Saturday, April 2, 2016

Faida kuu 5 za kutumia .tz domain kwenye biashara

Tayari umeshamaliza kusajili kampuni Brela na sasa unajiandaa kukamilisha taratibu za kupata TIN kutoka TRA na hatimaye leseni ya biashara ili kuanza rasmi biashara yako. Umeshikwa na shauku kubwa kusubiria siku kuu ambayo utakata keki kuashiria ufunguaji rasmi wa biashara yako. Lakini, Dudumizi inapenda kukukumbusha kuna kitu umekisahau kwenye orodha ya shughuli za kufanya, nacho ni usajili wa .co.tz domain.
Kumbuka, si lazima uwe na Website ndiyo usajili Domain, usajili wa domain unatakiwa kufanyika mapema ili kulinda jina lako hata kama haujaanza kulitumia. Sajili domain hapa.

Historia ya majina ya Website:

Kabla ya mwaka 1984 ambayo University of Wisconsin technicians walitengeneza seva za majina ya website(Name Server), hakukuwa na majina ya Website, watu walitumia namba tu, mfano, kama unataka kutembelea Website ya Dudumizi, ulitakiwa kuandika https://198.207.55.196. Hebu fikiria tungekwa tunaiandikaje kwenye Business card?
Mwaka 1985, majina ya Website kwa kutumia .com, .net na .org yalianza kutumika na watu kuanza kuachana na namba. Kwa kulitambua hilo, kwa tanzania, mchakato ulianza mwaka 1995 na hatimaye, TCRA iliuna tzNIC kama msimamizi mkuu wa .tz domaiin, na hatimaye, mwaka 2009, tzNIC ilianza rasmi kumanage majina ya .tz domain kupitia kwa mawakala wake, Dudumizi ikiwa mmoja wao.
Ingawa wapo watu wenye shauku ya kumiliki domain ya .co.tz lakini, kuna maswali au utata unaozunguka kichwani, hivyo, makala hii itasaidia kutatua maswali yanayoweza kujitokeza kuhusu .tz domain.

1. Je nitahitaji .tz pamoja na .com

Jibu la swali hili ni NDIYO au HAPANA, .tz ndiyo mpango mzima. Haijalishi unafanya biashara Tanzania pekee au dunia nzima, .tz itakufikisha huko na inatosha kabisa. Kumbuka, haijalishi unatumia kikoa cha .tz au .com, zote zitapatikanika dunia nzima. Tofauti tu, kwa kutumia .tz mtu anaweza kujua moja kwa moja hii ipo Tanzania bila hata kwenda kwenye mawasiliano.
Kuna woga au dhana ambayo ipo kwa wengi wetu ya kuhofia matumizi ya .co.tz inayopelekea kuamini kama .com ndiyo inayojulikana na watu. Google imeboresha sana upatikanaji wa Website bila kuathiriwa na kikoa.

2. .tz inakuwezesha kurudisha domain iliyopotea

Ni mara ngapi imeshatokea umepoteza mawasiliano na mtu aliyekutengenezea Website au kukusajilia domain (kwa wale wanaotumia watu binafsi), au ni mara ngapi mumeshindwa kufikia maelewano na mtu aliyekukusajilia domain na kupelekea kutaka kuifungia domain hiyo?
Kwakuwa usimamizi wa .tz unafanyika Tanzania moja kwa moja, hivyo, endapo kutatokea tatizo lolote na mtu aliyekusajilia domain mukashindwa kuwa na mawasiliano, kama unatumia .tz domain, taasisi ya tzNIC itakuwezesha kurudisha domain hiyo punde tuu utakapowasilisha taarifu za uhakikiwa umiliki wake.

3. .tz inakuwakilisha Kitanzania Zaidi

Mtembeleaji wa wavuti anapoona kikoo cha .tz, basi moja kwa moja anajua kuna mahusiano na Tanzania. Hivyo, hii hupelekea kuwa na imani na utulivu kwakuwa wateja wengi hupenda kufanya kazi na kampuni zilizo karibu nao.
Kwa mfano, makampuni ya kitalii, hii ni moja ya nyenzo muhimu sana kwenye kujitangaza, kwani watalii wanapenda kufanya kazi na mtu aliye karibu na eneo husika, .tz ni kiashiria tosha.
Ndiyo maana, hata Google wameamua kutumia Google.co.tz ambayo inawalenga watu wa Tanzania.

4. Uwanja mpana wa kuchagua

Ni mara ngapi umeona website imeongezewa tz mbele ya jina, mfano dudumizitz.com au michongotz.comkwakuwa majina ya kwanza yameshachukuliwa na muhusika anapenda  tuu kutumia .com. Kwanini usingefikiria kutumia majina kama dudumizi.co.tz badala ya dudumizitz.com?
 Kwa, kutumia .tz, unao uwanja mpana wa machaguzi kwakuwa majina mengi sana bado hayajachukuliwa.

5. Uzalendo

Ndiyo, kwa kutumia vikoa vya .tz, tunasaidia kutangaza nchi yetu, watu wanapoona domain za .tz inawasaidia kuikumbuka Tanzania na kufika mbali zaidi.

Unayo kila sababu ya kusajili .tz domain, kumbuka pia kusajili domain kutoka kwa makampuni yenye uhakika ili kuepuka kupoteza uhalali wa umiliki wake. Gharama za kusajili domain za .tz ni 25000 tu. Hivyo, sajili Domain yako Hapa.

No comments:

Post a Comment