Tuesday, December 1, 2015

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA DISEMBA 1,2015

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YANCHI JESHI LA POLISI TANZANIA.
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 01.12.2015.

- WATU WATATU WAUAWA KATIKA MATUKIO MATATU TOFAUTI WILAYA ZA CHUNYA, RUNGWE NA MBARALI.

- WATU WAWILI WAFARIKI DUNIA KATIKA TUKIO LA AJALI JIJINI MBEYA. 

- WATU WANNE WAKAMATWA NA SILAHA MBILI NA NYARA ZA SERIKALI WILAYANI CHUNYA.

- MTU MMOJA AKAMATWA NA NYARA ZA SERIKALI MENO YA TEMBO WILAYA YA MOMBA.

KATIKA LA TUKIO LA KWANZA.
MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA IGUNDU AITWAE SIANA MWANDOLA [48], ALIUAWA KWA KUPIGWA NA KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KISHA MWILI WAKE KUCHOMWA MOTO.

TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 29.11.2015 MAJIRA YA SAA 23:00 USIKU HUKO KIJIJI CHA IGUNDU,KATA YA CHOKAA, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA.

INADAIWA KUWA CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI KULIPIZA KISASI KUTOKANA NA TUHUMA ZA MAREHEMU KUHUSIKA KATIKA MAUAJI YA MWANAMKE MMOJA AITWAE ROZA KYUSA [63] TAREHE 22.11.2015 MAJIRA YA SAA 02:00 USIKU. UPELELEZI UNAENDELEA ILI KUWABAINI NA KUWAKAMATA WAHUSIKA WA TUKIO HILI


KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI, BADALA YAKE WAHAKIKISHE WANAWAFIKISHA KATIKA MAMLAKA HUSIKA WATU WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI ILI SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.

KATIKA TUKIO LA PILI:
MZEE MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA ILOLO, AITWAE BENARD BUJA [79], ALIKUTWA AMEUAWA NYUMBANI KWAKE NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA KWA KUKATWA PANGA SHINGONI NA KISHA MWILI WAKE KUTUPWA KWENYE SHAMBA MALI YA THOMAS MWAMAKASI.

TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 30.11.2015 MAJIRA YA SAA 09:00HRS KIJIJI CHA ILOLO,KATA YA KIWIRA,TARAFA YA UKUKWE WILAYANI RUNGWE.

INADAIWA KUWA CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI IMANI ZA KISHIRIKINA, KWANI MAREHEMU ALIKUWA ANATUHUMIWA KUWA NI MCHAWI KIJIJINI HAPO. 

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHNA NA TABIA YA KUAMINI NA KUSADIKI IMANI POTOFU ZA KISHIRIKINA KWANI ZINASABABISHA MADHARA MAKUBWA KWA JAMII IKIWA NI PAMOJA NA UPOTEVU WA NGUVU KAZI. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MTU/WATU WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.

KATIKA TUKIO LA TATU:
MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA IHENZANA AITWAE NIKO CHAULA [30], ALIUAWA KWA KUPIGWA NA KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KISHA MWILI WAKE KUCHOMWA MOTO.

TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 30.11.2015 MAJIRA YA SAA 17:00HRS KIJIJI CHA MKUNYWA, KATA YA MADIBIRA,TARAFA YA RUJEWA, WILAYANI MBARALI.

INADAIWA KUWA CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI KULIPIZA KISASI KUTOKANA NA TUHUMA ZA MAREHEMU KUHUSIKA KATIKA TUKIO LA KUPORA PIKIPIKI T.852 DAT AINA YA YAMAHA MALI YA AIDAN WAYA [19], MKAZI WA ISOKO NA KUMJERUHI KWA KUMCHOMA KISU TAREHE 29.11.2015 SAA 19:45HRS . UPELELEZI UNAENDELEA ILI KUWABAINI NA KUWAKAMATA WAHUSIKA WA TUKIO HILI

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI, BADALA YAKE WAHAKIKISHE WANAWAFIKISHA KATIKA MAMLAKA HUSIKA WATU WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI ILI SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.

KATIKA TUKIO LA NNE.
WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA SAMWEL SANGA [24], MKAZI WA UYOLE NA AMANI SANGA [31], MKAZI WA UYOLE WALIFARIKI DUNIA BAADA YA GARI WALILOKUWA WAKISAFIRIA LENYE NAMBA ZA USAJILI T.717 CFM AINA YA M/CANTER ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA SAMWEL SANGA KUACHA NJIA, KUPINDUKA NA KUSABABISHA VIFO VYAO.

TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 30.11.2015 MAJIRA YA SAA 06:30HRS ENEO LA UYOLE,KATA YA IGAWILO, TARAFA YA IYUNGA JIJINI MBEYA.

CHANZO CHA AJALI HIYO NI MWENDO KASI. MILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. 

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO, IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA /KUFUATA SHERIA/ALAMA NA MICHORO YA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.

KATIKA TUKIO LA TANO.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA MKAZI WA BANANA – DSM AITWAE LUKAS WAMBURA [38] MWENYE SHAHADA YA DHARURA YA KUSAFIRIA AB-10044029 KWA KOSA LA KUKUTWA NA VIPANDE VINNE VYA MENO YADHANIWAYO KUWA YA TEMBO VYENYE UZITO WA KILO 8.4 YENYE THAMANI YA DOLA ZA KIMAREKANI 30,000, SAWA NA TSHS 64,140,000/=.

TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 30.11.2015 MAJIRA YA SAA 06:00HRS ENEO LA CUSTOM – MPAKANI TUNDUMA, KATA NA TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA.

INADAIWA MTUHUMIWA ALIKUWA ANAVUKA MPAKA AKITOKEA NCHI JIRANI YA ZAMBIA KUINGIA NCHINI NA MZIGO HUO ALIKUWA AMEUFICHA NDANI YA BEGI LAKE LA NGUO.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO JAMII KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA PINDI WANAPOMTILIA SHAKA MTU/WATU ILI HATUA ZA HARAKA ZICHUKULIWE.

KATIKA TUKIO LA SITA.
JESHI LA POLISI LINAWASHIKILIA WATU WANNE KWA KUKUTWA NA SILAHA MBILI PAMOJA NA NYARA ZA SERIKALI AMBAO NI 1. MOHAMED HUSSEINNDILAVA [55], MKAZI WA MKWAJUNI 2. NASSORA OMARY [65], MKAZI WA TABORA 3. MWANZA MTOKAMBALI [39] MKAZI WA NJELENJE NA FRANK JONAS [32], MKAZI WA BITIMANYANGA.

TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 30.11.2015 SAA 21:00HRS KATIKA KIJIJI NA KATA YA KAPALALA,TARAFA YA KWIMBA, WILAYA YA CHUNYA.

INADAIWA WATUHUMIWA WALIKUTWA NA SILAHA MOJA AINA YA RIFFLE 416 YENYE NAMBARI C.6539833 NA GOBOLE MOJA LISILOKUWA NA NAMBA, PIA WALIKUTWA NA NYARA ZA SERIKALI KICHWA KIMOJA CHA PAA, NYAMA YA PAA NA NYAMA YA SUNGURA VYOTE VIKIWA NA THAMANI YA TSHS 1,176,000/=.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA WAHALIFU WAKIWEMO MAJANGILI KUZITOA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI HATUA ZA KISHERIA DHIDI YAO ZICHUKULIWE MARA MOJA.

[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

No comments:

Post a Comment