Tuesday, June 28, 2016

GGM YATOA VIFAA TIBA KWA WATOTO KATIKA HOSPITALI YA MUHIMBILI.

WAFANYAKAZI wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita(GGM) wametoa msaada wa vifaa tiba kwa watoto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam leo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,  Daktari Mkuu wa Mgodi wa Dhababu wa Geita (GGM), Kiva Mvungi amesema kuwa Msaada uliotolewa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili katika kitengo cha watoto ni wadhamani ya shilingi milioni 23.

Pia amesema kuwa msaada huo ni kwaajili ya kusaidia jitihada Serikali katika kuboresha huduma za Afya hasa katika kitendo cha watoto katika hospitali hiyo.
Nae Mkuu wa Idara ya watoto katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Mary Charles aliwashukuru wafanyakazi wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita(GGM) kwa kutoa msaada katika Hospitali hiyo.
"Lengo la ni kuwa sehemu ya Jamii ambapo uwepo wa Mgodi unaleta manufaa kwa jamii inayozunguka." Alisema Mvungi.

Vifaa vilivyotolewa na Mgodi wa Dhahabu wa Geita wa GGM katika Hospitali ya Muhimbili leo ni Bp Machine 10, Infrsion Pump 2 Themometers 6110, Standing Weighing Scale 6, Nebulises 3 na Pulse Oxymeter 10.

 Daktari Mkuu wa Mgodi wa Dhababu wa Geita (GGM), Kiva Mvungi (Wapili kulia) akikabidhi msaada wa Vifaa vya matibabu kwa watoto kwa Chama cha madaktari wa watoto Tanzania ukipokelewa na Mkuu Mawasiliano ya Umma katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Aminiel Aligaesha.
 Bara baada Mkuu Mawasiliano ya Umma wa Hospitali ya Taifa yaMuhimbili, Aminiel Aligaesha kukabidhiwa msaada wa vifaa tiba kwa watoto naye akakabidhi Msaada huo uliotolewa na Mgodi wa Dhababu wa Geita (GGM) kwa Mkuu wa Idara ya watoto katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Mary Charles jijini Dar es Salaam leo.
 Daktari Mkuu wa Mgodi wa Dhababu wa Geita (GGM), Kiva Mvungi akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada wa vifaa tiba katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkuu wa Idara ya watoto katika hospitali ya Taifa ya Muhimili, Mary Charles jijini Dar es Salaam leo.
Mkuu wa Idara ya watoto katika hospitali ya Taifa ya Muhimili, Mary Charles  akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo pamoja na kuwashukuru wafanyakazi wa Mgodi wa Geita wa GGM walipotoa msaada katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili katika Kitengo cha watoto. 
 Makamu wa Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania na  Daktari Bingwa wa Watoto katika Hopitali ya Tiafa ya Muhimbili, Namala Mkopi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kukabidhiwa Msaada uliotolewa na wafanyakazi wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita wa GGM.

No comments:

Post a Comment