Friday, March 4, 2016

ONESHO LA ARDHI NA MAENDELEO YA JAMII LAFUNGULIWA RASMI MAKUMBUSHO YA TAIFA

Mgeni Rasmi kwa niaba ya Balozi wa Sweden Bw Jorgen Erickson na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Prof Audax Mabula wakikata utepe kuashiria kufunguliwa rasmi kwa onesho la Ardhi na Maendeleo ya Jamii, kwenye Ukumbi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Prof Audax Mabula akitoa ufafanuzi juu ya onesho la Ardhi na Maendeleo ya Jamii na kuipongeza Serikali kupitia Wizara ya Ardhi na Makazi kwa kusimamia vyema matumizi ya ardhi, kwenye Ukumbi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.
mtafiti mzamivu katika taaluma ya mazingira na matumizi bora ya ardhi kutoka Sweden Bi. Emma Li Johansson akitoa maelezo mafupi juu ya utafiti alioufanya Kilombero Mkoani Morogoro juu ya Matumizi ya Ardhi ambapo matokeo yake ndio onesho lililofunguliwa leo Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni.
Mratibu wa onesho bi Adelaide Salema akitoa maelezo kwa Mgeni rasmi Bw Jorgen Erickson na wageni mbali mbali juu ya picha zilizopo kwenye onesho la Ardhi na Maendeleo ya Jamii, kwenye Ukumbi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.

wageni mbali mbali wakitazama picha zilizopo kwenye onesho la Ardhi na Maendeleo ya Jamii, kwenye Ukumbi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.
Mgeni Rasmi kwa niaba ya Balozi wa Sweden Bw Jorgen Erickson akiongea na wageni mbali mbali waliofika kushuhudia uzinduzi wa onesho la Ardhi na Maendeleo ya Jamii, kwenye Ukumbi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment