Monday, February 22, 2016

MHE. RAIS JOHN POMBE MAGUFULI APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO


Mhe. Balozi Jean Pierre Tshampanga Mutamba wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili Ikulu kwa ajili ya kuwasilisha Hati za Utambulisho. 
Mhe. Balozi Mteule wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hapa nchini, Mhe. Balozi Jean Pierre Tshampanga Mutamba akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu tarehe 22 February, 2016. 
Rais Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa DRC mara baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho. 
Mhe. Balozi Mteule wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hapa nchini, Mhe. Jean Pierre Tshampanga Mutamba (katikati) akisikiliza nyimbo za Taifa mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam katika hafla fupi ya kukabidhi Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli iliyofanyika tarehe 22 February, 2016. 
Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Mhe. Balozi Mteule wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) hapa nchini wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Naibu Waziri Dkt. Susan Kolimba (watatu kulia) Mhe. Katibu Mkuu Balozi Aziz Mlima (wa pili kulia) na Balozi Samuel Shelukindo, Mkurugenzi wa Idara ya Afrika, kushoto ni maofisa kutoka Ubalozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hapa nchini. 

Wakati huo huo Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli alipokea pia Hati za Utambulisho za Mhe. Balozi Mteule wa Namibia hapa nchini. 
Mhe. Balozi Mteule wa Namibia hapa nchini, Mhe. Theresia Samaria akisaini Kitabu cha wageni Ikulu mara baada ya kuwasili kwa ajili ya kuwasilisha Hati za Utambulisho. 
Mhe. Balozi Mteule wa Namibia hapa nchini, Mhe. Theresia Samaria akikabidhi Hati za Utambulisho kwa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu tarehe 22 February, 2016. 
Mhe. Balozi Mteule akisalimiana na Mhe. Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dkt. Suzan Kolimba. 
Mhe. Balozi akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikana na Kimataifa, Mhe. Balozi Azizi Mlima. 
Rais Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Namibia mara baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho. 
Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Mhe. Balozi Mteule wa Namibia wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa na maafisa wa Ubalozi wa Namibia hapa Nchini. 

No comments:

Post a Comment