Friday, January 1, 2016

MATUKIO MAKUBWA YA MUZIKI WA DANSI NCHINI KWA MWAKA 2015

BENDI MPYA
•Tarehe 31-Jan-2015, BMM Classic Band, ilizinduliwa katika ukumbi wa BMM Mwenge, opposite TRA.
•Tarehe 21-Feb-2015,  JJ Band yazinduliwa katika ukumbi wa. JJ Band ni bendi dada ya Skylight Band itakayokuwa inatumbuiza mjini Mwanza katika hotel ya Jembe ni Jembe Resort.
 •Tarehe 06-Mar-2015 (Ijumaa), Ruby Band ilitambulishwa rasmi katika ukumbi wa Coco Beach Pub ambapo pia ilizindua video ya wimbo mpya wa “Noma”.
•Tarehe 18-Jul-2015 (Jumamosi), Stars Band yazinduliwa katika ukumbi wa Mzalendo Pub. Bendi hiyo inaongozwa na mwanamuziki Aneth Kushaba aka “AK47” aliyekuwa Skylight Band. Meneja wa bendi ni mpiga drums James Kibosho. Bendi hii inaundwa pia na mpiga solo Alain Kisomundele na Mao Santiago aliyekuwa Machozi Band.
•Dec-2015, bendi mpya itakayojumuisha Mule Mule FBI, Totoo Ze Bingwa, Alain Mulumba Kashama, Montana Amarula na Didi “Number” Kayembe (Numero) aka “Dume la Mende” ipo katika maandalizi ya kuundwa na kuzinduliwa huku Mule Mule FBI akiwa rais (prezidaa) wa bendi hiyo huku Losso Mukenga, mpiga solo wa Ally Kiba, akiipigia pia bendi hiyo.

UZINDUZI WA ALBUM MPYA
•Tarehe 27-Dec-2015, Milimani Park Orchestra “Sikinde-Ngoma ya Ukae”, ndani ya TCC Chang’ombe, yazindua album ya “Jinamizi la Talaka” sambamba na kufanya sherehe za miaka 37 tokea bendi ianzishwe mwaka 1978

KILI MUSIC AWARD
•Tarehe 23-Mar-2015, Kililimanjaro Music Award 2015 yazinduliwa rasmi
•Tarehe 25-Apr-2015, Academy ya Kili Music Award yakutana kuchagua majina ya washiriki wa kila kipengele.
•Tarehe 29-Apr-2015, majina ya washiriki wa kila kipengele yatangazwa rasmi
•Tarehe 13-Jun-2015 (Jumamosi), sherehe za washindi wa Kili Music Award 2015 zilifanyika katika ukumbi wa Mlimani City. Kulikuwa na jumla ya vipengele (categories) 6  vya muziki wa dansi. Washindi walikuwa kama ifuatavyo;
1. Bendi Bora ya Mwaka- FM Academia
2. Mtunzi Bora wa Mwaka Bendi-Jose Mara (Mapacha Watatu)
3. Rapa Bora wa Mwaka Bendi- Fergusson (Mashujaa Band)
4. Wimbo wa Kiswahili Bendi- ”Wale Wale” (Vijana Ngwasuma)
5. Mwimbaji Bora wa Kiume Bendi- Jose Mara (Mapacha Watatu)
6. Mtayarishaji Bora wa Nyimbo Bendi-Amoroso Sound

NB: Mwaka huu hakukuwa na Mwimbaji Bora wa Kike Bendi

WANAMUZIKI WALIOFARIKI
•Tarehe 04-Jan-2015 (Jumapili), mwanamuziki  Flowin aka “Kachumbari” aliyekuwa mpiga drums na tumba wa Chuchu Sound afariki dunia.
•Tarehe 30-Jan-2015, mwanamuziki Peter Kanuti afariki dunia kwa ajali ya gari akiwa Zanzibar. Huyu anatokea familia ya wanamuziki Gaspar Kanuti, Fred Kanuti na Joseph Kanuti.
•Tarehe 28-Feb-2015, mwanamuziki, mwanasiasa, mwanajeshi mstaafu, mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi, Mkurugenzi wa kundi la sanaa za maonesho la Tanzania One Theatre (TOT Plus) Captain John Damian Komba afariki dunia.
•Tarehe 16-Apr-2015, mwanamuziki Joseph Chigwele “Che” Mundugwao afarikia dunia.
•Mwanamuziki Mutombo Lufungula “Audax”, mmoja ya waanzilishi na wamiliki wa bendi ya Maquis du Zaire (ambayo baadaye ikaitwa Maquis Original) afariki dunia alfajiri ya Alhamis tarehe 23-Apr-2015 na kuzikwa Jumapili ya tarehe 26-Apr-2015 katika makaburi ya Kinondoni.
•Tarehe 17-Jul-2015 (Ijumaa), mwanamuziki Ramadhan Ally Masanja aka “Banza Stone” afariki dunia siku ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhan. Azikwa Jumamosi tarehe 18-Jul-2015 sikukuu ya Idd Mosi (Eid al Fitr) katika makaburi ya Sinza.
•Tarehe 01-Nov-2015, Mkurugenzi wa bendi ya FM Academia, Martin Jotham Kasyanju, afariki dunia akiwa hospitali ya Aga Khan. Alizikwa Ijumaa ya tarehe 06-Nov-2015 katika makaburi ya Kinondoni.
•Tarehe 09-Nov-2015, mwanamuziki mkongwe Captain  John Simon afariki dunia katika hospitali ya Muhimbili. Alizikwa tarehe 11-Oct-2015 katika makaburi ya Tabata Kimanga.
•Tarehe 19-Nov-2015, aliyepata kuwa mtangazaji maarufu wa radio na TV Prince Baina Kamukulu hususan wa vipindi vya muziki wa dansi (kama Radio Free Africa na Star TV) afariki dunia. Aliwahi pia kuwa mtangazaji wa Kipindi cha “Afrika Bambataa” cha Clouds FM.
•Tarehe 20-Nov-2015, aliyepata kuwa rapa wa bendi ya Mashujaa “Kama Simba” afariki dunia.
•Tarehe 28-Nov-2015, muasisi wa Safari Trippers aliyekuwa mtunzi, mwimbaji, mpuliza sax na mpiga solo David Bernard Gordon aka “David Musa” afariki dunia. Azikwa tarehe02-Dec-2015 katika makaburi ya Kinondoni.
•Tarehe 02-Dec-2015, mwanamuziki Kasongo Mpinda “Clayton” afariki dunia. Azikwa tarehe 03-Dec-2015 katika makaburi ya Kisutu.

WANAMUZIKI WAKUBWA WALIOHAMA BENDI
•Feb-2015, mwanamuziki Badi Bakule “Mkandarasi” aondolewa katika bendi ya Twanga Pepeta.
•Tarehe 08-Apr-2015, Ally Choki na Super Nyamwela watangazwa rasmi kujiunga (kurejea) Twanga baada ya kuivunja rasmi bendi ya Extra Bongo. Hii ilitanguliwa na kitendo cha Ally Choki kusalimia kisanii kwenye jukwaa la Twanga Leaders Club 17-Jan-2015, tukio ambalo halijawahi kufanyika kwa miaka 8. Pia tarehe 30-Jan-2015, Ali Choki na Mama Asha Baraka walipatanishwa rasmi chini ya usuluhishi uliofanywa na Global Publisher. Tarehe 25-Apr-2015 (Jumamosi), ndio ilifanyika show ya kwanza ya Ally Choki na Super Nyamwela baada ya kurejea Twanga Pepeta yafanyika Mango Garden.
•May-2015, Wanamuziki Bob Kissa na Grayson Semsekwa wajiunga na Double M Sound wakitokea Extra Bongo iliyovunjika baada ya kundoka kwa Ally Choki.
•Tarehe 08-May-2015 (Ijumaa), Mashujaa Band imetambulisha wanamuziki wawili wapya Roggart Hegga Katapila na Dady Dipirone “Rais wa Masauti ya Chini”. Hiyo ilifanyika wakati Mashujaa Group wakizindua ukumbi wao wa Mashujaa Lounge ambao zamani ulikuwa unaitwa Business Park uliopo maeneo ya Victoria, Dar-es-Salaam.
•Jul-2015, mwanamuziki Janeth Kushaba aka AK47 ajiengua katika bendi ya Skylight Band na kuanzisha bendi mpya ya Stars Band.
•Tarehe 29-Jul-2015, mwanamuziki Elyston Angai awasili nchini na kujiunga na Mashujaa Band japo baadaye akarudi Afrika Kusini ambako inasemekana amekwenda kujiandaa ili aweze kurudi Tanzania moja kwa moja.
•Jul-2015, Wanamuziki Polepole Bahogwerhe “Papy Catalogue”, Chims Kamanyola na Ben Bievang wahama bendi ya Vijana Ngwasuma. Chims Kamanyola na Ben Bievang warejea FM Academia.
•Aug-2015, mwanamuziki Roggart Hegga Caterpillar ajiunga na Twanga Pepeta akitokea Mashujaa Band.
•Nov-2015, wanamuziki Salehe Kupaza, Dogo Rama na Jojo Jumanne kutoka Twanga Pepeta wahamia bendi ya  Double M Sound iliyo chini ya uongozi wa Prince Mwinjuma Muumin ambayo hivi sasa imebadilishwa jina na kuitwa Double M Plus.
•Nov-2015, mwanamuziki Jaddo Field Force ahama Mashujaa Band na kuhamia bendi ya Dar Musica.
•Nov-2015, mwanamuziki Eddo Sanga aihama Dar Musica na kurudi bendi ya Msondo Ngoma ambayo alipata kuwepo hapo awali. Kabla ya hapo, mwanzoni mwa mwaka alikuwa Victoria Sound kabla ya kuhamia Mlimani Park Orchestra “Sikinde” ambapo baadaye alielekea Dar Musica.
•Nov-2015, mwanamuziki Karama Regesu ahama bendi ya Dar Musica na kurejea bendi ya Mlimani Park Orchestra. Mwanamuziki mwingine aliyerejea Mlimani Park ni mpiga solo Adolph Mbinga.
•Dec-2015, mwanamuziki Mulemule FBI ahama bendi ya FM Academia. Aenda kuanzisha bendi mpya inayoundwa pia na Totoo Ze Bingwa, Alain Mulumba Kashama, Montana Amarula na Didi “Number” Kayembe (Numero) aka “Dume la Mende”.
•Dec-2015, mwimbaji Dispatch arejea Mashujaa Band.
•Dec-2015, mwimbaji Tarsis Marsela yupo katika sintofahamu ya kuendelea kubaki au kuondoka Akudo Impact baada ya likizo yake ya muda mrefu huku uongozi wake wa bendi akipewa Zagreb Butamu.

MATUKIO MENGINE MAKUBWA
•Tarehe 24-Jan-2015 (Jumamosi), tamasha linaloitwa TIGO KIBOKO YAO Concert lafanyika Leaders Club. Bendi za muziki wa dansi zilizoshiriki ni Msondo Ngoma, Mlimani Park Orchestra, Christian Bella & Malaika Music Band, Yamoto Band. Kila bendi ilipiga kwa dakika 45.
•Tarehe 25-Jan-2015 (Jumapili), tamasha la miaka 10 ya CDS lafanyika TCC Chang’ombe na kushirikisha bendi za muziki wa dansi za Msondo Ngoma, Mapacha Watatu, Malaika Music Band na FM Academia.
•Tarehe 07-Feb-2015 (Jumamosi), tukio la “Miaka 16 ya Luizer Mbutu” ndani ya Twanga Pepeta lafanyika Mango Garden.
•Tarehe 28-Mar-2015 (Jumamosi), wafanyika mpambano kati ya FM Academia na Twanga Pepeta katika ukumbi wa Escape One.
•Tarehe 18-Apr-2015 (Jumamosi), Christian Bella afanya tukio la “Usiku wa Masauti” ndani ya ukumbi wa Escape One. Christian Bella atumia tukio hilo kutambulisha/kuzindua audio na video ya wimbo wake mpya wa “Nashindwa”.
•Tarehe 25-Apr-2015 (Jumamosi), kundi la Les Wanyika kutoka Kenya latumbuiza katika kiwanja cha Escape One.
•Tarehe 26-Apr-2015, Bendi ya Cuban Marimba watunukiwa nishani ya Muungano kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete katika sherehe zilizofanyika katika viwanja vya ikulu. Waliopokea nishani kwa niaba ya bendi ni Waziri Nyange (mpiga solo) na Mzee Juma Sangura (mpiga bass).
•Tarehe 08-May-2015 (Ijumaa), Mashujaa Group wazindua ukumbi wao wa Mashujaa Lounge ambao zamani ulikuwa unaitwa Business Park uliopo maeneo ya Victoria, Dar-es-Salaam. Katika tukio hilo, Mashujaa Band imetumia nafasi hiyo pia kutambulisha wanamuziki wawili wapya Roggart Hegga Katapila na Dady Dipirone “Rais wa Masauti ya Chini”. Pia Mashujaa Band walitambulisha nyimbo 2 mpya. Ikumbukwe pia kuwa Mashujaa Group mwaka huu wamefanikiwa kuanzisha radio ya Mashujaa FM mkoani Lindi.
•Tarehe 18-Jul-2015 (Jumamosi), mpambano wa Msondo na Sikinde wafanyika siku ya Idd Mosi (Eid al Fitr) katika ukumbi wa TCC Chang’ombe kwa kuandaliwa na Fred Ogot na kampuni yake ya Bob Entertainment.
•Bendi ya African Stars Band-Twanga Pepeta yafanya tukio lililopewa jina la “Usiku wa Juzi, Jana na Leo” katika siku na sehemu 3 tofauti za Escape One (31-Jul-2015), Dar West Tabata (01-Aug-2015) na TCC Chang’ombe (02-Aug-2015)
•Tarehe 08-Aug-2015, bendi ya African Stars Band-Twanga Pepeta ndani ya ukumbi wa Mango Garden wafanya tukio lililoitwa “Usiku wa Dream Team” ambapo walizindua vyombo vipya, walishiriki wanamuziki kadhaa wa zamani wa bendi hiyo, walifanya show moja na bendi ya Mapacha Watatu na walipiga baadhi ya nyimbo zao bora kabisa tokea bendi kuanzishwa.
•Tarehe 06-Aug-2015, Rais JM Kikwete ahudhuria hafla maalum ya kumuaga iliyoandaliwa na Muungano wa Wasanii Tanzania iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City.
•Tarehe 21-Aug-2015, bendi ya FM Academia wafanya sherehe ya birthday ya 18 katika ukumbi wa Arcade, Mikocheni.
•Tarehe 28-Nov-2015, bendi za Twanga Pepeta na Mapacha Watatu zafanya onyesho moja katika ukumbi wa Mango Garden katika tukio la “Usiku wa Kuachwa” ambapo wanamuziki Chaz Baba, Khalid Chokora, Kalala Juniour na Jose Mara walipanda jukwaa moja .
•Tarehe 27-Dec-2015, Mlimani Park Orchestra “Sikinde-Ngoma ya Ukae” wafanya tukio la kuadhimisha miaka 37 tokea bendi ianzishwe mwaka 1978. Siku hiyo pia walizindua album ya “Jinamizi la Talaka”. Siku moja kabla, yaani Boxing Day 26-Dec-2015, walitembelea hospitali ya wagonjwa wa saratani ya Ocean Road kuwajulia hali na kuwapa msaada wagonjwa.

No comments:

Post a Comment