Friday, March 25, 2016

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO ASHUHUDIA KUORODHESHWA KWA HISA STAHILI ZA MAENDELEO BANK PLC, KATIKA SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM (DSE)

Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Dkt. Ashatu Kijaji, Mwenyekiti wa Maendeleo Benki, Amulike Ngeliama (kushoto) na Mkurugenzi wa Tafiti, Sera na Mipango wa(CMSA) Nicodemus Mukama wakifuatilia jambo katika hafla hiyo.
Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Dkt. Ashatu Kijaji akipiga kengele kuashiria uorodheshwaji rasmi wa Maendeleo Benki katika soko la hisa DSE jana. Kushoto ni Mwenyekiti wa Maendeleo Benki, Amulike Ngeliama na Mkurugenzi wa Capital Markets na Securities Authoriy (CMSA) Nicodemus Mukama 
Emmanuel Nyalali, Mkuu wa Kitengo cha Uendeshaji DSE akizungumza katika hafla hiyo. 
Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Dkt. Ashatu Kijaji akiongea wakati wa hafla ya kuorodheshwa kwa Maendeleo Benki katika soko la hisa DSE 
Mkurugenzi mtendaji wa Maendeleo Benki, Ibrahim Mwangalaba akitoa hotuba yake kabla ya kumkaribisah Mwenyekiti wa Benki hiyo kuzungumza na washiriki wa hafla hiyo. 

Bank PLC ni benki iliyoanzishwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Mashariki na Pwani na inamilikiwa na Wananchi mbalimbali kwa njia ya HISA bila kujali, kabila, itikadi, dini wala rangi, kwani benki hii imesajiliwa na soko la hisa la Dar es Salaam (DSE), kupitia dirisha dogo yaani Enterprise Growth Market (EGM) na inaendeshwa kwa kufuata taratibu zote za BOT na Soko la Hisa la Dar es S alaam. 

Maendeleo Bank ilianza kutoa huduma za kibenki tarehe 9/9/2013 baada ya kupewa leseni na Benki Kuu ya Tanzania na tarehe 05/11/2013 ilisajiliwa rasmi katika soko la hisa la Dar es Salaam baada ya kukidhi vigezo vyote vilivyowekwa na mamlaka husika. Benki hii ilianza na mtaji wa shilingi bilioni 4.5 kutoka kwa wanahisa zaidi ya 3,000 wa rika na itikadi mbalimbali walionunua wakati wa mauzo ya awali (IPO) yaliyofanyika mwaka 2013.

Tarehe 9/11/2015 benki ilipata kibali cha kuuza hisa stahili ambapo matarajio yake yalikuwa kupata shilingi bilioni 3.06 ambazo zitatumika kuimarisha shughuli za uendeshaji wa benki pamoja na kuongeza matawi. Katika zoezi la uuzaji wa hisa stahili benki imeweza kupata jumla ya shilingi bilioni 2.8 na kufikisha jumla ya mtaji wa benki kuwa shilingi bilioni 7.3.

Kusudi kubwa la kuanzishwa kwa Maendeleo Bank PLC ni kufikisha huduma za kibenki kwa wananchi wa kipato cha chini na cha kati kwani hao ndio walio wengi na upatikanaji wa huduma za kibenki kwao ni changamoto kubwa. 

Benki hii imepata mafanikio mengi tangia kuanzishwa kwake takribani miaka miwili iliyopita ambapo mpaka tarehe 31/12/2015, benki imefikisha wateja zaidi ya 12,000, amana zaidi ya shilingi bilioni 46.0, mali za benki zimefikia zaidi ya shilingi bilioni 55, imetoa mikopo zaidi ya shilini bilioni 21.0 na mwaka 2015 imepata faida ya takribani shilingi milioni 200.0 baada ya kodi. 

Benki hii inatoa huduma mbalimbali za ubunifu ambazo zinawalenga wananchi wa kada mbalimbali, zikiwemo: huduma za kibenki kwa njia ya simu, huduma za BIMA, ATM kupitia mtandao wa UMOJA Switch, akaunti mbalimbali zenye gharama rafiki, kutuma na kupokea pesa kutoka nje na ndani ya nchi, na kutoa mikopo ya aina mbalimbali, ikiwemo kwa wajasiliamali wadogo ambayo haina dhamana, yaani mikopo ya vikundi. 

No comments:

Post a Comment