Na Woinde Shizza, Mwanga
Wanachama
wa chama Mpinduzi wilaya ya Mwanga mkoa kiliimanjaro Wameeleza kuwa
pamoja na kupita kimbunga cha siasa za maji taka zilizosheheni ushabiki ,
ubabaishaji na hujuma,Wana CCM wilayani humo wamebaki wamoja bila
kuyumbishwa na wanasiasa wasaka madaraka kwa njia za hila na fedha .
Wamesema
kuwa wale wote ambao walifuata siasa za ushabiki kwa kushabikia mambo
bila kupima uzani wa siasa na ubora wa kila chama, sasa hivi wako
katika dimbwi la majuto na fedheha kwani wameshaona hasara za kuhama
chama hicho.
Katibu
wa CCM wilaya ya Mwanga Mkoa kilimanjaro Mwanaidi Hussein Mbisha
aliyasema hayo wakati akitoa neno la shukran mara baada ya Kaimu katibu
Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka kuzungumza na viongozi wa vijiji na kata
pamoja na wanachama wa chama hicho wilayani Mwanga mkoani hapa.
Mbisha
alisema umadhubuti wa CCM usichukuliwe kama janbo jepesi na rahisi
badala yake viongozi wa upinzani na wanachama wanaoshabikia vyama hivyo
wakubali ukweli kuwa CCM iko imara .
Alisema
CCM iliioachwa na marehemu baba wa Taifa Mwalimu julius Nyerere , Mzee
Abeid Karume,Mzee Rashid Kawawa na mzee Thabit Kombo itabaki kuwa
kimbilio na tarajio la wananchi katika kufanikisha masuala yao kisiasa,
kijamii na kiuchumi.
"Shaka
nimekuwa nikikusikiasikia tu na kukusoma katika vyombo vya habari,wewe
bado kijana mdogo, ila unatosha kubeba hata dhamana kubwa, endelea Mungu
atakusaidia uthibitishwe kuwa Katibu mkuu "alisema mbisha.
Awali
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa kilimanjaro Juma Raibu Juma aliisifu wilaya
ya mwanga kwa kuendelea kuwatoa mchanga wa macho kwa kuilinda jimbo
hilo lisichukuliwe na upinzani.Raibu alisema heshima ya wana mwanga kwa
ccm itaendelea kuenziwa na kukumbukwa kila wakati kwa sababu ni watu
jasiri wenye msimamo thabiti.
"Unapokuwa
vitani halafu wapiganaji wako wakakataa katakata kupokea hongo toka kwa
maadui, wakasema hatutaki na hatufaiki chochote , hao ni
wazalendo"alisema Juma
Hata
hivyo Mwenywkiti huyo wa UVCCM mkoa wa Kilimanjaro alimpongeza Kaimu
katibu mkuu shaka kwa uthubutu wake wa kupania kurudisha heshima na
hadhi ya UVCCM iliyokuwa inapotea.Shaka anaendelea na ziara yake katika
wilaya ya Same ambako atahitimisha katika mkoa kilimanjaro kabla ya
kuanza mkoani Tanga kwa siku sita baadae Mikao ya Manyara,Kilimanjaro na
Arusha itafanya majumuisho ya pamoja mkoani mkoani hapa.
Kaimu katibu mkuu wa UVCCM taifa Shaka Hamdu Shaka akiwa anapanda mti nje ya ofisi ya CCM wilaya ya Mwanga
kaimu katibu mkuu UVCCM taifa akiwa anaongea na wananchi wa kata ya Kileo iliopo ndani ya Wilaya ya Mwanga
kaimu
katibu mkuu UVCCM taifa Shaka Hamdu Shaka akiwa anamkabidhi kiongozi wa
timu ya Kileo jezi ambazo UVCCM mkoa wa Kilimanjaro waliaidi timu
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa kilimanjaro Juma Raib Juma akiwa anapanda mti wa ukumbusho nje ya ofisi ya CCM wilaya ya mwanga
Shaka akiongea na wanachama wa CCM wilaya ya Mwanga hii leo
No comments:
Post a Comment