Thursday, March 24, 2016

Bunge la Tanzania kuanzisha Ushirikiano wa kirafiki na Bunge la Israeli

Na Zuhura Mtatifikolo, Bunge

Katibu wa Bunge Tanzania Dkt Thomas Kashililah leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Bunge la Israeli (KNESSET) Ronen Plot aliyemtembelea Ofisini kwake jijini Dar es Salaam akitokea Nchini Zambia alikokuwa akishiliki Mkutano wa 134 wa umoja wa Mabunge Duniani (IPU) uliofanyika tarehe 19 hadi 23 Machi, 2016.

Akizungumzo wakati wa kikao na Dkt. Kashililah, Mkurugenzi huyo wa Bunge la Israel, amesema ziara yake hapa nchini kutembelea Bunge la Tanzania ina lengo la kuwasilisha Mkataba wa Makubaliano wenye lengo la kuanzisha cha Urafiki wa Kibunge baina ya Bunge la Tanzania na Bunge la Israel.

Plot ambaye alimbatana na mkewe Shosh Plot, amesema Bunge la Israel linautaratibu wa kuwa na mahusiano na mabunge mengine duniani kwa lengo la kubadilishana uzoefu katika masuala ya uendeshaji Mabunge ambapo hadi kufikia sasa tayari Bunge hilo lina ushirikiano wa karibu kupitia utaratibuy huu na mabunge zaidi ya  30 Duniani kote na kwa  upande wa Afrika ni nchi Tano walizotiliana saiani na kuanzisha ushirikiano wa namna hiyo.

Akielezea, nia hiyo ya Bunge la Israel, Katibu wa Bunge la Tanzania Dkt Thomas Kashililah amesema amefurahishwa sana na ujio wa Mkurugenzi wa Bunge hilo kutembelea Bunge la Tanzania na tayari wamezingatia kwenye mipango uanzishwaji wa Chama cha Ushirikiano wa Mabunge haya mawili kikihusisha Wabunge kutoka pande zote mbili kubadilishana mawazo hususani katika namna bora ya uendeshaji na usimamizi wa shughuli za kibunge.

Katika kufanikisha hilo, Dkt. Kashililah amesema ujumbe huo utakutana na Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai siku ya Jumamosi ili kufanya mazungumzo nae na kisha kuangalia namna utekelezaji wa wazo hilo utakavyokuwa kabla ya kutiliana saiani makubaliano hayo.

Tayari Bunge la Tanzania  lina makubaliano ya ushirikiano na  vyama vya kirafiki kutoka Mabunge mengine ya Nchi mbalimbali duniani ambazo ni Uturuki, China, Korea Kusini, Morroco, Misri, Uholanzi na Poland
Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Thomas Kashililah (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Bunge la Israel wakati alipomtembelea leo ofisini kwake Jijini Dar es Salaam na kufanya mazungumzo naye.
Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Thomas Kashililah (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Bunge la Israel, Rone Plotwakati alipomtembelea leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam na kufanya mazungumzo naye.
Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Thomas Kashililah (kulia) akiongea na Mkurugenzi Mkuu wa Bunge la Israel, Rone Plot wakati wa chakula cha mchana katika hoteli ya Kilimanjaro iliyopo jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Thomas Kashililah (kulia) akimkabidhi zawadi ya trei ya kubebea vinywaji mke wa Mkurugenzi Mkuu wa Bunge la Israel, Bi. Shosh Plot wakati wa chakula cha mchana katika hoteli ya Kilimanjaro iliyopo jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Thomas Kashililah (kulia) akipokea zawadi toka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Bunge la Israel, Ronen Plot wakati wa chakula cha mchana katika hoteli ya Kilimanjaro iliyopo jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Thomas Kashililah (wa pili kulia)akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Bunge la Israel, Ronen Plot (wa pili kushoto) wakati wa chakula cha mchana katika hoteli ya Kilimanjaro iliyopo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Katibu wa Bunge John Joel

No comments:

Post a Comment