Monday, April 25, 2016

SAKATA LA MATIBABU YA WAGONJWA WA SICKLE CELL (SELIMUNDU), MUHIMBILI, SERIKALI WATOA MSIMAMO.


Bi.Yasmin Razak, akiwa amembeba mtoto anayeugua maradhi ya Selimundu (Sickle cell), wakati wa mkutano wa waandishi wa habari kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Mama huyu ambaye mwanaye pia anaugua ugonjwa huo, lakini matibabu yake anapatanchini Uingereza, ameamua kusimama kidete kutetea wagonjwa wa selimundu kuendelea kuhudumiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, na kumuomba Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kuingilia kati mpango wa kuwaondoa wagonjwa 6,000 hospitalini hapo na kuwapeleka kwenye hospitali wanakotoka.
NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said, MNH.
HOSPITALI ya Taifa Muhimbili, MNH, na Serikali kupitia Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee na Watoto, wametoa msimamo kuhusu sintofahamu iliyowakumba wagonjwa wa sickle cell (Selimundu), waliokuwa wakipatiwa matibabu kwenye hospitali hiyo kubwa kabisa hapa nchini.

Kauli ya MNH kuhusu tiba ya Selimundu
Tunapenda umma uelewe kuwa huduma hii haijasitishwa na wala Hospitali haitasitisha utoaji wa huduma hiyo.” Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali hiyo, Profesa Lawrence M. Museru, amewaambia waandishi wa habari leo Aprili 25, 2016.

Hofu ya wagonjwa
Awali baadhi ya wazazi wa watoto wenye kuugua maradhi ya Selimundu, wakiongozwa na Bi.Yasmin Razak, wameonyesha hofu ya maisha ya watoto wao kufuatia taarifa kuwa jumla ya wagonjwa 6,000 waliokuwa wakipatiwa matibabu ya Selimundu hospitalini hapo chini ya mradi wa utafiti wa ugonjwa huo, “Welcome Trust.” Watarudishwa kwenye utaratibu wa matibabu chini ya muongozo wa Wizara ya Afya kwenye hospitali walikotoka, kwa vile mradi huo wa utafiti umemaliza kazi yake Machi 31, 2016.

Gharama za matibabu ya Selimundu
Ni kweli kwamba takribani miaka kumi kulikuwa na mradi uliokuwa ukifadhili matibabu pamoja na utafiti wa wagonjwa wa selimundu,  Mradi huu kwa sababu ya utafiti ulihitaji wagonjwa wote wa selimundu kuja Muhimbili kwa ajili ya utafiti na tiba. Hivyo basi hali hii ilisababisha wagonjwa wengi wanaohitaji huduma ya selimundu kuja Hospitalini hapa licha ya kwamba mahitaji yao hayakuhitaji utalaamu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Amesema Profesa Mseru.

Naye Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Wizara ya Afya, Dkt.Doroth Gwajima, amewaondoa hofu wagonjwa kuhusu gharama za matibabu hayo ambapo alisema, muongozo wa serikali uko wazi, wazee na watoto watapatiwa matibabubure na wengine wanachangia kupitia bima ya afya na fedha taslim, hata hivyokwa wale ambao hawatakuwa na uwezo utaratibu wa kuwapatia matibabu upo.

Hofu ya wagonjwa
Kutokana na mazoea ya muda mrefu ya kupatiwa matibabu bure ya ugonjwa huo wa selimundu, na hasa ikizingatiwa hakuna tiba ya kuuponya kabisa ugonjwa huo, wagonjwa wamehoji watawezaje kumudu kulipia gharama hizo?

Wazazi wa watoto wanaougua ugonjwa huo, wametmuomba Rais John Magufuli, kuingilia kati suala hilo ili kuokoa maisha ya wagonjwa hao ambao kwa asili ya ugonjwa wenyewe, mgonjwa hupata maumivumakali mwilini, mabadilikoya viungo, na wakati mwingine kupungukiwa damu mara kwa mara.

Kauli ya Mganga Mkuu wa jiji la Dar es Salaam
“Hospitali zote za Manispaa ya jiji la Dar es Salaam, na hata zile zilizopo mikoani na wilayani, zina uwezo wa kutoa huduma za ugonjwa wa Selimundu, na hata ikionekana kuwa mgonjwa anahitaji matibabu zaidi, rufaa huandaliwa na mgonjwa hupelekwa kwenye hospitali kubwa zaidi ili kupatiwa matibabu yanayofaa.” Dkt.Grace Magembe, Mganga Mkuu wa jiji la Dar es Salaam.



 Bi.Getrude Thadeo kutoka Tabora, akiwa na mtoto wake wa miaka 13, Angela Romwadi, ambaye anaugua Selimundu
 Bi.Mkami Titus wa Temeke jijini Dar es Salaam akiwa na mtoto wake Shedrack Yahaya(4), anayeugua selimundu
 Bi.Walivyo Mohamed kutoka Rufiji mkoani Pwani, akiwa na mtoto wake wa miaka 4, Siraji Majid
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitaliya Taifa Muhimbili, (MNH), Profesa Lawrence Museru, (kulia), akiwa na Mkuu wa Idara ya Magonjwa na Afya ya Watoto ya MNH, Dkt. Mary B. Charles, akizungumza na waansdishi wa habari wakati akitoa taarifa yake mapema leo Aprili 25, 2016
 Profesa Museru
 Dkt.Doroth Gwajima, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia Wazee na Watoto.
 Profesa Museru natimu yake wakati akiongea na waandishi wa habari
 Dkt.Grace Magembe, Mganga Mkuu wa jiji la Dar es Salaam
 Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Damu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dkt. Elineema Meda. Dkt. Meda ni mmoja wa walioshiriki kwenye utafiti wa ugonjwa huo wa Selimundu chini ya mradi wa Welcome Trust
 Bi. Yasmin wakati wa mkutanona waandishi wa habari kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Baadhiya akina mama wakiwa na watoto wao wanaosumbuliwa na maradhi ya Selimundu. Hapa wakihudhuria mkutano na waandishi wa habari ulioitishwa na Bi. Yasmin ambaye ameamua kuwasimamia na kuwasemea wagonjwa wa Selimundu

Bi. Yasmin (katikati), akiwa na Bi.Walivyo Mohammed na mtoto wake Siraji (kushoto) na Bi. Getrude Thadeona mtoto wake Angela.

No comments:

Post a Comment