Thursday, May 5, 2016

Wateja wa KLM sasa kununua tiketi kwa M-Pesa

Ofisa Mtendaji Mkuu wa kitengo cha huduma za kibiashara na makampuni  wa Vodacom Tanzania,Gregory Verbond(Kushoto aliyekaa)na Meneja mkuu wa Shirika la Ndege la KLM nchini,Sharad Khuller(kulia)wakisaini mkataba wa ushirikiano kwa ajili ya wateja wa KLM kulipia tiketi zao za kusafiri kupitia huduma ya M-Pesa,Mkataba huo ulisainiwa jijini Dar es Salaam leo,Anaeshuhudia katikati ni Kaimu Ofisa Mkuu wa kitengo cha Kifedha wa Vodacom Tanzania,(M-Commerce),Sitoyo Lopokoiyit.
Kaimu Ofisa Mkuu wa kitengo cha Kifedha wa Vodacom Tanzania,(M-Commerce),Sitoyo Lopokoiyit(katikati)akishuhudia Ofisa Mtendaji Mkuu wa kitengo cha huduma za kibiashara na makampuni  wa Vodacom Tanzania,Gregory Verbond(Kushoto)na Meneja mkuu wa Shirika la Ndege la KLM nchini,Sharad Khuller wakibadilishana mikataba baada ya kuisaini kwa ajili ya wateja wa KLM kulipia tiketi zao za kusafiri kupitia huduma ya M-Pesa,Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam leo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa kitengo cha huduma za kibiashara na makampuni  wa Vodacom Tanzania,Gregory Verbond(Kushoto)na Meneja Mkuu wa Shirika la Ndege la KLM nchini,Sharad Khuller(kulia)wakielekeza jinsi ya kukata tiketi kupitia huduma ya M- PESA na Kaimu Ofisa Mkuu wa kitengo cha Kifedha wa Vodacom Tanzania,(M-Commerce),Sitoyo Lopokoiyit(katikati) wakati wa hafla ya kusainiana mkataba kwa ajili ya wateja wa KLM kulipia tiketi zao za kusafiri kupitia huduma hiyo,Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam leo.
Meneja Mkuu wa Shirika la Ndege la KLM nchini,Sharad Khuller(kulia)akimsisitiza jambo Ofisa Mtendaji Mkuu wa kitengo cha huduma za kibiashara na makampuni  wa Vodacom Tanzania,Gregory Verbond,baada ya kusainiana mkataba kwa ajili ya wateja wa KLM kulipia tiketi zao za kusafiri kupitia huduma ya M- Pesa,Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja na Kaimu Ofisa Mkuu wa kitengo cha Kifedha wa Vodacom Tanzania,(M-Commerce),Sitoyo Lopokoiyit(kushoto) Ofisa Mtendaji Mkuu wa kitengo cha huduma za kibiashara na makampuni  wa Vodacom Tanzania,Gregory Verbond(wanne toka kushoto)pamoja na Meneja Mkuu wa Shirika la Ndege la KLM nchini,Sharad Khuller(watano toka kushoto) wakati wa hafla ya kusainiana mkataba kwa ajili ya wateja wa KLM kulipia tiketi zao za kusafiri kupitia huduma ya M-PESA,Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam leo.

Wateja wa Shirika la ndege la Uholanzi la KLM watakaokuwa wanatumia usafiri wa anga kuanzia sasa wataweza kulipia tiketi zao za kusafiri kupitia huduma ya M-Pesa,Hiyo imekuja baada ya kusainiwa kwa makubaliano ya kutoa huduma hiyo kwa Kampuni hiyo na Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania leo.Huduma hii imekuwa inatumiwa na makampuni mbalimbali kupokea malipo na kuwarahisishia wananchi maisha.

Wateja wa shirika la KLM pia sasa wataweza kulipia huduma mbalimbali kupitia M-Pesa badala ya kupoteza muda kutembelea ofisi za shirika hilo na mawakala wake baadhi ya huduma hizo zikiwa ni kununua tiketi za safari,kulipia mizigo ya ziada,malipo ya kuahirisha safari.

Akiongea kuhusu ushirikiano huu Ofisa Mtendaji Mkuu wa kitengo cha huduma za kibiashara na makampuni wa Vodacom Tanzania,Gregory Verbond,alisema “Tunayo furaha kufanya kazi na shirika la KLM ambapo sasa wateja wetu maisha yao yamezidi kurahisishwa sasa wanaweza kupata huduma za shirika hili kupitia simu zao za mkononi kwa kufanya malipo kwa M-Pesa”.

Verbond aliongeza kuwa mtandao wa M-Pesa hivi sasa unatumiwa na taasisi na makampuni mbalimbali ya serikali na binafsi katika kurahisisha kupokea malipo kwa urahisi kutoka kwa wateja wao na imethibitika kuwa njia inayorahisisha maisha,kuokoa muda na ni salama.

Aliyataja baadhi ya mashirika ya ndege ambayo kwa sasa wateja wake wanafanya malipo kupitia huduma hii kuwa ni Qatar Airways, Precision Air, Kenya Airways, Air Tanzania, Fast Jet, Eagle Air na Auric Air.

Kwa upande wake Meneja wa Shirika la KLM nchini,Sharad Khuller alisema kuwa wamejiunga na huduma ya M-Pesa kutokana na maombi ya wateja wake katika kuwarahishia maisha kwa kulipia huduma wanazohitaji hususani kununua tiketi za safari za kwenda nchi mbalimbali duniani,Huduma kwa wateja kwa kampuni yetu ni kitu muhimu sana kwa KLM.

Ushirikiano huu na Vodacom Tanzania kupitia huduma ya M-PESA ni njia muhimu sana kwa kutoa huduma zilizo bora kwa wateja wetu ni huduma inayowafanya wateja wawe huru kwa kulipia tiketi zao kwa haraka na bila usumbufu,alisema Khuller

Kupata huduma hii anachopaswa kufanya mteja ni kupiga namba*150* 00#,ambapo kwenye menu ya simu yake atachagua huduma namba 4 inayoelekeza kulipa kwa M-Pesa,baadaye atachagua huduma namba 3,kuchagua aina ya biashara ni namba 9,kisha atachagua namba 3 inayoonyesha huduma za usafiri na mwisho atachagua KLM

No comments:

Post a Comment