Thursday, December 24, 2015

SIMU TV:HABARI KUTOKA TELEVISHENI

Watu wenye ulemavu nchini walalamikia kunyanyapaliwa na vyombo vinavyotoa huduma ya usafiri na kuiomba serikali kuingilia kati.https://youtu.be/Rgby5r6WnSg
Imeelezwa kuwa huenda uzalishaji wa mahindi katika halmashauri ya Tunduma mkoani mbeya ukashuka kwa asilimia 85 baada ya wakulima kukosa ruzuku za pemebejeo za kilimo ikiwemo mbegu na mbolea.https://youtu.be/vhU_dPLBIOc

Wakristo nchini waungana na wenzao duniani kote katika kufanya maandalizi ya kusheherekea Sikukuu ya Krismas. https://youtu.be/KZhqLSJPXPk

Katika kuelekea sherehe za Krismasi na Mwaka mpya Jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani kwa kushirikiana na Vodacom waendelea na kampeni za kueleimisha jamii hususani madereva kutii sheria za barabarani ili kuepusha ajali. https://youtu.be/33KGyOwmZcY

Viongozi wa dini mkoani Tanga wahimizwa kushirikiana na serikali  katika kuwajengea vijana maadili mema yatakayo waepusha na vitendo viovu ikiwemo matumizi ya dawa za kulevya. https://youtu.be/Gh5EWcEw9tg
Mgogoro wa kisiasa nchini Burundi waendelea kuchukua sura mpya kimataifa huku serikali ya nchi hiyo ikitoa tuhuma kwa pande mbalimbali ikiwemo nchi jirani. https://youtu.be/uI6z7H319P4  

Serikali yaahidi kuendeleza kwa kasi mradi wa umeme vijijini REA na kupatikana kwa umeme wa uhakika ili kukidhi mahitaji ya viwanda, na pia kuahidi kushusha bei ya nishati hiyo. https://youtu.be/Gm2WRBAiWvU
Jeshi la polisi nchini latoa tahadhari kwa madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani hususani kipindi hiki cha siku kuu za mwisho wa mwaka.https://youtu.be/EVPB0yn6SO0
Wizara ya Afya yapiga marufuku matangazo yote yanayohusu tiba asili na tiba mbadala kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii mpaka pale maelekezo yatakapo tolewa. https://youtu.be/6dPREsL_8us

Serikali yasema ni kinyume cha sheria kwa raia wa kigeni kuingia nchini na kuomba ajira kwa vibali vya ukazi na badala yake wanapaswa kufuata sheria ya ajira. https://youtu.be/da-hLHgAwvM

Baaada ya Rais John Magufuli kumalizia uteuzi wa baraza lake la mawaziri, wachambuzi mbalimbali waendelea kutoa maoni mbalimbali kufuatia uteuzi huo. https://youtu.be/hQ0N6R9hgAg

Waziri mkuu awataka viongozi wa dini kuwasimamia waumini wao kudumisha umoja na mshikamano ili kudumisha amani nchini;https://youtu.be/XQNHuvzYVUY

Waislamu mkoani Dodoma wametakiwa kuitumia siku ya kuzaliwa kwa mtume Muhammad S.A.W kujitafakari juu ya mienendo ya maisha yao ya kila siku;https://youtu.be/BrDocSOTSF4

Waislamu nchini wametakiwa kuzingatia maagizo ya mtume Muhammad S.A.W Kwa kufanya yale aliyoyaagiza na kuacha yale aliyoyakataza;https://youtu.be/UQBWPyZKLsw

Waumini wa dini ya kiislamu mkoani Ruvuma wamesheherekea siku ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad S.A.W katika hali ya amani na utulivu;https://youtu.be/L7LSGxLZjk0
Mabondia Francis Cheka na Thomas Mashali kila mmoja ametamba kumshinda mwenzake katika pambano litakalochezwa hapo kesho mkoani Morogoro;https://youtu.be/Ozz6mMIlzkQ

Jeshi la polisi mkoani Arusha linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kuhusika na  mauaji ya afisa wa TANAPA; https://youtu.be/pRSB6jU-rRI

Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mhe. Baraka Konisaga amewaogonza wananchi, askari polisi na maafisa wa jeshi la polisi kuaga mwili wa askari polisi PC Petro Matiko, aliyeua kwa kupigwa risasi na askari mwenzake;https://youtu.be/EoY-aNM1SWE

Kaya 12 hazina mahali pakuishi baada ya mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali kuboa nyumba zao katika kijiji cha Ikuti wilayani Rungwe mkoani Mbeya;https://youtu.be/cPXr48zbXNQ

Fahamu kuhusu dini ya kiisalmu na namna baadhi ya watu wanavyoihusisha na ugaidi hapa duniani; https://youtu.be/tLoxrkalYv4

Inaelezwa kuwa jiji la Mwanza bado halijafanikiwa katika kupambana na kuthibiti kuenea kwa ugonjwa wa kipindupindu jijini humo;https://youtu.be/Gx8kGFTDwhk

Chama cha wafugaji kanda ya ziwa kimeiomba serikali kuwatambua kuwa wao ni sekta muhimu inayoweza kuinua uchumi wa taifa kwa kulipa kodi;https://youtu.be/oWWETiAyKs8

Michuano ya ligi daraja la kwanza kwa msimu wa pili inatarajiwa kuanza kutimua vumbi ifikapo disemba 26. 2015; https://youtu.be/q38AKUz2OkQ
   
Baada ya Sepp Blatter na Michel Platin kufungiwa miaka 8 kutojihusisha na msaula ya soka, nchi ya Urusi imejitokeza kuwatetea na kusema kuwa Blatter na mwenzake hawajantendewa haki; https://youtu.be/XyGq0WjY3tA

No comments:

Post a Comment