Wednesday, May 25, 2016

MFANYAKAZI WA KITUO CHA MIKUTANO CHA JNICC AJISHINDIA KITITA CHA MILIONI 3



Mshindi wa tuzo ya ubunifu, ndugu Hussein Baitira (kushoto) akiwakatikapichayapamojanaMhasibu Mkuu ambaye pia anakaimu nafasi ya Mkurugenzi wa Fedha na Utawala ndugu Augustine Karadoga, Afisa Utawala na Rasilimali Watu ndugu Fanuel Festo pamoja na Katibu wa Chama cha Wafanyakazi (TUICO) tawi la AICC ndugu Rashid Habib Rashid mara baada ya kukabidhiwa hundi yenye thamani ya shilingi 3,800,000/-.
Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC kimemtunuku mfanyakazi wake Hussein Baitira tuzo ya ubunifu baada ya mfanyakazi huyo kugundua mbinu ya kurekebisha viyoyozi zaidi ya 10 vya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere ambavyo vilikuwa havifanyikazi.

Mkurugenzi Mwendeshaji wa AICC, ndugu Elishilia Kaaya amemkabidhi Hussein hundi yenye thamani ya shilingi 3,800,000/- ikiwa ni motisha kwa mfanyakazi huyo kutokana juhudi alizozionesha nakulipunguzia shirika gharama ambayo Shirika lingeingia kwa kukodisha mtaalamu kutoka nje ya nchi kuja kurekebisha viyoyozi hivyo.
Akiongea wakati wakukabidhi hundi hivyo, ndugu Kaaya alieleza kuwa tuzo hiyo imetolewa kwa mujibu wa utaratibu wa Shirika wa kumzawadia mfanyakazi ambaye ameonesha ubunifu wa hali ya juu katika kuliletea shirika maendeleo.                                                                                                                                                                                                                                                                                         
“Napenda kukupongeza kwa kuonesha ubunifu wa hali ya juu katika kazi yako na tuzo hii iwe kichocheo cha kuongeza ubunifu zaidi kwako wewe pamoja na wafanyakazi wengine wote wa AICC”, alisisitiza.

Mkurugenzi wa Miliki na Miradi, ndugu Victor Kamagenge amesema kwamba kama viyoyozi hivyo visingeendelea kushindwa kufanyakazi shirika lingelazimika kuingia gharama ya kununua viyoyozi vipya na kubadilisha mfumo wa umeme.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa hundi hiyo, Hussein alisema kuwa majuma kadhaa kugundua tatizo la viyoyozi hivyo na kupata ufumbuzi wake.
Alieleza kuwa viyoyozi vya JNICC ni aina ya mfumo wa teknolojia ya Hisense lakini mfumo huo haupo kwasasa na hivyo kulazimika kuingia katika mtandaokutafuta teknolojia nyingine kama Hitachi nakutumia kitabumtando cha maelekezo (internet manual) kugundua tatizo na kupata ufumbuzi wake.

No comments:

Post a Comment