Thursday, March 31, 2016

MWENYEKITI WA MTAA WA OYSTERBAY, LUBUVA ASAIDIA WATUNZA MAUA WA MBUYUNI JIJINI DAR.





WANAKIKUNDI cha Green Garden ambao wanafanya biashara uuzaji na utunzaji  maua  pembeni kidogo ya kituo cha mabasi cha Mbuyuni jijini Dar es Salaam wapewa mpira kumwagilia maua wa Mita 100 na Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa Oysterbay(CCM), Zefrin Lubuva.

Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa Oysterbay(CCM), Zefrin Lubuva amesema kuwa ameona vyema kutimiza ahadi alizoahidi wakati wa kampeni za uchaguzi wa viongozi wa serikali za mtaa kwa wanakikundi hicho kwani aliwaahidi kuwasaidi amesema Mwenyekiti huyo wakati wa kukabidhi mpira wa kumwagilia wa mita 100 leo pembeni ya kituo cha mabasi ya Mbuyuni jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa wa kikundi cha Green Garden, Mohamed Mombo ameashukuru  Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa Oysterbay(CCM), Zefrin Lubuva kwa kutimiza ahadi ahadi yake.

"Tulikua na mpira ambao ulikuwa umetoboka tulijitahidi kuziba na makaratasi ili usivuje sasa tumepata mpya tena wa mita 100 sasa tutakuwa kukijitahidi kutunzaji wa maua vizuri"

Mombo amesema kuwa kikundi hicho kimeanzishwa mwanzoni mwa mwaka 1985 mpaka sasa wapo tuu kwa sababu ya kujitafutia liziki ikiwa wanapata changamoto mbali mbali hasa za kukosa wateja kwa mda mwingine.
 Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa Oysterbay(CCM), Zefrin Lubuva akimwagilia maua mara baada ya kuwakabidhi mpira wa Mita 100 kwa wanakikundi cha Green Garden jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa kikundi cha Green Garden, Mohamed Mombo akizungumza kwa mwandishi wetu mara baada ya kupewa msaada wa mpira wenye mita 100 utakao wawezesha kumwagilia maua kwa urahisi zaidi tofauti na mwanzo na 

 Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa Oysterbay(CCM), (kushoto) Zefrin Lubuva  akikabidhi Mpira wa Mita 100 kwa wanakikundi cha Green Garden kilichopo Mbuyuni jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa Oysterbay(CCM) (Mwenye kitambulisho), Zefrin Lubuva akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi mpira wa mita 100 jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa Oysterbay(CCM) (mwenye kitambulisho), Zefrin Lubuva akipewa maelekezo na Mwenyekiti wa kikundi cha Green Garden, Mohamed Mombo mara baada ya kukabidhi mpira wa kumwagilia maua katika kikundi hicho kilichopo Mbuyuni jijini Dar es Salaam.
Wanakikundi wakiufungua mpira kwaajili ya kuanza kazi  mara baada ya kukabidhiwa mpira wa mita 100 leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

No comments:

Post a Comment