Friday, June 3, 2016

Mama Janeth Magufuli aahidi kuendelea kusaidia Jamii ya Wazee na walemavu nchini

Wananchi wa Kijiji cha Nandagwa Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi wakimlaki Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli aliwapowasili eneo hilo kwa ajili ya kutoa Msaada wa Vyakula, Mafuta pamoja na Dawa kwa ajili ya Kambi ya Wazee ya Nandanga iliyopo katika kijiji hicho.
Mratibu wa kambi ya Kulea wazee na watu wenye ulemavu ya Nandanga Bw. Agnerus Chiamba akimpa maelezo Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli kuhusu nyumba za malazi katika kambi hiyo, aliwapowasili eneo hilo kwa ajili ya kutoa Msaada wa Vyakula, Mafuta pamoja na Dawa.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mh. Godfrey Zambi akimuonesha Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli nyumba za malazi katika Kambi ya Wazee na watu wenye ulemavu ya Nandanga iliyopo katika kijiji hicho aliwapowasili eneo hilo kwa ajili ya kutoa Msaada wa Vyakula, Mafuta pamoja na Dawa.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akifungua kitambaa kwenye jiwe la msingi cha zahanati ya kijiji cha Nandanga itakayorahisisha upatikanaji wa huduma ya afya kwa wakazi wa eneo hilo waliokuwa wakisafiri umbali mrefu kufuata huduma hiyo.
Baadhi ya Vitu vilivyotolewa kwa ajili msaada katika kambi ya kulea Wazee na watu wenye ulemavu ya Nandanga.
Jengo la Zahanati ya Nandanga lililozinduliwa na Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli
Mratibu wa kambi ya Kulea wazee na watu wenye ulemavu ya Nandangwa Bw. Agnerus Chiamba akimkabidhi Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli taarifa ya kambi ya Kulea Wazee ya Nandanga.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mh. Godfrey Zambi akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo kwa Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli wakati wa hafla ya utoaji misaada katika kambi ya kulea wazee ya Nandanga iliyopo Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mh. Godfrey Zambi akimkabidhi Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mh. Godfrey Zambi akiwaeleza Jambo Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli (Katikati) na Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa Wakicheza Ngoma na kikundi cha Vijana wakati wa hafla ya utoaji misaada katika kambi ya kulea wazee ya Nandanga iliyopo Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi.
Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa akiongea na wananchi wa Kijiji cha Nandanga na kumshukuru Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli kwa kutoa msaada katika kambi ya Wazee na watu wenye ulemavu iliyopo katika kijiji hicho.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli(kushoto) akikabidhi misaada kwa wawakilishi wa kambi ya kulea wazee ya Nandanga iliyopo Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi, Katikati ni Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akiongea na wananchi wa Kijiji cha Nandanga kilichopo Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi na kuahidi kuendelea kusaidia kambi hizo za wazee na watu wenye ulemavu wa ukoma ambapo mpaka sasa meshatoa msaada katika kambi 4 katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Lindi na Mtwara yenye thamani ya Takribani shilingi 250.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akipokea zawadi kutoka wawakilishi wa kijiji cha Nandanga kilichopo Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akisalimiana na baadhi ya watoto waliofika katika hafla ya utoaji misaada katika kambi ya kulea wazee ya Nandanga iliyopo Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akiagana na wananchi wa Kijiji cha Nandanga kilichopo Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi baada ya kutoa msaada katika kambi ya kulea wazee ya Nandanga iliyopo eneo hilo. PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO

No comments:

Post a Comment