Saturday, May 28, 2016

SHEREHE YA MAADHIMISHO MIAKA 6 YA JUMUIA YA WATANZANIA WALIOSOMEA TANZANIA (CAAT) YAFANA

Sherehe ya maadhimisho ya miaka 6 ya Chama cha Watanzania Waliosoma China kwa kiingereza China Alumni Association of Tanzania (CAAT) imefana kwa kiwango kikubwa.

Sherehe hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Cardinal Laurian Rugambwa Social Centre pembezoni mwa kanisa la Mtakatifu Peter (St Peter), Oysterbay Ijumaa ya tarehe 20-May-2016.

Mgeni rasmi wa sherehe hiyo alikuwa Prof Elisante Gabriel (Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo) akimuwakilisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye. Wageni wengine wa heshima walikuwa Counselor Gao Wei wa ubalozi wa China (ambaye alikuwa anamuwakilisha balozi Dr Lu Youqing) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika La Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (Tanzania Industrial Research Developments Organization-TIRDO) Prof Mkumbukwa Madundo Angelo Mtambo.

HISTORIA FUPI YA CAAT

•CAAT ni chama kilichoanzishwa mwaka 2010 ambapo mkutano mkuu wa kwanza wa chama (General Assembly) ulifanyika Jumapili ya tarehe 14-Nov-2010 katika ukumbi wa Rombo Green View Hotel, Sinza/Ubungo, Dar-es-Salaam (ambao hivi sasa unaitwa Rombo Hotel).

•Baada ya hapo, sherehe za uzinduzi/ufunguzi rasmi wa chama zilifanyika Alhamis ya tarehe 11-Aug-2011 katika ukumbi wa Karimjee, Dar-es-Salaam.

•Awamu ya kwanza ya uongozi ya CAAT (2010-2016) iliongozwa na Eng Fred Maiga (Mwenyekiti), Dr Haji Mwita (Makamu Mwenyekiti), Eng Mosses Swai (Katibu) na Wajumbe: Dr Paul Peter Mhame, Dr George Oreku, Ponera Ally Kacheuka, Eng Francis Mugisha, Gustav Sanga, Hawa Ngasongwa na Dr Uwesu Mchepange.

•Baada ya uchaguzi uliofanyika kwenye Mkutano Mkuu wa Jumamosi tarehe 20-Feb-2016 katika eneo la New Msasani Club viongozi wapya ni Dr Paul Peter Mhame (Mwenyekiti), William Kaijage (Makamu Mwenyekiti), George Oreku (Katibu Mkuu), Ponera Ally Kacheuka (Naibu Katibu Mkuu), Johnspeter Majura (Naibu Katibu Mkuu) pamoja na Shija Boniphace Bundala (Mweka Hazina).
Mgeni rasmi Prof Elisante Gabriel (Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo) akikata keki ya maadhimisho ya miaka 6 ya chama cha Watanzania Waliosomea China.
Mgeni rasmi Prof Elisante Gabriel (Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo) akitoa hotuba akimuwakilisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye
Mwenyekiti wa Chama cha Watanzania Waliosomea China (CAAT) Dr Paul Peter Mhame akitoa hotuba.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika La Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (Tanzania Industrial Research Developments Organization-TIRDO) Prof Mkumbukwa Madundo Angelo Mtambo akitoa hotuba.
Mgeni rasmi Prof Elisante Gabriel (Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo) akizindua rasmi tovuti ya chama cha Watanzania Waliosomea China (CAAT).
​Mgeni rasmi Prof Elisante Gabriel (Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo) akikagua maonesho ya bidhaa na huduma za kibiashara zinazotolewa na baadhi ya watanzania waliopata kusomea China.
Picha ya pamoja kati ya mgeni rasmi, wageni waheshimiwa na viongozi wa Chama cha Watanzania Waliosomea China.
Picha ya pamoja ya watanzania waliosomea China.

No comments:

Post a Comment