Thursday, February 25, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI

SIMU.TV: Watu 3 wa kabila la wasonjo wauawa kwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa wamasai kwa kile kilichodaiwa kuwa mgogoro wa ardhi. https://youtu.be/-PEJpTZpzO0  
  
SIMU.TV: Rais John Magufuli apokea ugeni maalum kutoka kwa Rais wa Guinea na kumhakikishia kuwa nchi hiyo itaendelea kushirikiana na Tanzania katika Nyanja mbalimbali ikiwemo uchumi.https://youtu.be/klWuXSc2aVU   

SIMU.TV: Waziri wa ardhi William Lukuvi afanya ziara wilayani Mvomero mkoani Morogoro ikiwa ni juhudi za kutekeleza agizo la raisi la kumaliza migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji.https://youtu.be/hI9NP_TqYys  
  
SIMU.TV: Jiji la Dar es salaam laelezwa kukabiliwa na tatizo kubwa la maeneo ya maziko ya binadamu baada ya maeneo mengi yaliyotengwa kwa ajili ya kazi hiyo ya maziko kujaa na kupelekea wakazi wa jiji hilo kurudia maeneo amabayo yalikwisha tumika.https://youtu.be/wjQFPAz_Se4  
  
SIMU.TV: Serikali ya Tanzania na Zambia zaanza juhudi za kufufua mazungumzo yenye lengo la kuanzisha tume ya pamoja ya ushirikiano baina ya nchi hizo huku ikiwa ni miaka 9 tangu maungumzo ya mwisho kufanyika miaka 9 iliyopita nchini Zambia.https://youtu.be/Fj4J_qrqkbM  
  
SIMU.TV: Serikali yawataka watumishi wa umma kutokuwa na hofu kutokana hatua ya zinazochukuliwa na serikali kuwasimamisha kazi wale wote wanaobainika kutumia vibaya madaraka au ubadhilifu.https://youtu.be/hbAKjR3SEBc  
  
SIMU.TV: Mtoto mwenye umri wa miaka 3 aishiye mkoani Morogoro anaomba msaada wa matibabu na kiti maalum kutokana ulemavu alionao. https://youtu.be/cLGZAILjmfs  
  
SIMU.TV: Utafiti uliofanywa na shirika la Twaweza waonesha asilimia 88 ya watanzania wanaimani kubwa na serikali ya awamu ya tano; https://youtu.be/ZKyJFPFwJFo  
  
SIMU.TV: Rais wa nchini Guinea, Jose Mario Vaz amhakikishia Rais John Magufuli ushirikiano mzuri katika sekta ya uchumi;https://youtu.be/q7I-08sEoXk
   
SIMU.TV: Serikali yasema haitasita kuwachukulia hatua kali wafanyabiashara  wa madini watakaobainika kukwepa kodi;https://youtu.be/tywD1qAe9tE
  
SIMU.TV: Halmashauri ya wilaya ya Kiteto yafuta posho ya vikao na matumzi yasiyo ya lazima ili kuelekeza fedha hizo katika shughuli za kimaendeleo; https://youtu.be/H1uvp3LebaM

SIMU.TV: Serikali yasema itawachukulia hatua kali za kinidhamu maafisa ushirika wazembe wanaosababisha kufirisika kwa vyama vya ushirika nchini;  https://youtu.be/HX_AFQTC3EI
  
SIMU.TV: Serikali yawataka wafanyabishara wa Mbuzi waliopo katika eneo la machinjio la Vigunguti  kuondoka mara moja;https://youtu.be/PRr5VkMAxYQ
   
SIMU.TV: Jeshi la Polisi mkoani Mara lafanikiwa kuwakamata watu saba wanaodaiwa kuhusika katika mauaji ya mtoto Mariam Deogratius; https://youtu.be/5hyZIieE3Cs

 SIMU.TV: Umoja wa wazalishaji vinywaji baridi nchini waipatia serikali msaada wa vifaa tiba kwa ajili ya kuboresha sekta ya afya nchini; https://youtu.be/raYNKXK7mQQ
  
SIMU.TV: Serikali yaitaka benki ya Amana kuwashirikisha wafanyabiashara wadogo wa eneo la Mbagala kwa kuwapatia mikopo kwa ajili ya kuboresha biashara zao;https://youtu.be/MU6q1FLenvM

 SIMU.TV: Serikali kwa kushirikiana na bodi ya filamu nchini itaaunda sera ya filamu kwa lengo la kukomesha wizi wa kazi za wasanii;https://youtu.be/nzl2Yi7628w
  
SIMU.TV: Mabingwa watetezi wa michuano ya kikapu ya NBA Golden state warriors yaibuka na ushindi wa jumla ya pointi 118 kwa 112 dhidi ya Miami Heat; https://youtu.be/ePa8eetescU 

SIMU.TV: Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yauomba uongozi wa nchi wananchama wa umoja wa falme za kiarabu kuiunga mkono Zanzibar katika harakati za kupata usajili wa kudumu wa kituo cha usajili wa vyombo vya usafiri wa  baharini;https://youtu.be/pM1dLJmewu4

No comments:

Post a Comment