Tuesday, January 5, 2016

WATANZANIA MSIKUBALI KUTOZWA RUSHWA KWA AJILI YA DAMU, TOA TAARIFA KWA NESI, DAKTARI ATAKAYETOZA DAMU!- DK. KIGWANGALA

IMG_0681
Afisa Uendeshaji wa Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini Dar es Salaam, Bw. Abdu Juma akitoa maelezo ya namna wanavyoendesha shughuli zao kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kigwangalla aliyefanya ziara ya kushtukiza katika ofisi hizo, Januari 4, 2016. (Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
IMG_0770
Afisa Uendeshaji wa Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini Dar es Salaam, Bw. Abdu Juma akimwonyesha Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kingwangalla moja ya damu ambayo ni maalum kwa wamama wajawazito wakati wa kujifungua zilizohifadhiwa kwenye jokofu katika mabara hiyo.
IMG_0760
Mmoja wa watumishi katika maabara ya ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama (ambaye jina lake halipatikana) akiendelea kutekeleza majukumu yake kama alivyokutwa na mpiga picha wetu.

Na Modewjiblog, Team.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla ameagiza watanzania wote wasikubali kutozwa rushwa kwa ajili ya damu salama na baadala yake kwa mtu atakayefanya hivyo watamchukulia hatua kali.

Kauli hiyo imetolewa mapema Januari 4 (jana) na Naibu huyo wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Kingwangalla alipofanya ziara katika Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini Dares Salaam.

Dk. Kigwangalla amefafanua kuwa, kwa watu wote ikiwemo Nesi, Daktari ama mtaalamu wa afya, atakayemtoza mtu damu, atachukuliwa hatua kali ikiwemo kufukuzwa kazi.“Kwa watanzania wote, msikubali kutoa rushwa kwa ajili ya damu. Na kama itatokea Nesi ama Daktari ama nani, anakuambia ulipie ili upate damu!. Kwa sababu kuna uhaba wa damu kwa sasa.. Ripoti kwa Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa Mkoa ama Daktari Mkuu husika ama fika Wizara ya afya moja kwa moja na kuna namba tutaitoa kwa watanzania wote mtupatie ripoti.

Mtu atakayekutoza damu, wewe tuambie, huyo tutamfukuza kazi moja kwa moja, hatuwezi kuendekeza watu wa namna hii... Serikali inaingia gharama kubwa kukusanya damu kwa watu, Kuna watu wanajitolea damu zao bure. Leo wewe nesi ama mganga ukauze damu, hilo jambo hatutakubali hata kidogo kwa hiyo natoa rai kwa watanzaia hiyo damu ni bure na haiuzwi na usikubali kuuziwa damu hata kidogo.” Ameeleza hilo Dk. Kigwangalla.

Awali katika ziara hiyo, Dk. Kigwangalla ameipongeza Ofisi ya Mpango wa Taifa wa Damu Salama kwa kazi wanayofanya na ubunifu waliofikia wa kuhusisha Halmshauri katika ukusanyaji wa damu huku wao wakisimamia kudhibiti viwango vya damu ya matumizi kwa watanzania huku akitumia wasaha huo kutoa maelekezo ya kuboresha mfumo wa motisha kwa wanaochangia damu salama ambapo kwa wachangiaji damu kuingizwa kwenye mfumo wa kieletroniki wa kuwatambua watu wanaochangia damu, kutoa taarifa jinsi damu zao zilivyookoa miasha ya wagonjwa na kuwapa motisha ili waweze kuwa wachangiaji endelevu.

“Motisha sio soda na maji kwa wanaochangia damu. Motisha ni hata kupewa taarifa kwamba damu yake imesaidia kuokoa maisha ya mwanadamu mwenzake aliyekuwa anaumwa ugonjwa fulani, hii ni motisha kubwa sana kuliko hata pesa, ama soda ama maji yanayotolewa anapochangia damu.

Lakini kama imeshajitokeza mtu kuwa na tabia ya kuchangia damu, huyu sio wa kumpoteza, maana yake kuna uwezekano mkubwa wa akarudi tena kuchangia damu, mtu huyu ni lazima kuwe na mfumo wa kielekrioniki wa komputa wa kumtakia salamu, taarifa na anakuwa kwenye database yenu.

“Mnatakiwa muwe na mfumo wa kumpa taarifa pindi damu yake imetumika, ikiwemo kumueleza kuwa damu yako imemsaidia Mama mjamzito aliyejifungua na kutokwa damu nyingi, na mtu huyo akipata taarifa hiyo ni motisha tosha hivyo ni lazima muwe na huo mfumo kutoa motisha zaidi.
IMG_0689
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla na msafara wake wakishuka ngazi kuelekea kukagua idara mbalimbali katika ofisi hizo, Januari 4, 2016.

Awali akielezwa na Meneja wa kanda ya Mashariki katika Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini Dar es Salaam, Eveline Mgassa kwamba changamoto zilizopo katika upatikanaji wa damu nchini ni halimshauri kutenga bajeti za kutosha kwa ajili ya huduma hiyo, Kwa hatua hiyo, Dk. Kigwangalla ameziagiza Halmshauri zote nchini kuhakikisha zinatenga bajeti za kutosha ilikusapoti mpango wa damu salama.
Katika hilo Dk. Kigwangalla ameapa kuwashughulikia wale wote watakaozembea na kuwachukulia hatua kali Ma DMO, Wakurugenzi na kushtakiwa kwa mamlaka zilizopo na kufukuzwa kazi.

“Naziagiza Halmashauri zote kuhakikisha zinatenga bajeti za kusapoti mpango wa ukusanyaji damu salama. Na Halmashauri zitakazoshindwa, DMO na Mkurugenzi wake tutahakikisha tunawashtaki kwa mamlaka zilizowateua ili uteuzi wao ukome mara moja. Maana hatuwezi kuacha akinamama wajawazito wapoteze damu wakati wa kujifungua, watu wanaopata ajali wapoteze maisha kwa sababu ya watu hawataki kutimiza wajibu wao.

Hilo haliwezi kukubalika, Mfumo wa hali ya damu kwa Tanzania kwa sasa unatisha. Kwa sasa nchi inakiwango cha chini mno, tokea wafadhili wajiondoe katika hili. Ni lazima tuwe makini sana maana leo mzima kesho umepata ajali, umepasuka mfupa wa kwenye paja damu nyingi zimemwagika unahitaji damu!!

Kwa upande wa watu wote wanaopata damu salama nchini, huduma hiyo wanazipata bure kwani damu hizo ni za Serikali, Hata hivyo mifuko na vitu vinavyotumika kuhifadhia damu hiyo vina gharama kubwa.

“Damu inatolewa bure na serikali. Mtambue kuwa, vifaa vya kutunzia damu hii ni gharama kubwa. Hivyo mifuko mashirika ya Bima, na mashirika mengine kuanzia leo kutazama namna ya kulipa gharama za vifaa vya utunziaji damu hizo. Damu ni bure, lakini mfuko ule wa kutunzia ile damu ni gharama kubwa sana na hata vifaa vya kupimia damu ile nayo ni gharama kubwa hivyo walipie kwa kila damu watakayochukua.” Alieleza Dk. Kigwangalla.
IMG_0703
Meneja wa kanda ya Mashariki Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini Dar es Salaam, Eveline Mgassa (mwenye miwani) akielezea utaratibu wa ukusanyaji wa damu unavyofanyika kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla aliyefanya ziara ya kushtukiza katika ofisi hizo, Januari 4, 2016 jijini Dar.
IMG_0690
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla (aliyeipa mgongo kamera) akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Uendeshaji wa Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini Dar es Salaam, Bw. Abdu Juma ya namna wanavyopokea watu wanaofikia kuchangia damu kwa hiari na kuhifadhiwa kwenye benki hiyo yaTaifa ya Damu Salama, alipofanya ziara ya kushtukiza, Januari 4, 2016 katika ofisi hizo.
IMG_0725
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kingwangalla akitoa mkono wa pongezi kwa wananchi walioonyesha uzalendo kwa kufika katika ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Januari 4, 2016 na kuchangia damu kwa hiari yao ambapo mmoja kati yao alisema hii ni mara yake ya nne na ni utararibu aliojiwekea.
IMG_0729
IMG_0743
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kingwangalla akisalimiana na kumpongeza mmoja wa wananchi (jina lake halikuweza kupatikana) aliyefika kuchangia damu kwa hiari, Januari 4, 2016 katika makao makuu ya ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama.
IMG_0764
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kingwangalla akiwa ndani ya maabara ya Mpango wa Taifa wa Damu Salama alipofanya ziara ya kushtukiza kwenye ofisi hizo, Januari 4, 2015 jijini Dar es Salaam.
IMG_0774
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kingwangalla akisaini vitabu vya wageni nje ya ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini Dar es Salaam, Januari 4, 2016 wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika ofisi hizo.
IMG_0826
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kingwangalla akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufanya ziara ya kushtukiza na kuzungikia vitengo mbalimbali katika ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment