Monday, June 27, 2016

Maombi Maalumu Kwa Ajili ya Kumuombea Rais Magufuli na Tanzania Katika Kanisa la IEAGT Shinyanga



Hapa ni ndani ya kanisa la The International Evangelical Assemblies Of God –Tanzania (IEAGT) lililopo katika kata ya Kambarage katika manispaa ya Shinyanga ambapo leo Jumapili Juni 26,2016 kumefanyika Maombi Maalumu kwa ajili ya taifa la Tanzania, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli,makamu wa rais,bunge,mahakama,polisi na viongozi mbalimbali wa serikali.
Maombi hayo yameongozwa na askofu wa kanisla la (IEAGT) David Elias Mabushi na kuhudhuriwa na kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Josephine Matiro ambaye ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga.
Maombi hayo pia yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali,vyama vya siasa,mashirika,waandishi wa habari,wageni mbalimbali na waumini wa kanisa hilo.
Pamoja na maombi hayo maalumu, Kanisa hilo  limeadhimisha siku ya watoto katika kanisa hilo ambapo pia Juni 26 ni siku ya kuzaliwa kwa askofu wa kanisa la IEAGT David Mabushi ambaye leo ametimiza umri wa miaka 53.
Sambamba na matukio hayo mawili makubwa,kanisa hilo pia lilikabidhi madawati 20 kwa uongozi wa wilaya ya Shinyanga kwa ajili ya kumuunga mkono rais Magufuli katika jitihada zake za kuhakikisha kuwa changamoto ya madawati inamalizika katika shule.
Awali akisoma risala,Katibu wa kanisa la IEAGT, Mchungaji Obed Jilala alisema baada ya uchaguzi mkuu 2015,kanisa la IEAGT limekuwa likisikia kwa nyakati tofauti rais Magufuli akiomba maombi kwa ajili ya kazi yake ya kuliongoza taifa,hivyo kanisa lao limeguswa sana na kauli hiyo na katika kuonesha wanamuunga mkono walikubaliana siku ya Jumapili Juni 26,2016 iwe ya maombi maalumu kwa ajili ya kiongozi wa taifa sambamba na kuliombea nchi ya Tanzania.
"Maombi haya yamebebwa kwa kiasi kikubwa na upendo tulio nao kwa nchi yetu ,kanisa la IEAGT kama sehemu ya jamii ya watanzania tumeona siku ya leo iwe kilele cha maombi ya kitaifa katika mkoa wetu na mahali popote lilipo kanisa letu",aliongeza Mchungaji Jilala.
Naye Askofu wa kanisa hilo David Mabushi akitoa mahubiri yake,mbali na kumpongeza rais Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa rais,alimuomba kuendelea kuonesha msimamo wake katika kuwaletea maendeleo watanzania huku akimfananisha na Nabii Musa akisema Magufuli amekuja kuiokomboa nchi na kuifanya kuwa nchi ya asali na maziwa.
"Tumeandaa siku hii muhimu kwa ajili ya kuiombea nchi yetu ili iendelee kuwa na amani,tunamuombea rais wetu kwa sababu wenye haki wakiwa na amri,watu hufurahi..sisi kama kanisa tutahakikisha tunamuunga mkono rais Magufuli kwa maneno na vitendo ndiyo maana leo tunatoa sadaka ya madawati 20,tunaomba watanzani waendelee kumuombea rais wetu aliyeonesha kuwajali watanzania tangu alipoingia madarakani amekuwa mstari wa mbele kupigana dhidi ya rushwa na vitendo vyote viovu",aliongeza askofu Mabushi.
Kwa upande wake mgeni rasmi Kaimu Mkuu wa mkoa wa Shinyanga ,Josephine Matiro ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro,alilipongeza kanisa hilo kuona umuhimu wa kuombea viongozi wa nchi na kuongeza kuwa kanisa la IEAGT ni kanisa la kwanza mkoani Shinyanga kufanya maombi kwa ajili ya viongozi wa nchi.
"Ndugu zangu watanzania naomba tuendelee kuiombea nchi ili iendelee kuwa ya amani na viongozi kuwa na hofu ya mungu,lakini pia naomba watanzania wafanye kazi,sasa ni muda wa kuchapa kazi tuache siasa za majukwaani,tumuunge mkono mheshimiwa rais katika kutekeleza kauli mbiu ya Hapa Kazi tu",aliongeza Matiro.
Miongoni mwa mambo yaliyoombewa katika ibada hiyo ni kuombea taifa,kumuombea rais Magufuli,makamu wa rais,waziri mkuu na viongozi wengine wa serikali,kuombea bunge na madiwani,kuombea mahakama na katika maeneo yote viongozi wa dini waliwataka viongozi hao kuwa hofu ya mungu na kuchukia rushwa pamoja na kutumia nguvu zao kupambana na vitendo vya kihalifu ikiwemo mauaji ya watu kwenye nyumba za ibada,vikongwe,albino na watu mbalimbali wasio na hatia.
Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog, Kadama Malunde alikuwepo kuanzia mwanzo mpaka mwisho…ametuletea picha 74 tazama hapa chini…
Mshereheshaji mkuu(MC) Thomas Batenga ambaye pia ni mjumbe wa bodi ya wakurugenzi katika kanisa la IEAGT akitambulisha wageni mbalimbali kanisani
Wanakwaya wa kwaya ya BBC ya kanisa la IEAGT wakiimba kanisani wakati wa Ibada maalum ya maombi kwa ajili ya nchi ya Tanzania,maadhimisho ya siku ya watoto wa kanisa hilo na zoezi la kukabidhi madawati kwa uongozi wa serikali ya wilaya ya Shinyanga.
Meza kuu wakiwa na mgeni rasmi,kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga Josephine Matiro(wa pili kutoka kulia),ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga.Wa kwanza ni kulia ni mwakilishi wa mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga Grace Haule ambaye pia ni katibu wa UWT wilaya ya Shinyanga vijijini,wa pili kutoka kushoto ni naibu meya wa manispaa ya Shinyanga mheshimiwa Agnes Machiya
Kushoto ni askofu wa kanisa la IEAGT David Mabushi akiwa na katibu mkuu wa kanisa hilo Mchungaji Obed Jilala wakiwa kanisani
Watoto wa kanisa la IEAGT wakiimba na kucheza kanisani ikiwa leo Jumapili,Juni 26,2016 ni siku ya watoto wa kanisa hilo lililopo nyuma ya shule ya msingi Jomu mjini Shinyanga
Watoto na waumini wengine wa kanisa hilo wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea kanisani
BBC kwaya wakiimba kanisani
Tunafuatilia kinachoendelea kanisani....
Askofu wa kanisa la IEAGT David Mabushi akizungumza kanisani
Waumini wa kanisa la IEAGT wakitafakari kanisani
Watoto wakiwa kanisani
Waumini wa kanisa hilo wakiwa kanisani
Tunafuatilia kinachoendelea kanisani......
Mashemasi wa kanisa la IEAGT wakiimba kanisani
Mahubiri kwa njia ya wimbo yakiendelea
Wanakwaya wa kwaya ya BBC wakiwa wamekaa kanisani
Waandishi wa habari(mstari wa mbele) wakiwa kanisani
Watoto wakiimba wimbo maalumu kuiombea nchi ya Tanzania na jamii kwa ujumla huku wakihamasisha wazazi na walezi kudumisha upendo kwa watoto
Watoto wakiimba huku wamelala ..Miongoni mwa maneno yaliyokuwa yanasikika ni...."Dunia ni mbaya..changamka itakupoteza..."
Wageni waalikwa wakiwa kanisani
Katibu mkuu wa kanisa la IEAGT ,Mchungaji Obed Jilala akisoma risala wakati wa maombi hayo maalumu kwa ajili ya Tanzania,rais Magufuli na viongozi mbalimbali wa serikali.Mchungaji Jilala pia ni diwani wa kata ya Lubaga katika manispaa ya Shinyanga kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo( CHADEMA).
Katibu wa kanisa hilo Mchungaji Jilala alisema baada ya uchaguzi mkuu 2015,kanisa la IEAGT limekuwa likisikia kwa nyakati tofauti rais Magufuli akiomba maombi kwa ajili ya kazi yake ya kuliongoza taifa,hivyo kanisa lao limeguswa sana na kauli hiyo na katika kuonesha wanamuunga mkono walikubaliana siku ya Jumapili Juni 26,2016 iwe ya maombi maalumu kwa ajili ya kiongozi wa taifa sambamba na kuliombea nchi ya Tanzania
Watoto wakiimba kanisani
Wazee wa kanisa la IEAGT wakiwa kanisani
Tunafuatilia kinachoendelea kanisani....
BBC kwaya wakiimba wimbo maalumu wa kuiombea nchi ya Tanzania
Waumini wakiwa kanisani
Askofu wa kanisa la The International Evangelical Assemblies of God –Tanzania (IEAGT) David Mabushi akitoa mahubiri wakati wa ibada maalumu ya kumuombea rais Magufuli na taifa la Tanzania.Alitumia fursa hiyo kuwataka viongozi wa Tanzania kuwa na hofu ya mungu hali itakayosaidia kupunguza maovu mbalimbali katika jamii 
Waumini wakiwa kanisani...
Ibada inaendelea
Waumini wakimsikiliza Askofu Mabushi
Askofu Mabushi akimuombea rais Magufuli ili aongoze taifa vizuri
Askofu Mabushi akiendelea kufanya maombi kwa ajili ya rais Magufuli
Meza kuu wakimuombea rais Magufuli 
Maombi yanaendelea
Waumini wakimuombea rais Magufuli na nchi ya Tanzania
Ibada ya maombi maalumu kwa ajili ya rais Magufuli inaendelea
Maombi yanaendelea....watumishi wa mungu wasoma biblia
Waumini wakimuombea rais Magufuli ili aongoze nchi kwa hekima na busara,awe na afya njema,asimamie kwa haki na uadilifu awe mlinzi wa nchi na kuwa chanzo cha baraka za nchi
Askofu Mabushi na katibu wa kanisa la IEAGT Mchungaji Jilala wakiliombea taifa la Tanzania ili liwe na amani na salama
Maombi kwa ajili ya taifa la Tanzania yakiendelea
Mchungaji Mabushi akiwa na Katibu wa kanisa la IEAGT Mchungaji Obed Jilala wakiwa wameshikilia bendera ya Tanzania wakati wa kuliombea taifa
Waumini wakiombea nchi ya Tanzania
Maombi yanaendelea
Wazee wa kanisa wakiwa kanisani
Maombi yanaendelea
Meza kuu wakiliombea taifa la Tanzania
Maombi yanaendelea..
Mchungaji Mabushi akiendelea kuombea nchi ya Tanzania
Waumini wakitafakari wakati wa maombi hayo
Askofu Mabushi akimuombea Mgeni rasmi/Mkuu wa wilaya ya Shinyanga kwa niaba ya viongozi wote wa nchi ya Tanzania
Askofu Mabushi akiwaombea viongozi wote Tanzania 
Meza kuu wakiwa wamesimama kanisani
Tunafuatilia kinachoendelea kanisani...
Mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga ambaye pia ni mwenyekiti wa ALAT,mheshimiwa Gulam Hafeez Mukadam akizungumza kanisani ambapo alilipongeza kanisa hilo kwa kufanya maombi maalumu kwa ajili ya viongozi wa nchi
Watoto wakiimba wimbo maalumu kwa ajili ya kuiombea nchi ya Tanzania na viongozi wake ili watawale kwa haki
Haya ni miongoni mwa madawati 20 yaliyotolewa na kanisa la IEAGT kama sadaka kwa ajili ya shule zilizopo katika wilaya ya Shinyanga ikiwa ni kuunga mkono jitihada za rais Magufuli katika kumaliza tatizo la uhaba wa madawati katika shule
Kulia ni Askofu wa kanisa la IEAGT David Mabushi akijiandaa kukabidhi madawati kwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro (kushoto)
Zoezi la kukabidhi madawati linaendelea
Mgeni rasmi mheshimiwa Josephine Matiro akitoa salamu za serikali wakati wa ibada hiyo 
Matiro alilipongeza kanisa hilo kwa kuandaa ibada kwa ajili ya kumuombea rais Magufuli na kuwataka watanzania kumuunga mkono kwa vitendo badala ya kuendesha mijadala kwenye majukwaa ya kisiasa na kuongeza kuwa hivi sasa ni muda wa kufanya kazi tu na sio vinginevyo
Pamoja na mambo mengine Matiro aliwataka wazazi na walezi kuwa karibu na watoto wao kuhakikisha wanasoma na kuwaepusha dhidi ya ndoa na mimba za utotoni
Mjumbe wa bodi wa wadhamini katika kanisa hilo Ezekiel Honga akitoa neno la shukrani baada ya ibada ya maombi kumalizika
Mgeni rasmi na wageni waalikwa wakiwa katika picha ya pamoja
Mgeni rasmi,viongozi wa kanisa,wageni waalikwa na wazee wa kanisa wakiwa katika picha ya pamoja
Mgeni rasmi,viongozi wa kanisa,wageni waalikwa na mashemaji wa kanisa hilo wakiwa katika picha ya pamoja
Picha ya kumbukumbu mgeni rasmi,wageni waalikwa na viongozi wa kanisa
Mgeni rasmi na watoto
Picha zikaendelea kupigwa
Waimba kwaya ya BBC nao wakapiga picha na mgeni rasmi
Kanisa la IEAGT lipo nyuma ya shule ya msingi Jomu mjini Shinyanga...Pichani ni mgeni rasmi Josephine Matiro(mwenye nguo nyeusi) akiangalia choo cha shule ya msingi Jomu kilichojengwa na kanisa hilo 
Hili ni tundu la choo kati ya matundu 8 katika choo kilichojengwa na kanisa la IEAGT katika shule ya msingi Jomu
Meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam(mwenye miwani),nyumba yake ni askofu wa kanisa la IEAGT David Mabushi wakiwa wameongozana na mgeni rasmi(haonekani) wakitoka kuangalia choo cha wanafunzi katika shule ya msingi Jomu
Mgeni rasmi Josephine Matiro akitoka kuangalia choo cha wanafunzi katika shule ya msingi Jomu
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akitoka katika choo hicho
Muonekano wa choo kwa mbali (kushoto)
Mgeni rasmi Josephine Matiro akitoka katika choo hicho,akiwa ameambatana na wageni waalikwa na viongozi wa kanisa hilo
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

No comments:

Post a Comment