Wednesday, December 2, 2015

MSD YATAKAIWA KUTOA DAWA ZINAZOHITAJIKA

Vikundi mbalimbali vya wajasiriamali wa Vicoba, Saccos na wasindikaji
ngozi waMji mdogo wa Mirerani Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara,
wakiwa kwenye kongamanola uhamasishaji wa mpango wa bima ya afya kwa wajasiriamali na vikundivilivyosajiliwa (Kikoa) 
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Nchini (NHIF) Mkoani Manyara, Isaya Shekifu akizungumza jana katika kongamano la uhamasishaji wa mpango wa bima ya afya wa kikoa kwa wajasiriamali na vikundi vilivyosajiliwa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro (kulia) ni Mkuu wa wilaya hiyo Mahamoud Kambona na kushoto ni mratibu wa NHIF na mfuko wa afya ya jamii (CHF) mkoani humo Reginald Kileo.
Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Mahmoud Kambonaakizungumza wakati akifungua kongamano la uhamasishaji wa mpango wa bima yaafya wa kikoa kwa wajasiriamali na vikundi vilivyosajiliwa Mji mdogo wa Mirerani, (kushoto) ni Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Nchini (NHIF) wa mkoahuo, Isaya Shekifu na kulia ni Ofisa Tarafa ya Moipo Joseph Mtataiko 
 Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Nchini (NHIF) wa Mkoawa
Manyara, Isaya Shekifu akiandika maswali yaliyokuwa yanaulizwa katika
kongamano la uhamasishaji wampango wa bima ya afya wa kikoa kwa
wajasiriamali na vikundi vilivyosajiliwa Mjimdogo wa Mirerani Wilayani
Simanjiro. 

Na Woinde Shizza 
MKUU wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Mahmoud Kambona amewaasa viongozi wa mfuko wa Taifa wa bima ya afya nchini (NHIF) kuishinikiza bohari ya dawa nchini (MSD) kutoa dawa zinazohitajika.



Kambona aliyasema hayo jana mji mdogo wa Mirerani kwenye uzinduzi wa
kongamano la uhamasishaji wa mpango wa bima ya afya kwa wajasiriamali na 
vikundi vilivyosajiliwa (Kikoa).

Kambona alisema amepata malalamiko kwenye vituo vya afya Mirernai na
Orkesumet kuwa wamekuwa wanaomba dawa MSD na kuzilipia lakini wanapatiwa 
dawa ambazo hawana mahitaji nayo hivyo kupata hasara.

“Haina maana watu waagize dawa za malaria wao wawape dawa za kuvimba miguu 
zisozohitajika, ila NHIF mpo karibu na watu wa MSD, zungumzeni nao ili 
watoe dawa zinazoombwa na siyo kwa matakwa yao,” alisema Kambona. 

Pia, alivitaka vikundi vya ushirika wa Saccos, Vicoba, Amcos, Vibindo,
wachimba madini, waendesha bodaboda, mama na baba lishe na wasindika ngozi, 
wajiunge na bima ya afya ya Kikoa ili wapatiwe matibabu kwa unafuu. 


*Meneja wa mfuko wa Taifa wa bima ya afya nchini (NHIF) mkoani Manyara
Isaya Shekifu alisema mpango huo wa kikoa utamwezesha mwanachama wa
kikundi kupata matibabu yote kama watumishi wa serikali wanavyopata kwenye 
zaidi ya vituo 6,000 nchini nzima kwa mchango mtu mmoja sh76,800 kwa mwaka.

*Shekifu alisema gharama za matibabu nchini zinapanda kila uchao na huwa
vigumu kwa mwananchi wa kawaida kuweza kuzimudu pindi anapougua, bali 
kupitia kikoa wajasiriamali nchini watanufaika kupitia matibabu
watakayoyapatiwa.

*“Ugonjwa haupigi hodi bali humpata mtu wakati wowote na gharama za
matibabu zipo juu, ila kupitia kikoa wajasiriamali watapata matibabu bila
tatizo lolote, hivyo wanapaswa kujiunga kwa wingi kwenye bima hii,”
alisema.

*Mratibu wa NHIF na mfuko wa afya ya jamii (CHF) mkoani Manyara, Reginald 
Kileo alitaja mafao hayo yatahusisha* *gharama za kujiandikisha kumuona 
daktari, dawa zote zilizoidhinishwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, 
vipimo vidogo na vikubwa kama MRI na CT Scan, kulazwa na miwani ya kusomea.

“Mafao mengine ni upasuaji mdogo na mkubwa na upasuaji wa kujifungua kwa 
wanawake, matibabu ya kinywa na meno, matibabu ya macho, mazoezi ya 
kimatibabu ya viungo (physiotherapy) na vifaa saidizi kama magongo na
vishikizi vya shingo,” alisema Kileo. 

No comments:

Post a Comment