Wednesday, May 4, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

Simu.tv: Waziri wa habari, Sanaa, utamaduni na michezo Nape Nnauye asema serikali iko tayari kukaa meza moja na wadau wa habari pamoja na bunge ili kupata namna bora ya urushaji matangazo ya bunge. https://youtu.be/_M_jAt5XF00
 Simu.tv: Katika kuadhimisha siku ya uhuru wa habari waandishi wa habari mkoani Mtwara watumia siku hiyo kukikumbusha serikali juu ya ujenzi wa kituo cha polisi ili kuzuia uhalifu. https://youtu.be/yFQrz46bbDI
 Simu.tv: Waziri wa kilimo, mifugo na uvuvi Mwigulu Nchemba asema kuwa serikali ya awamu ya 5 imepania kukuza sekta ya kilimo na mifugo kwa kuzalisha mazao ya biashara na kulifanya jembe la mkono kuwa historia nchini. https://youtu.be/or1-icumqyM
 Simu.tv: Jeshi la polisi mkoani Tanga limefanikiwa kuwaua watu 4 wanaosadikiwa kuwa majambazi katika mapambano yaliyodumu kwa muda katika eneo la Amboni.https://youtu.be/zAp6EIgH3XQ
 Simu.tv: Katibu mkuu wa wizara ya habari awataka waandaaji wa vipindi vya elimu kwa umma kutoka katika taaisi za umma na binafsi kuielimisha jamii juu ya mambo muhimu yanayoendelea nchini badala ya kuwapotosha. https://youtu.be/_xeEE2OX9CA
 Simu.tv: Kamati kuu ya halamashauri kuu ya CCM taifa yapitisha majina ya wabunge walioomba ujumbe wa halmashauri kuu ya CCM NEC huku ikitoa onyo kali kwa wabunge walioteuliwa. https://youtu.be/b2JmqJCik74
 Simu.tv: Shangwe, nderemo na vifijo vilirindima kwenye mji wa Leicester baada ya timu yao kunyakua ubingwa wa wa ligi kuu ya Uingereza.https://youtu.be/IFHX5QoXjP0
 Simu.tv: Kamati ya rufani ya nidhamu ya TFF yatupilia mbali rufaa zilizokatwa na viongozi na timu zilizotiwa hatiani kwa kosa la kupanga matokeo.https://youtu.be/IfjkbrArSVU
 Simu.tv: Uongozi wa soko la Ilala la jiji la Dar es salaam umehakikishiwa kutengewa fedha kwenye bajeti ijayo kwa ajili ya ukarabati wa soko hilo.https://youtu.be/Pu7aU1ZwMR4
 Simu.tv: Kampuni ya uwakala wa soko la hisa la Dar es salaam yasogeza huduma za ununuzi wa hisa mkoani Mara. https://youtu.be/8ucdXvoaC-c
 Simu.tv: Mabingwa watetezi na vinara wa ligi kuu Vodacom Yanga yaendendelea kutumbua majipu baada ya kuitumbua Stand United goli 3 kwa 1.https://youtu.be/9l2A81XFOkE
 Simu.tv: Serikali yakubali kukaa meza moja na wadau wa sekta ya habari nchini ili kutatua matatizo yanayo minya uhuru wa habari nchini.https://youtu.be/fbnCmS40W4g  
 Simu.tv: Waziri mkuu mstaafu Fredrick Sumaye asema kitendo cha wananchi kuzuiwa kuangalia bunge live ni kuondoa uhuru wa kupata habari. https://youtu.be/bh-nUCaPiwU  
 Simu.tv: Mahakama kuu inatarajia kuanza kusikiliza kesi inayowakabili aliyekuwa kamishna wa TRA Hary Kitilya na wenzake baada ya kutolewa mahakama ya hakimu mkazi Kisutu. https://youtu.be/IG4eZVS0ZYY   
 Simu.tv: Serikali imekumbushwa kuwa kitendo cha kuwanyima watanzania kuona Bunge moja kwa moja ni kuwanyima haki yao ya msingi iliyoainishwa kikatiba.https://youtu.be/GtTaV-aRNcw  
 Simu.tv: Hospitali ya Amana ya jijini Dar es Salaam yaingia kwenye mgogoro na wananchi baada madaktari wake wawili na muuguzi mmoja kudaiwa kusababisha kifo cha dereva wa bodaboda aliepigwa risasi na majambazi. https://youtu.be/5AzR8l4dI-s  
 Simu.tv: Wadau wanaopenda maendeleo wameombwa kujitokeza ili kutatua tatizo la miundombinu ya samani katika shule za msingi na sekondari ili kufanikisha lengo la serikali la kutoa elimu bure. https://youtu.be/d1BclMG_SF0  
 Simu.tv: Wakati Tanzania na Uganda zikitajwa kuwa nchi zinazozalisha zao la ndizi kwa kiasi kikubwa barani Afrika  imeelezwa kuwa kunahitajika kupatikana kwa mbegu ambayo itastahimili magonjwa na ukame. https://youtu.be/dvs03_u4Log  
 Simu.tv: Wananchi mkoani Shinyanga wamelalamikia serikali kushindwa kuthibiti kupanda kiholela kwa bei ya sukari kutoka shilingi 1800 hadi 2800 na kufanya wananchi kutomudu kununua bidhaa hiyo. https://youtu.be/siX8JQQvGbY   
 Simu.tv: Timu ya Yanga imezidi kuusogelea ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom baada ya kuifunga timu ya Stand United mabao matatu kwa moja.https://youtu.be/ONSKrvhdDW8
 Simu.tv: Kamati ya rufaa ya ligi nchini imetoa uamuuzi wa rufaa nane ziliwasilishwa baada ya kutolewa kwa adhabu iliyosababishwa na upangaji wa matokeo ya ligi daraja la kwanza. https://youtu.be/iJz_0z4-gu0  

No comments:

Post a Comment