Thursday, March 24, 2016

Shule Direct yazindua MAKINI SMS kwa ajili ya wanafunzi wa Sekondari

Mkurugenzi na Muasisi wa Shule Direct, Faraja Kotta Nyalandu akitoa hotuba wakati wa hafla ya uzinduzi wa mfumo mpya wa kujifunza kupitia simu za mkononi mahususi kwa wanafunzi wa Sekondari ufahamikao kama MAKINI SMS. Kupitia mfumo huo, wanafunzi wa Sekondari wanaweza kujipima kupitia maswali; kupata masomo yaliyofupishwa kwa matumizi ya meseji (SMS); kumuuliza mwalimu mtaalamu wa masomo mbalimbali ‘Ticha Kidevu’; kutumia Wikipedia na kutumia ‘search’ kutafuta na kupata mada wanayohitaji moja kwa moja. Hafla hiyo ilifanyika hivi karibuni, Jijini Dar es salaam.
Sasa ni uzinduzi wa MAKINI SMS.
Mkurugenzi wa Mawasiliano, Iku Lazaro na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Shule Direct. Fatma Said, wakifurahia jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa mfumo mpya wa kujifunza kupitia simu za mkononi mahususi kwa wanafunzi wa Sekondari ufahamikao kama MAKINI SMS, uliofanyika hivi karibuni Jijini Dar es salaam.

Mabalozi wa Shule Direct wakimuelekeza mgeni aliyehudhuria uzinduzi huo.
Nyuso za furaha kwa upatikanaji wa elimu bora, popote, muda wowote
Timu ya Shule Direct.
Wageni mbalimbali wakielekezwa jinsi ya kutumia MAKINI SMS na Balozi wa Shule Direct kutoka Azania.

No comments:

Post a Comment