Monday, April 4, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI



SIMU.tv: Klabu ya Yanga ya jijini Dar es saalam imewapa raha mashabiki wake baada ya kuitumbua Kagera Sugar kwa ushindi wa goli 3 kwa 1. https://youtu.be/5hF3K8O06GQ 

SIMU.tv: Klabu ya Leicester City imeendelea kujikita kileleni mwa ligi ya Uingereza baada kushinda goli 1 huku Manchester United wakiichapa Everton.https://youtu.be/QMG98YF5tbg

SIMU.tv:  Mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Manyara zimesababisha maafa baada ya kaya zaidi ya 50 kukosa makazi na uharibifu wa mazao.https://youtu.be/FH7c6zyxBVY

SIMU.tv: Halmashauri ya wilaya ya Ilala yaituhumu serikali kuwa na njama za kupunguza vyanzo vya mapato vya manispaa hiyo kwa kuvipeleka katika mamlaka zingine za ukusanyaji kodi. https://youtu.be/78qNULBCRPA

SIMU.tv: Rais John Magufuli awataka watanzania kuendeleza upendo na mshikamano huku akipiga vikali ubaguzi wa udini, makabila na rangi. https://youtu.be/FQbdn_V3DlA

SIMU.tv: Wakulima na wafugaji wilayani Mvomero mkoani Morogoro ambao mara kwa mara huingia katika migogoro wapinga hatua ya serikali ya kutenga maneo ya pande hizo mbili huku wakidai hawakushirikishwa. https://youtu.be/__yPpdkiBFs

SIMU.tv: Jeshi la polisi mkoani Mwanza imefanikiwa kuvunja mitandao miwili ya ujambazi kati ya 7 baada ya hapo awali kukithiri kwa vitendo vya uhalifu huo.https://youtu.be/nuCvwrXwNlA

SIMU.tv: Changamoto ya ukosefu zana za kisasa, masoko pamoja na mitaji kwa wakulima, wafugaji na wavuvi mkoani Kigoma imeelezwa kuwa sababu ya makundi hayo kuendelea kuwa masikini licha ya kuzalisha zaidi. https://youtu.be/ijF3nFxn0KM

SIMU.tv: Hatimae ubomoaji wa jingo la ghorofa 16 katika manispaa ya Ilala wafikia tamati baada ya kapuni inayobomoa jengo hilo kubakiza msingi.https://youtu.be/eZJGDPL5SBc

SIMU.tv: Shirika la viwango nchini TBS, limevifungia viwanda 4 vya kuhoka mikate mkoani morogoro kwa kushindwa tekeleza agizo la kurekebisha kasoro zilizobainika katika viwanda hivyo. https://youtu.be/eaDwglplgc8

Kamati ya kudumu ya bunge ya nishati na madini yalitaka shirika la umeme nchini TANESCO kumsimmisha kazi mkandarasi wa usambazaji wa umeme vijijini REA mkoani Njombe baada ya kutoridhishwa na utendaji wake. https://youtu.be/cyfAgzOjcLw

SIMU.tv: Askari zaidi ya 40 wa JWTZ waliokwenda nchini Kenya kushiriki mafunzo ya amani warejea nchini huku wakielezea manufaa waliopata kupitia mafunzo hayo.https://youtu.be/CjK9bPVE_fM

SIMU.tv: Serikali imejipanga kutokomeza mitandao 5 ya ujambazi inayojihusisha na uvamizi wa mabenki na mauaji mkoani Mwanza. https://youtu.be/G5NnSOYUiiI

SIMU.tv: Naibu waziri wa mambo ya ndani asema mkoa wa Kigoma unapaswa kupewa kipaumbele kwa kuongezewa vitendea kazi kama magari, rasilimali fedha, askari polisi na uhamiaji ili kuweza kukabiliana na uhalifu wa aina mbalimbali.https://youtu.be/DYpS56-U2qY

No comments:

Post a Comment