Thursday, May 26, 2016

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA MKUTANO WA MASHAURIANO WA BODI YA USAJILI WA MAKANDARASI NCHINI CRB.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili kwenye ukumbi wa Mikutano wa Diamond Jubilee kwa ajili ya Ufunguzi rasmi wa Mkutano wa Siku mbili wa Mashauriano wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi nchini CRB.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia Wakandarasi, Wahandisi na wadau mbalimbali wa sekta ya Ujenzi kabla ya kufungua rasmi Mkutano  wa Siku mbili wa Mashauriano wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi nchini CRB uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipewa maelezo kuhusu katapila linalotumika katika kazi mbalimbali za ujenzi mara baada ya kufungua mkutano wa siku mbili wa Mashauriano wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi jijini Dar es Salaam.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati akikagua baadhi ya mitambo na magari mbalimbali katika maonesho ya vifaa hivyo vinavyotumika katika sekta ya ujenzi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia vifaa vya ujenzi katika moja ya mabanda mara baada ya kufungua mkutano wa siku mbili wa Mashauriano wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi jijini Dar es Salaam.
 Wadau mbalimbali wa Sekta ya Ujenzi wakiwemo Wahandisi na Wakandarasi wakipiga makofi wakati wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia katika mkutano huo wa Mashauriano wa CRB jijini Dar es Salaam. 
PICHA NA IKULU.

RAIS Magufuli akemea vitendo vya ruswa kwa wakandarasi
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli amewataka wakandarasi nchini kujiepusha na vitendo vya rushwa ili kulisaidia Taifa kupiga hatua ya kimaendeleo.

Mhe. Rais Magufuli ameyasema hayo leo wakati akifungua Mkutano wa Mashauriano wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi nchini (CRB) uliofanyika jijini Dar es Salaam.

“Mnaweka viwango vikubwa vya fedha kwenye miradi ili muweze kupata fedha ya kutoa rushwa, kwa nini mnafanya hivyo?”amewauliza Mhe. Rais Magufuli na kuwambia kuwa kama wapo watumishi wa serikali wanaowaomba rushwa ili wapate kazi waitaarifu Takukuru mara moja ili wachukuliwe hatua.

Mhe. Rais amewataka wakandarasi wazawa wajipange kufanya kazi na kuwaonya wasiwe wanaweka viwango vikubwa ambavyo vinachangia kuwakosesha zabuni. 

 Akitoa mfano, Mhe. Magufuli alisema katika ujenzi wa mahakama za mwanzo hapa nchini, jengo moja lilikadiriwa kukamilika kwa milioni 200 lakini wakandarasi wa Tanzania walioomba zabuni hiyo walitoa kiwango cha kati ya shilimgi milioni  670 na bilioni 1.4. Amesema kwa jinsi hii hata mtu awe na huruma ya namna gani hawezi kuwapa kazi.

Amesema serikali yake itawajali kwanza wakandarasi wa hapa nchini lakini akawataka wajipange na pengine waungane ili kufanya kazi kwa pamoja.

Aidha, Mhe. Rais amesema ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima, Uganda hadi Tanzania unakaribia kuanza lakini akauliza wakandarasi wa hapa nchini wamejipangaje katika kushiriki ujenzi huo. 

Kuhusu ulipaji wa madeni ya wakandarasi, Mhe Rais amesema, serikali yake imekuwa ikilipa madeni hayo na itaendelea kufanya hivyo hadi deni litakapoisha. Amesema kwa kuanza serikali imelipa bilioni 650 na baadaye ikatumia bilioni 462 kutoka Mfuko wa Barabara kuwalipa wakandarasi.

Amesema wakandarasi ni watu wa muhimu sana katika maendeleo ya Taifa na ni injini ya maendeleo kwani wako kila sekta ya maendelo. Amesema kwa mfano  wako katika ujenzi wa mioundombinu, kwenye zana za kilimo,kwenye  uvuvi, na pia usafirishaji wakandarasi hawakosekani.

No comments:

Post a Comment