kwa kuandika habari za kumtuhumu kuhusika na utapeli wa bilioni 2.https://youtu.be/57E-KJKyP10

SIMU.TV: Benki ya dunia imeipatia msaada mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF kwa ajili ya kuendelea kusadia kaya maskini nchini. https://youtu.be/PH1v6tUJqt8

SIMU.TV: Serikali imechukua hisa zake zilizokua zikimilikiwa na BAT Airtel kwa kampuni ya simu ya TTCL na kuzirejesha serikalini. https://youtu.be/wVdj2kM9nPo

SIMU.TV: Mamlaka ya mapato nchini TRA imetumia siku ya kilele cha utumishi wa umma kwa kuzungumza na wateja wake ili kuona kama wanaridhika na huduma za TRA.https://youtu.be/lvVADn_nEUQ
SIMU.TV: Benki ya Barclays imezindua tawi jipya la kutoa huduma za kibenki kwa wateja wake kwenye jingo la Dar city Mall. https://youtu.be/DhkI5J-WhaU

SIMU.TV: Serikali imeshauriwa kuendelea kuwaandaa wanawake kushiriki katika fursa za uongozi katika sekta za umma na binafsi. https://youtu.be/a2QQH9j6QRM
SIMU.TV: Benki ya KCB imeahidi kuwapatia mikopo wafanyabiashara wadogo na wakubwa ili kuwawezesha kuendeleza biashara zao. https://youtu.be/YWVxMm17GRE
SIMU.TV: Miundo mbinu mibovu na upangaji wa matokeo vimetajwa kuwa sababu zilizofanya michezo ya ligi kuu Tanzania kutokuingizwa kwenye michezo ya kubahatisha.https://youtu.be/gDp2Yi_-g0o

SIMU.TV: Ombi la klabu Yanga la mchezo wao kuchezwa siku ya jumatano limekataliwa na shirikisho la soka barani Afrika CAF na kubakia siku ya jumanne kama ilivyopangwa.https://youtu.be/k4svMDKFiIM

SIMU.TV: Usaili kwa ajili ya mashindano ya Club raha leo show unatarajia kuanza kesho katika viwanja vya Coco beach ambapo utafanyika kwa siku tatu.https://youtu.be/j9tH9Ghfr3A

SIMU.TV: Mshanbuliaji wa Leicester city  Jemmy Vard ameongeza mkataba na klabu yake hiyo na kuachana na mipango ya kujiunga na klabu ya Arsenal.https://youtu.be/26qb4S6LGsI
SIMU.TV: Jumla ya mataifa 16 yametinga katika hatua ya mtoano kwenye mashindano ya EURO 2016 yanayo endelea nchini Ufaransa. https://youtu.be/naOz2Ata3Oc

No comments:

Post a Comment