Wednesday, December 23, 2015

Watendaji wa Tanesco Wazidi Kubanwa Watakiwa Kukamilisha Miradi Kabla Ya Februari Mwakani

Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medadi Kalemani (wa kwanza kulia) akitoa maagizo ya kukamilika kwa mradi huo ifikapo february mwakani kwa Mkurugenzi Mwandamizi wa Miradi TANESCO Bw.Gregory Chegere (wa kwanza kushoto) alipofanya ziara yake leo katika mradi wa Tanzania Energy Development Access Program (TEDAP) eneo la Mbagala Rangi Tatu,jijini Dar es Salaam,Mradi huo utasaidia kusambaza umeme wenye nguvu ya kutosha na unaotarajia kunufaisha zaidi ya wananchi elfu kumi wa eneo hilo,watatu kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Paul Masanja.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medadi Kalemani (kushoto) akitoa maagizo kwa Mkandarasi wa Kampuni ya SAE Power Lines Bw.Tahir Mehmood (wa kulia) anayejenga mradi wa TEDAP eneo la Kurasini jijini Dar es salaam kuhakikisha mpaka mwanzoni mwa mwakani awe amshafunga Transifoma katika eneo hilo la mradi ni baada ya kutoridhishwa na kasi ya utekelezaji wake katika mradi huo.
Mhandisi Mkuu wa Miradi TANESCO Bw. Frank Mashalo (wa kwanza kulia) akimweleza Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medadi Kalemani (wa pili kushoto)kuhusu maendeleo ya mradi TEDAP uliyopo maeneo ya Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam na (wa kwanza kushoto) ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Paul Masanja.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medadi Kalemani (kushoto) akisikiliza malalamiko ya mmoja wa wateja wa huduma za TANESCO Bw.Michael Sedyan, Mkazi wa Sinza,hii ni baada ya Naibu waziri kufanya ziara ya kushtukiza katika ofisi za Tanesco Magomeni leo jijini Dar es Salaam.
Afisa Muendesha Mitambo kituo cha TANESCO Kipawa Bibi Zuhura Mmanyi (wa kwanza kulia)akimweleza Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medadi Kalemani (wa kwanza kushoto) namna mitambo ya eneo hilo inavyofanya kazi na maeneo mitambo hiyo inayosambaza umeme ikiwemo eneo la Gongo la mboto,Kiwalani,Segerea,Chang’ombe na Buguruni leo jijiji Dar es Salaam Naibu waziri alipo fanya ziara yake katika ofisi hiyo (wapili kushoto ni Mkurugenzi Mwandamizi wa Miradi TANESCO Bw.Gregory Chegere na wapili kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Paul Masanja.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medadi Kalemani (wa kwanza kushoto) akitoa maagizo kwa Mkandarasi wa Kampuni ya SAE Power Lines Bw.Stephen Joseph (wa kwanza kulia) anayejenga Mradi wa TEDAP eneo la Gongo la Mboto kuhakikisha umeme unaanza kuwaka katika mitambo hiyo ifikapo mwishoni mwa mwezi Desemba 2015 kwa kuwa kila kitu kimeshakamilika katika mradi huo na malipo yake tayari ameshamaliziwa kulipwa, (wapili kushoto) ni Mkurugenzi Mwandamizi wa Miradi TANESCO Bw.Gregory Chegere.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medadi Kalemani (kulia) akimsikiliza mmoja wa wateja wa Ofisi ya TANESCO Magomeni Bw.Mohamed Bago Mkazi wa Manzese alipokuwa akitoa kero yake kuhusu kusubiri zaidi ya masaa matatu kupatiwa huduma ya tatizo ya luku yake ambayo haiingizi umeme,hiyo ni baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika ofisi za Tanesco Magomeni.

No comments:

Post a Comment